Hello jamani hivi mtu akiwa anafanya mazoezi ya kuruka kamba yanasaidia kukata weight? Au tumbo. Please.
---Wewe unataka kufanya mazoezi au unataka kukata certain parts of the body?
Hakuna mazoezi ya sehemu moja kama hufanyi mazoezi ya mwili mzima.
Kamba ni mazoezi ya jumla kama kukimbia, unaongeza pumzi, unachoma calories zisizohitajika na unakuwa fit!
---Inasaidia sana, mimi hayo ni mazoezi yangu makubwa ,baada ya kumuona sister wangu alivyopungua kwa kuruka kamba.
Asubuhi kabla ya kula, kunywa maji ya uvugu vugu ,changanya na asali na mdalasini inasaidia.
Mwanzo kuruka ilikuwa ngumu mno, ila kwa sasa naruka mpaka mia kwa mkupuo.ila ni kazi.
Zoezi la urukaji kamba ni zuri sana kwa wale wenzangu na mimi tulio bize na kutafuta maisha. Wengi wetu tu wavivu kuamka asubuhi sana na kwenda mazoezini hasa ya kukimbia, lakini ukiwa kila siku unaruka kamba kwa usahihi walau kwa dakika 30, jua umempita mtu aliyekimbia kwa zaidi ya saa moja.
Kamba ina faida nyingi sana hasa kwa vibonge na kwa wale wanaotaka kuwa na mwili mzuri uliojengeka.
Njoo turuke kamba
Pia unashauriwa kusoma mada hii:
= > Mazoezi ya Ndani: Zoezi la kuruka kamba