Faida za kutembea bila viatu

Faida za kutembea bila viatu

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,780
Reaction score
8,155
Maisha ya miili yetu chimbuko lake ni ardhini(vumbi la nyota), viumbe na mimea tunayokula na maji tunayokunywa, vyote vina asili ya ardhini(udongo)

Ardhini kuna madini, chumvichumvi, antibiotics, antifugal na anti-viral chemicals. Udongo ni maisha na maisha ni udongo.

Je, unazifahamu faida za kutembea bila ya viatu, kushika na kuubusu udongo/ardhi?

Mitume yoote, manabii wote, wagunduzi na wafumbuzi woote wenye hadhi ya Issac Newton, Socrates, Avogadro, Eisten, Boyle, Archimedes na nk, mababu zetu, maaskofu, mapope, masheikh, walioandika vitabu vya dini kama Bibilia na Msahafu na wengine wengi ambao waliofanya mambo makubwa hapa duniani wote walikuwa mara nyingi wakitembea kwa miguu ardhini, kushika udogo na kuibusu ardhi kwa nyakati tofauti.

Magonjwa mengi kuanzia vidonda hadi upunguvu wa damu vilikuwa vikitibiwa kwa udongo. Hadi sasa wanyama, wadudu, ndege, samaki na mimea yote vinajipakaa mchanga/mchanga kwa sababu mbalimbali za kiafya kama sehemu ya matibabu.

Kwa binadamu:

👉FAIDA ZA KUTEMBEA PEKU

🔹 kunavuta sumu za mwilini kwenda ardhini kupitia vinyweleo/ndugu ndogo zilizoko kwenye ngozi. Uvutano wa dunia na mwili (gravitational forces), osmosis na sweating vinasaidia jambo hili kutokea.

🔹 mchanga unavuta harufu mbaya ya mwilini na kupotelea ardhini. mtu anayetembea peku hasumbuliwi na fangasi wala harufu mbaya ya soksi wala jasho baya.

🔹Mpapaso(massage) kati ya ardhini na nyao za miguu unasababisha msisimko wa tissue zote (misuli, neva, ubongo, mimeng'enyo na vichocheo mabali mbali vya mwili mzima kuimarika na kuwa madhubuti sana. Hii inasababisha viungo vyote hivi kufanya kazi kwa usahihi wake (use and disuse).

🔹 Kutembea peku ardhini (sio kwenye tiles,sakafu au lami) kunasawazisha uzalishaji na utoaji wa hormones mwilini, hali hii inaondoa msongo wa mawazo (stress free) hivyo kumfanya mtu awe mwenye furaha mara zote na kuweza kupata usingizi wa kweli na halisia. Usingizi wa aina hii unazifanya ndoto za mtu ziwe za kweli na zenye maana.

Ukitembea peku viungo vyote vinakuwa sensitized and alert,hata aliyekukosea ni rahisi kumsamehe bila masharti, maana ule mpapaso wa ardhi kwenye nyanyo unazalisha umeme mwingine kabisa utakaoleta seti nyingine ya kufikiria. Ardhi ina umeme na sumaku inayoweza kukubadilisha kabisa hata kinga yako ya mwili.

🔹Ardhi inaponyesha majeraha na michubuko kwenye ngozi, babu zetu walitibu vidonda kwa kuviweka mchanga tu basi. wakati mwingine udongo ni chakula, mama zetu wajawazito wanakula kuuongeza madini ya damu (iron) na yako makabila yanachanganya asali na udogo na kuwa sehemu ya chakula cha kawaida.

🔹Vijidudu vya ardhini vikiingia mwilini kwa kiwango kidogo vinasababisha kinga kubwa ya mwili dhidi ya magonywa mbalimabli.

🔹Kutembea bila viatu kwenye ardhi hasa ya moto wakati wa jua husaidia mzunguuko wa damu (perfusion) kwenye viungo vyote vya mwili, hivyo kuongeza uwezekano wa kuepuka kupata magonjwa ya figo, pressure, kisukali.n.k

🔹Kutembea peku ardhini kunakufanya uonje uhalisia wako wa kuwepo duniani. Yani hapa Kuna kitu kinaitwa umiliki,unajiona kutawala vyote vilivyokuzunguka na kufurahia uumbaji

🔹Kutembea peku hurahisisha ufunguaji wa chakra(magurudumu ya kinishati) ambayo hupelekea kukua kiroho hasa kwa yule anaefahamu kanuni hii ya kufunga,kuomba ukiwa unatembea PEKU.

Ukiulizwa taja faida za mtu Kutembea peku? mweleze hivi👇

1. Huimarisha afya ya mwili
2. Huimarisha afya ya akili
3. Hukuweka karibu na ulimwengu wa asili
4. Hurahisisha ufunguaji wa chakra
5. Huongeza muda wa miili kuishi
6. Huongeza ulinzi wa kiroho
7. Hukupa umiliki wa eneo

👉Kama ilivyo penye chanya hapakosi na hasi,zipo changamoto ndogo za mtu asievaa Viatu kuzipata kama kuchomwa na miiba,kugongwa na nyoka,funza,minyoo ya safura,kujikwaa,mavumbi .n.k lakini hizi ni changamoto ndogo ndogo mno ukilinganisha na faida nyingi za kifizikia na za kiroho ambazo mtu anazivuna kupitia Kutembea peku, wewe hapo ulipo anza sasa kutenga muda wa kukanyaga ardhi huku ukitembea angalau lisaa limoja ama masaa mawili kilasiku hakika magonjwa kama kuuma kwa miguu,ganzi ,kichwa,kizunguzungu,n.k vitatoweka haraka sana na utajikuta furaha Yako inaongezeka siku hadi siku

✍️
 

Attachments

  • FB_IMG_1745690642796.jpg
    FB_IMG_1745690642796.jpg
    8.4 KB · Views: 18
  • FB_IMG_1745690639743.jpg
    FB_IMG_1745690639743.jpg
    20.6 KB · Views: 22
  • FB_IMG_1745690636422.jpg
    FB_IMG_1745690636422.jpg
    23.5 KB · Views: 20
Back
Top Bottom