Faida za kupeleka majeshi yetu Congo DRC

Faida za kupeleka majeshi yetu Congo DRC

rugumye

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
561
Reaction score
179
Watanzania wenzangu hasara tuliyo pata kwa kuwatunza hawa wakimbizi kutoka Rwanda, Burundi na Congo ni kubwa sana, bahati mbaya wengi hamjafika katika kambi zao mkaona. misitu ambayo tungetumia kwa zaidi ya miaka 50 imetumika kwa muda wa miaka 5 tu. siraha walizoleta zinatumika kwenye ujambazi nchi nzima, ni bora tuwasaidie wapigane huko huko kwao ni siyo kukimbilia Tanzania. tufanye kama USA zero grazing.

Pili, jeshi letu litapata mbinu za kivita na mazoezi, tumekuwa tukijindanganya kuwa sisi ni bora east and central lakini tukajipime tuone uwezo wetu.

Tatu, wanajeshi wetu wana hamu ya vita kwani baadhi wanakaribia kustaafu bila kujua mlio wa risasi wa kifaru. matokeo yake wanaua raia kila wakati au kushirikiana na majambazi. wewe mtu unampeleka mafunzo mazito lakini hayatumii matokeo yake anaamua kupigana na aliye karibu nae. mfano juzi kawe askari wa jw waliua raia wao walijua ni simple kumbe adhabu ile hupewa mateka wa kivita. acha waende wakapate ozoefu pia nchi yetu itapat heshima kubwa.

Ni salamu kwa MSEVEN NA KAGAME wanaotaka himaya ya kitusti. wajue uwezo wetu. na hii hili litakuwa ni onyo kali kwao.

Tano: Congo ikiwa shwari tutafanya biashara na kukuza uchumi wa nchi yetu, kwaani wanatumia bandari yetu na baadhi ya bidhaa hununua Bongo usione kariakoo kuwa busy ukafiri ni wabongo tu, neda utawakuta akina mama wa kikongo wanafunga mizigo. ngano yao wanategemea AZAM, MFANO. kabla ya vita congo miaka ya Tz tulijenga tawi la BOT kigoma kwa kuwa kulikuwa na fedha nyingi za kigeni yaani US dola. lakini baada ya vita kongo majengo yale yamekuwa kumbi za miziki na ofisi za watu.


sita. Kabila mtoto wetu acheni tumsaide, najua kuna makubaliano hatuwezi kewnda tu kienyeji. kuna mlnago tutapata kitu kutoka kwa dogo kijana wetu kabila.

Tuwaombee vijana wetu warudi salama
 
Hizi sababu kama ingekuwa ni mtihani kwa mwl makini ungepata below pass marks
 
ah. kabila wanasema nduguye kabalege bosi wa majeshi rwanda. kuna watu wanaituhumu rwanda kuivuruga congo. kabila hawezi kwenda kinyume na rwanda lakini anaweza kwenda kinyume na tz. jwtz wakiwa genuine watakuwa na wakati mbaya congo. lets wait and see
 
ah. kabila wanasema nduguye kabalege bosi wa majeshi rwanda. kuna watu wanaituhumu rwanda kuivuruga congo. kabila hawezi kwenda kinyume na rwanda lakini anaweza kwenda kinyume na tz. jwtz wakiwa genuine watakuwa na wakati mbaya congo. lets wait and see

Ningekuambia lakini mambo mengine ni siri ya jeshi letu tukufua....ila usiishi kwa hisia...
 
Nadhani hatuendi kwa jina la Tanzania....ni kwa jina la UM...
 
tatizo la mihadarati ya kuchanganya na vinyesi
 
mwenye uelewa na mambo ya kijeshi atajua faida zilizopo maana nchi nyingi zinapenda kupeleka majeshi yao kwenye mission za umoja wa mataifa kwa kujua faida zake. lakini asiyejua mambo hayo ni sawa na kumsemesha kiswahili sanifu mtu anayejua lugha ya asili peke yake.
 
Back
Top Bottom