white wizard
JF-Expert Member
- May 18, 2011
- 8,618
- 13,896
Mkuu biashara ya hisa haiko hivyo kuwa akwambie eti baada ya mwaka mmoja utakuwa umetengeneza faida kiasi gani?!! Hiyo sio fixed deposit ambayo faida inajulikana!! Biashara ya hisa inatakiwa elimu ys kutosha sana kabla hujaingia kichwa kichwa!! Gawio linategemea na faida iliyopatikana kwa mwaka!! Mnaweza kaa miaka hata 4 hakuna gawio lolote lile!! Kila mwaka ni hasara tuVodacom tumbueni huyu marketing manager wenu hapo umemaliza kuainisha na kubainisha faida za ununuzi wa hisa vodacom?
Mbona umeacha maswali muhimu kama
Mpaka mwisho wa wiki hii hisa zimeuzwa na kununuliwa kwa shi ngapi?
Kwa trend ilivyo mtu akinunua labda tuseme hisa za milioni moja baada ya miezi sita au mwaka atatengeneza faida kiasi gani? N.k n.k
unaongea too technical,waweken watu wazi kua kampuni ikipata hasara hata miaka mi5 mfululizo bas hata na gawio kwa kipindi hicho chote hakuna.Mbona hicho hukizungumzii?eleza yote faida ni zipi 1,2,3 ....6,7 na hasara ni hizi 1,2,3,4,5,.....10 then mwananchi yeye ndio ataamua anunue au aache.Lakin sio kumwambia anunue then unamuorodheshea faida tu huku upande mwingine ukiuminya.Wengine tumekua tukiona watu waliowekeza kwenye hisa wakitegemea gawio wakiishia kunung'unika tu . sasa epukeni hicho kitu kwa kutoa elimu bora kabisa na sio bora elimu.Mbali na kuzungumzia suala la hisa leo, wajasiriamali wanashauriwa kusoma baadhi ya vitabu ambavyo waandishi wameandika mada mbalimbali za ujasiriamali ikiwamo uwekezaji katika hisa.
Tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 84 ya Watanzania wakiwamo wasomi na wengine ambao hawajabahatika kusoma hawajui au hawana elimu kuhusu kuwekeza katika hisa.
Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba mada hii haijawekwa katika mitaala mbalimbali ya elimu. Kama ipo basi wale wanaostahili kuifundisha ama hawana uelewa mpana na uzoefu wa kuwawezesha wanafunzi wao kufahamu umuhimu wake katika medani za kiuchumi.
Hisa inaelezeka kwa namna mbalimbali, kwa ujumla wake hisa ni mali, rasilimali, kitegauchumi, hati miliki, biashara, dhamana ya mkopo, ni akiba, ni fedha iliyohifadhiwa, na ni mtaji.
Katika mtazamo wa kibiashara, hisa ni uwekezaji wa mtaji au fedha ambayo imewekezwa na mfanyakazi, mkulima, mfanyabiashara au mtu mwingine ambaye ameamua kununua hisa kutoka katika kampuni fulani kwa lengo la kupata faida kupitia gawio na ongezeko la bei ya hisa husika.
Uwekezaji katika hisa kama biashara nyingine unahitaji umakini na upembuzi yakinifu. Kufanya upembuzi wa wapi uwekeze fedha zako na wapi ununue hisa kwa msingi wa kupata faida.
Mjasiriamali au watu wengine wanaweza kufanya upembuzi yakinifu, lakini kama watu makundi niliyoyataja hapo juu wana uelewa wa kutosha na mbinu za kusoma taarifa mbalimbali za kampuni ambayo unakusudia kununua hisa. Kwa mfano, unapaswa kufanya upepenuzi yakinifu wa taarifa za fedha na hali halisi ya kampuni husika.
Uwekezaji katika hisa unachangamoto zake ikiwzmo kushuka kwa bei ya hisa, kukosa gawio, mfumuko wa bei, viwango vya riba, kukosa wanunuzi kutokana na ukwasi na hitilafu mbalimbali.
Kwa hali ya kawaida uwekezaji katika hisa una faida nyingi kuliko changamoto kwa mfano, kupata gawio baada ya kampuni kutengeneza faida, ongezeko la thamani ya hisa, punguzo la kodi ya zuio kwenye gawio.
Katika masuala ya hisa, hakuna kodi kwenye ongezeko la thamani, urahisi wa kuuza na kununua hisa, na ukiwekeza katika hisa unapata muda wa kufanya shughuli nyingine. Kwa upande mwingine hisa ni dhamana ya kupata mkopo, hisa ni urithi mzuri, ukijiwekea utaratibu wa kutenga asilimia fulani ya pato lako kutoka kwenye mshahara ama biashara kwa ajili ya kununua hisa ni uamuzi mzuri, na hisa pia ni utajiri.
Nawashauri na kuwakaribisha kuwekeza na Vodacom
Tembelea ofisi za Vodacom kwa Maelezo zaidi.
[HASHTAG]#WekezaNaVodacom[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Tanzania[/HASHTAG]
Mfano mzuri kwa apa Tanzania.unaongea too technical,waweken watu wazi kua kampuni ikipata hasara hata miaka mi5 mfululizo bas hata na gawio kwa kipindi hicho chote hakuna.Mbona hicho hukizungumzii?eleza yote faida ni zipi 1,2,3 ....6,7 na hasara ni hizi 1,2,3,4,5,.....10 then mwananchi yeye ndio ataamua anunue au aache.Lakin sio kumwambia anunue then unamuorodheshea faida tu huku upande mwingine ukiuminya.Wengine tumekua tukiona watu waliowekeza kwenye hisa wakitegemea gawio wakiishia kunung'unika tu . sasa epukeni hicho kitu kwa kutoa elimu bora kabisa na sio bora elimu.
Mkuu inaonyesha una uelewa mkubwa na mambo ya hisa, kwa faida ya wengi hebu tupe tofauti ya ORDINARY na PREFERENCE shares, Faida na hasara ya kila moja pamoja na gharama za kila moja(Kama zinatofautiana).MKUU HIO 10% SIO HASARA KWA KAMPUNI,HIO NI BEI YA HISA KATIKA SOKO LA HISA MAANA HUA INAPANDA NA PIA HUA INASHUKA BEI KWA MAANA KUA UNAWEZA KUNUNUA HIZO HISA 100 LEO KWA (100 × 850 = 85,000/=)LAKINI BAADA YA MUDA FULANI BEI YA HISA SOKONI IKAPANDA HADI KUFIKIA 900 MAANA YAKE HAPA UKIUZA HISA ZAKO WEW UTAPATA FAIDA YA TSHS 50 KWA KILA HISA ILA PIA BEI YA HISA INAWEZA KUPUNGUA LABDA IKAWA 800 KWA HISA MAANA YAKE NI KUA UKIUZA HISA ZAKO KIPINDI HIKI UTAPATA HASARA YA TSHS.50 KWA HISA SASA HAYA MABADILIKO YA BEI YA HISA HAYAATHIRI GAWIO LAKO MWISHO WA MWAKA...GAWIO LAKO LITAASHIRIWA NA VARIABLES MBILI TU
1.FAIDA AU HASARA KATIKA BIASHARA ZA KAMPUNI AMBAZO ZITAASHIRI MAPATO YA KAMPUNI
2. AINA YA HISA UNAZOMILIKI.
SASA HAPA KWA MFANO MAPATO YA KAMPUNI BAADA YA KUFANYA BIASHARA KWA MWAKA MZIMA YAKIWA MADOGO KULIKO MATUMIZI MAANA YAKE KAMPUNI ITAKUA IMEPATA HASARA SASA KWENYE HALI HII WENYE HISA ZA AINA FULANI(PRERERENCE SHARES) WAO HAWATAATHIRIKA NA HASARA HII MAANA WAO GAWIO LAO LIKO FIXED KAMA SEHEMU YA EXPENSES ZA KAMPUNI YAN WAO WATAPATA GAWIO KAMA MTU ANAVYOPOKEA MSHAHARA VILE LAKINI WALE WENYE ORDINARY SHARES KWA SABABU KAMPUNI IMEPATA HASARA BASI HAWATAPATA GAWIO.
Nami nimeshangaa sana.Vodacom tumbueni huyu marketing manager wenu hapo umemaliza kuainisha na kubainisha faida za ununuzi wa hisa vodacom?
Mbona umeacha maswali muhimu kama
Mpaka mwisho wa wiki hii hisa zimeuzwa na kununuliwa kwa shi ngapi?
Kwa trend ilivyo mtu akinunua labda tuseme hisa za milioni moja baada ya miezi sita au mwaka atatengeneza faida kiasi gani? N.k n.k
Kutokana na waraka uliotolewa kila hisa itanunuliwa kw sh.850. Kwa mwaka 2017 kila hisa itazalisha sh. 28 ambayo ni 3% ya bei ya hisa na mwaka 2018 kila hisa itazalisha sh.42 ambayo ni 5% ya bei ya kununulia. Kwahiyo uamuzi ni wako.Ukiwekeza kwa kuweka hela yako ni kwa namna gani nitanufaika?
Kwa muda gani ntakuwa napata hio faida?
Hasa kama nimewekeza lets say 1 mil tshs
Tofauti kati ya hawa ordinary na Preference ipo katika nini hasa mbali na magawio yao....? Yani ni kiasi cha share wanazomiliki au...?ORDINARY SHARE ni umiliki wa Share katika kampuni ambapo shareholders watapewa gawiwo lao baada ya preferential shareholders kupewa gawiwo(DIVIDEND) lao.
Wamiliki wa ordinary shares/common shares huwa wanapewa kipaumbele kidogo au cha chini sana katika kupewa gawiwo. Hii inamaanisha kwamba kampuni ikipata faida wanaoanza kupewa gawiwo ni wale wanaomiliki wa preference shares halafu wanafuatia hawa wamiliki wa ordinary shares endapo tu gawiwo litabakia.
Wamiliki wa shea za kawaida(ORDINARY SHARES) katika kampuni huwa hawa kiwango dhahiri cha gawiwo lao. Hawa gawiwo lao hutolewa kulingana na DIRECTORS watakavyo amua.
PREFERENCE SHARES -ni umiliki wa shares ambapo preferential shareholders anapewa kipaumbele cha kwanza katika kupewa gawiwo.Hawa preferential shareholders wanapata gawiwo pale tu kampuni inapopata faida.
Katika Preference shares, hapa wana kiwango dhahiri cha gawiwo lao(Specific Dividend Rate).
Nielekezen namna ya kumiliki hisa
Biashara kichaa hii...Kwaio ikizalisha sh 28, na sh 42, 2018 faida ipo wapi hakuna biashara ya kijinga kama hii aiseee mfano 850 x 10,000 = 8,500,000 baada ya mwaka ambayo itakua kwa sh 42 nitakua na hisa yenye thamani ya 892 x 10,000 = 8,920,000 kwaio mwaka mzima unasubiria faida ya sh 492,000....
Tofauti kati ya hawa ordinary na Preference ipo katika nini hasa mbali na magawio yao....? Yani ni kiasi cha share wanazomiliki au...?
hakuna kitu kama hiki mkuu,inazalishaje jio 28 na 42?hivi hufatilii soko ls hisa kuona bei za jisa zinavyopanda na kushuka?unaweza kununua hisa kwa 850 na baada ya muda kutokana na ufanisi wa kampuni,bei ya hisa ikashuka hata hadi kufikia 500...watanzania wengi hili hawalijui,wao wanajua tu faida itapatikana kitu ambacho si kweli,khna hasara pia,unatakiwa jjue vyote viwili faida na hasara kuna kimoja wapo hua kitatokea.Sas ili bei ya hisa za kampuni zipande thaman yani kutoka 850 kuja 900,kuja 1000 na kuendelea kuna mambo ya kufanyika.Kutokana na waraka uliotolewa kila hisa itanunuliwa kw sh.850. Kwa mwaka 2017 kila hisa itazalisha sh. 28 ambayo ni 3% ya bei ya hisa na mwaka 2018 kila hisa itazalisha sh.42 ambayo ni 5% ya bei ya kununulia. Kwahiyo uamuzi ni wako.