Faida ya Siasa za Chuki na Fitna

Faida ya Siasa za Chuki na Fitna

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,198
Reaction score
7,536
Wadau,

Wapo ndugu zetu ambao wanadhani kwamba siasa bora, au siasa wanazoziweza ni siasa za chuki na fitna na hivyo wamewekeza sana kwenye eneo hilo.Ni vyema tukawekana sawa juu ya faida ya siasa hizo ili waliowekeza humo wawe wanafanya wakiwa na 'Informed Mind '

1. Siasa za chuki humfanya muhusika awe anapambana na watu badala ya kupambana na hoja (Concepts& arguments) kwa mtu yeyote anayefanya siasa kwa kusukumwa na chuki, hata ije hoja nzuri kiasi gani, haangalii hoja bali huangalia nani kaileta na kuanza kupambana naye.

2. Mfanya siasa za chuki huwa hana amani moyoni na wala hana uso wa tabasamu.Hii ni kutokana na roho ya visasi na nia mbaya ambavyo vinakuwa vinamsuta ndani yake. Hali hii humsababisha awe anaishi katika msongo wa mawazo wakati wote na kuwa na sura ama ya kuchukiza au ya kutisha.

3. Wanaowekeza katika siasa za chuki, hujikuta wakiwajibika kutumia mbinu yetote iwe halali au haramu kuwashinda wale wanaowachukia kitu ambacho wakati mwingine huleta madhara kwao wenyenye au kwa jamii nzima.

4. Wenye kufanya siasa za chuki, inapotokea wakashindwa katika uchaguzi, hu- panic kwa kuogopa uwezekano wa kulipiziwa visasi kwa kuwa huogopa kuwa huenda wakafanyiwa yale waliowafanyia wengine. Wakati mwingine huishia kukata tamaa na kuamua kujiua kama balozi wa Libya.

Kuna faida nyingi za siasa za aina hii nawe unaweza kuongezea.

Kwa ujumla tushauri tu kuwa, ni vyema tukafanya siasa tukiwa free minded na tukisukumwa na hoja pamoja na dhamira safi badala ya chuki. Hii itatuwezesha kuwa flexible pamoja na kuwa na amani (peace of mind) Ikionekana inafaa ni bora tukaziepuka siasa hizi.
 
Leo umeishiwa hoja za kuisifia ACT??
Siasa za chuki humfanya muhusika awe anapambana na watu badala ya kupambana na hoja (Concepts& arguments) kwa mtu yeyote anayefanya siasa kwa kusukumwa na chuki, hata ije hoja nzuri kiasi gani, haangalii hoja bali huangalia nani kaileta na kuanza kupambana naye.
 
Pole sana mdogo wangu, njaa zinakufanya uwe bendera fuata upepo, kila inapopigwa ngoma ukasikia mdundo unakolea ndiko unakoelekea.

Jiandae kuhamia tena chama kipya pindi kitakapoanzishwa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Pole sana mdogo wangu, njaa zinakufanya uwe bendera fuata upepo, kila inapopigwa ngoma ukasikia mdundo unakolea ndiko unakoelekea.

Jiandae kuhamia tena chama kipya pindi kitakapoanzishwa

Pole ndugu, mtoa mada ameeleza vizuri sana, kwa jinsi usivyo na akili unajibu upuuzi. Hizo ndio siasa za chuki. Bethlehem kaandika vizuri sana na wala hajamtaja mtu. Acha kutumika
 
kondoo wa zito wana shida sana inaelekea malisho yamekauka
 
kondoo wa zito wana shida sana inaelekea malisho yamekauka
Hii inakuwa je ninyi mnamuona zitto kwenye kila mada jamani? huyo zitto ana nini mnamwaza wakati wote hata kuacha kujadili mambo ya msingi na kumuwaza yeye tu?
 
Hii inakuwa je ninyi mnamuona zitto kwenye kila mada jamani? huyo zitto ana nini mnamwaza wakati wote hata kuacha kujadili mambo ya msingi na kumuwaza yeye tu?

wewe ni mfuasi wa zitto, usitufanye watoto
 
si kwamba anawazwa isipokuwa mnatumika vibaya
kwa sababu kama si beth ni doto na usipomwona doto yupo bokoaramu etc
 
Mtumwa wa Zitto leo umekuja na hadithi nyingine,

hii nchi wanasiasa wanawapelekapeleka wananchi kama wanavyotaka kwa sababu ya wajinga wajinga kama wewe. Chuki tu zimewaja wajinga nyie, mada nzuri imeandikwa ungepaswa kujenga hoja unaongea upuuzi tu.
 
Mkuu betlehem usikate tamaa endelea kuelimisha hawa wenye chuki za kijinga humu jf. Tafadhali sio wote ni baadhi tu.
 
Mkuu betlehem usikate tamaa endelea kuelimisha hawa wenye chuki za kijinga humu jf. Tafadhali sio wote ni baadhi tu.

Mkuu sorry, niliona kwenye comment moja ukiniuliza kwamba kwa nini nimepotea kitambo sana, kimsingi nipo sema majukumu tu ndio mengi.Tushirikiane kuijenga nchi yetu.
Asante.
 
Hauwezi kuwa na furaha au kuwafanya wengine wawe na furaha kama we we ni kiongozi mchafu kwenye siasa chafu, kama hauwezi kuwa na furaha wala kuwafurahisha wenzako, maisha yako hayawezi kuwa na dhamani
 
Ni vyema vijana ndani ya vyama vya siasa wakawa chachu na chimbuko LA mawazo chanya ndabi ya vyama vyao
 
Back
Top Bottom