Faida tatu za uvutaji wa sigara

Jay Mato

Member
Joined
Dec 17, 2014
Posts
69
Reaction score
6
Kulengana Na Utafiti Wa Dr Mwana Wa Visa Imebainika Kuna Faida Tatu Za Uvutaji Sigara. (1) MVUTAJI SIGARA HAWI MZEE: Inamaanisha Kila Anaevuta Sigara Hufa Akiwa Kijana Na Huwa Vigumu Kwake Kufika Uzeeni. (2) MVUTAJI SIGARA HAUMWI NA MBWA: Hili Halina Pingamizi, Kila Mvutaji Sigara Hudhuru Afya Yake Na Mwishowe Huwa Mchovu Hadi Akashindwa Kutembea Mpaka Apate Usaidizi Wa Bakora Anapo Jikongoja Njiani, Hapo Ndipo Mbwa Huogopa Hata Kumsogelea Maana Kashikilia Bakora. (3)NYUMBANI MWA MVUTAJI SIGARA HAKUINGII MWIZI: Bila Shaka Kifua Cha Mvutaji Sigara Hudhurika Akawa Kila Mara Anakohoa Na Kutema Tema Makohozi. Mwizi Anapojaribu Kuja Kumuibia Na Usiku Akifika Dirishani Jamaa Akianza Kukohoa Mwizi Atatimua Mbio Akijuwa Wazi Bado Jamaa Yule Hajalala. Hizo Ndio Faida Za Uvutaji Sigara, Ili Kuhakikisha Umenufaika Na Faida Hizi Hakikisha Umevuta Paketi Sita Za Sigara Kila Siku. Kila La Heri Katika Uvutaji Wenu Wa Sigara,,,, {WAKATABAHU: DR. Mwana Wa Visa}
 
unatafuta ugomvi na wavuta sigara eeh.,??
 
mvuta sigara huwa hasikii baridi kwas kila mda anawashasha moto mmbu wenyewe hawamsogelei kuumwa maleria kwake ni ndoto
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…