Faida na hasara za bodaboda

Faida na hasara za bodaboda

Ghaysh

Member
Joined
Feb 12, 2015
Posts
33
Reaction score
57
Habari zenu wakuu,

Mimi nikiwa kama kijana wa Tanzania na mmoja kati ya watumiaji wa usafiri wa pikipiki (Bodaboda) naomba niwasilishe maoni yangu yanayotokana na uzoefu kiasi nilioupata kuhusu usafiri wa Bodaboda.

Naomba nianze na upande wa faida zake, tukiangalia jiografia ya mji kama wa Dar es salaam swala la usafiri wa gari limekua ni changamoto kubwa sana kupelekea baadhi ya watu kutumia usafiri wa bodaboda na hiyo ni kutokana na mfumo wetu wa utafutaji kutegemea eneo moja, hivyo kusababisha watu wote tuwe tunaelekea katikati ya jiji nyakati za asubuhi na kutoka kwa pamoja nyakati za jioni. Kwa mtindo huu wa maisha ni ngumu kusafiri kwa kutumia usafiri wa gari pekee hasa ukizingatia ufinyu wa barabara za kuingilia katikati ya jiji.

Tukija upande wa madhara yatokanayo na usafiri wa bodaboda ni mengi sana na wengi wetu tunayafahamu ila naomba niyataje kwa uchache tu kama kuwakumbusha, nayo ni vifo , ulemavu wa kudumu n.k

Je, Bodaboda ni mbaya?
Jibu ni hapana usafiri wa boda boda sio mbaya ila mifumo ya usimamizi wa usafiri huu ndio ina kasoro mbalimbali zinazofanya uonekane mbaya.

Mfano ni kwamba mpaka sasa hakuna mfumo rasmi na rafiki wa kuwakagua madereva wa bodaboda kama wamekizi vigezo.

Nini kifanyike?
Maderva na vituo vya kazi.

Kwanza kuwe na usajili wa vituo rasmi vya bodaboda, madereva waende kupata mafunzo ya maalum ya uendeshaji salama. Kuwe na ukaguzi wa madereva pamoja na pikipiki katika vituo vyao vya kazi kwa yule asiyekizi vigezo asiruhusiwe kupakia abiria hadi pale atakaporekebisha kasoro zake.

Nguvu ya pikipiki
Nakazia hapa kwani ndiyo chanzo cha ajali nyingi
Pikipiki za kusafirishia abiria zisiwe na nguvu zaidi ya cc100.

Kwa sababu vigumu kupakia abiria zaidi ya mmoja(Mishikaki), kutembea mwendo mkubwa au kuovertake bila tahadhari ukiwa na pikipiki yenye cc100, hivyo hapo tutakua tumepunguza ajali zitokanayo na mwendo kasi pamoja na uzito kupita kiasi.
Pikipiki za bodaboda nyingi kwa sasa ni cc125-150.

Wajibu wa abiria
Kuhakikisha anapanda bodaboda kituoni.

Kuchagua dereva aliye smart( hakuna mstaarabu wa mambo anayevaa rafu.)

Kukataa kupanda abiria zaidi ya mmoja (mishikaki) kwa sababu udhibiti(control) wa chombo hupungua kwa dereva akipakia abiria zaidi ya mmoja, hivyo ni rahisi kwenu kupata ajali endapo itatokea dharura yoyote.

Naomba niwasilishe.
 
Back
Top Bottom