Kawaida ikiona kuna alama ya
NO EXIT kuingia humo lazima ufikiria mara mbili
Kitendo cha kutoa ahadi kwamba Hadi kifo kitakapotutengenisha ukweli binadamu unakuwa ume launch moja ya ahadi za pekee duniani.
No turning back, no escape route kulia au kushoto, wawili mnaingia kwenye life boat, hakuna kwa kwenda zaidi ya kubaki na huyo umemkubali.
Ukweli ni kwamba mtu mwenye akili timamu akiambiwa nyumba unayoingia haina
EXIT atafikiria kwa makini zaidi na zaidi ya mara mbili.
Kazi yako ipo well defined hakuna kutoka, hapa nazungumzia mtu ambaye kweli yupo serious kwanza kuhakikisha ndoa yake inampa Mungu utukufu na kwamba Kristo ni Bwana katika maisha yake.
Na kwamba suala la dini na imani ni muhimu sana kwake otherwise hakuna shida.
Mambo ambayo wakati mwingine huleta shida sana kwenye ndoa ni dini, rangi (
race) na taifa hata hivyo linaloweza kuwa mwiba mkali ni suala la dini.
General rule ni kwamba
The more couples have in common the better the chance of success
Ukweli unabaki palepale kwamba waumini wa kweli wa dini tofauti (
let say muislam wa swala tano na mkristo aliyeokoka) wakioana kuna uwezekano mkubwa kukumbwa na matatizo yanayohusiana na dini katika ndoa yao.
(
Najua ukianza kuzungumzia dini unaweza kuwasha moto ambao kuzima ni ngumu hata hivyo lazima kuongea ukweli)
Watu ambao hupuuza hiki kipengele baada ya kuoana wanayo ya kusimulia kwa masikitiko.
Jambo la msingi kabla ya kuoa au kuolewa ni vizuri kupata
solution ya suala la dini au suala la imani, usijidangany kwamba mkioana utanyoosha kwa pasi ya umeme kirahisi suala la hili la dini, hapa unahitaji kuwa genius tumia akili zako zote kuhakikisha umejua nini hatima yake.
Unaweza kuvuka mito mingi tu lakini mto wa dini ni lazima uvuke ukiwa makini kabisa maana unaweza kuzama mbele ya safari.
Je, mtasali wapi na kivipi, na watoto wakizaliwa watakuwa dini gani na dini ya mwenzako ina amini vipi kuhusu ndoa?
Ni maswali ya msingi sana.