Fahamu zaidi kuhusu huduma za afya

P2013

New Member
Jul 29, 2021
1
0
Maana ya Afya
Afya ni ukamilifu wa binadamu bila kuwa na magonjwa yoyote, binadamu aliyekamilika kumwili,kiakili,na kijamii pamoja na kuwa na nguvu za kufanya kazi bila wasiwasi wowote.

MAANA YA HUDUMA ZA AFYA YA MSINGI
Ni utaratibu unaoangazia Afya na uzima wa Jamii huduma hizo zikijikita kwenye mahitaji na matakwa ya watu binafsi, familia, na jamii. Hushughulikia maswala mapana yanayoelezea Afya na huangazia Hali kamili Na yenye mfano kuhusu Afya na uzima wa kimwili ,akili Na Jamii.

HUDUMA ZA AFYA YA MSINGI ULINWENGUNI KOTE
Huduma za Afya ya msingi inaweza kushughulikia mahitaji mengi ya afya ya mtu Katika Maisha yake yote ambayo Ni pamoja na kuzuia, kutibu matibabu ya kurekebisha na kutunza .
Zaidi ya watu bilioni 7.3 ulimwenguni bado hawapati huduma kamili na muhimu za Afya.
Kwa nchi 30 ambazo maelezo yake yanapatikana Ni 8 pekee ambazo hutumia angalau dola za Amerika 40, kwa kila mtu kwa huduma za kimsingi ya afya kwa mwaka

WHO
WHO imebuni tafsiri linganifu inayoegemea maswala matatu

1-Kutimiza mahitaji ya watu ya kiafya kupitia njia pana ya kuhimiza ,kulinda, kuzuia kutibu, kurekebisha, na kutunza Katika kipindi chote Cha maisha ,kwa kuzipa umuhimu huduma kuu za Afya zinazolenga watu,binafsi Na familia kupitia kwa matibabu ya kimsingi na watu kupitia kwa hafla za Afya ya Uma Kama maswala makuu ya huduma jumuishi za Afya .

2-Kushughulikia kwa mpangilio maswala mapana yanayoelekeza afya ( yakijumuisha ya kijamii, kiuchumi, mazingira, pamoja Na desturi za tabia za watu) kupitia sera thibitifu na fafanuzi ya Uma , pamoja Na hatua zilizochukuliwa Katika sekta zote.

3- Kuhamasisha watu binafsi ,familia na jamii kuimarisha afya yao, Kama watetezi wa sera zinazohimiza na kulinda Afya Na uzima, Kama washirika wenza wa kuendeleza Afya Na huduma za Afya za kijamii Na ili waweze kujitunza binafsi Na kuwatunza wengine.

AFYA KATIKA NCHI YETU YA TANZANIA
Serikali imeendelea kutoa kipaumbele Katika huduma za Afya zenye ubora na zinazowafikia wananchi wote ili kuboresha Afya zao.Serikali yetu inatambua umuhimu wa Afya Bora kwa wanachi wake kwani afya Bora Ni rasilimali muhimu kwa maendeleo. Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania yataletwa na wananchi wenye Afya Na wenye uwezo wa kuzalisha Mali.

MAZOEZI YA MWILI,FAIDA, NA JINSI YA KUFANYA MAZOEZI YA MWILI
Serikali yetu pia kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee Na Watoto , imeendelea kuwahimiza wananchi wake juu ya umuhimu wa kufanya mazoezi ili kujiepusha na magonjwa mbalimbali .

MAZOEZI KWA AJILI YA AFYA
Mazoezi Ni kitu ambacho wachache Sana wanakifahamu Katika dawa, au kuzuia maradhi , pamoja na kwamba binadamu tunatofautiana, wote tunahitaji kufanya mazoezi kwa ajili ya Afya zetu , mazoezi ya kila wakati yanatusaidia kujikinga na maradhi yakiwemo ya
Mshtuko wa Moyo
Kiharusi
High blood pressure
Kisukari
Unene
Magonjwa ya maungio ya mifupa na kuvunjika kwa mifupa
Mfadhaiko
Saratani za utumbo Mpana na za maziwa
Kukosa kumbukumbu.
Watu wazima wenye Afya, kwa ajili ya kuwa Na Afya nzuri, inashauriwa kwa Mtu mzima apate mazoezi yasiyopungua saa 2 Na nusu kwa wiki, mazoezi ya nguvu kiasi ya kuongeza mapigo ya Moyo - moderate intensity aerobic activity, au upate mazoezi ya nguvu ya kuongeza mapigo ya Moyo ( aerobic activity) yasiyopungua saa 1 na robo kwa wiki au mchanganyiko wa mazoezi ya nguvu Na ya nguvu kiasi .

Aerobic exercise Ni mazoezi yanayofanya mapigo ya Moyo kufikia asilimia 70 Hadi 80 ya kikomo Cha mapigo yake, Lakini watu wengi huhitaji zaidi ya saa 2 Na nusu kwa wiki, ili kuweka miili Yao kwenye uzito unaotakiwa.
Kama unafanya mazoezi ili kupunguza unene wa mwili dakika 30 kila siku zitakusaidia zikiambatana Na mlo kamili.

MWUSHO, TUANGALIE VIRUSI VYA CORONA ( COVID-19 ) KATIKA NCHI YETU TANZANIA
Virusi vya Corona Covid-19 Ni mlipuko mpya uliogundulika mwaka 2019 na haikuwahi kubainika Hapo kabla miongoni mwa binadamu .

Dalili zake Ni pamoja Na homa, kikohozi, shida Katika kupumua Katika Hali ngumu zaidi , maambukizi yanayoweza kusababisha nimonia, kukosa pumzi, kushindwa kufanya Kazi kwa Figo Na hata kifo

Jinsi ya kujikinga na kujilinda Na Virusi vya Corona Covid-19 Katika nchi yetu Tanzania.
Tunashauriwa kufanya yafuatayo
  • Kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima
  • Kunawa mikono Mara kwa Mara kwa kutumia sabuni Na maji tiririka , Na kuepuka kusalimiana kwa kutumia mikono
  • Kuvaa barakoa unapokuwa kwenye ufasiri wa Uma, unapokuwa kwenye mikusanyiko
  • Kuboresha Afya zetu kwa kufanya mazoezi Mara kwa Mara Kama nilivyoeleza Hapo awali.
  • Kuzingatia social distance.
  • Mwisho tuzingatie maelekezo yanayoendelea kutolewa Na wataalamu juu ya afya zetu.
 
Back
Top Bottom