The Consult
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 220
- 252
Kuna njia nyingi za kupata fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi; aina ya njia itumikayo kwa kiasi kikubwa hutegeme;
· Kiasi cha pesa unachohitaji kwa ajili ya kutekelezea mradi wako (Financial need)
· Rasilimali ulizonazo (Available resources)
· Uzoefu wako katika mchakato wa kutafuta fedha (Experience in fundraising)
Ni vyema ukafahamu kwamba shughuli ya utafutaji wa fedha kwa ajili ya mradi ni shirikishi, hivyo unapaswa kushirikiana na viongozi wa Taasisi yako pia na wafanyakazi wenzako. Utafutaji wa fedha wakati mwingine unakuwa na changamoto, kwa mfano unaweza kupeleka ombi kwa mfadhili na asikujibu, kutojibiwa kusikufanye ukasitisha zoezi, jitahidi kujiuliza/kutafuta sababu za kukutaliwa kwa ombi lako kisha rekebisha kasoro au tumia njia/chanzo kingine.
Miongoni mwa vyanzo vya ukusanyaji wa fedha kwa ajili ya mradi wako ni;
Utafutaji fedha kupitia mitandaoni (Crowdfunding), hii ni njia mpya ambayo imeanza kutumika hivi karibuni, na watumiaji wakubwa ni taasisi za kati, na pia mtu mmoja mmoja. Kuna tovuti maalum kwa ajili ya kukusanyia fedha kwa njia hii ambazo ni Indiegogo: From concept to market with crowdfunding , RocketHub - Faster Forward, Together, Kickstarter , Fundraising Website - Raise Money Online For Causes & Charities - CrowdRise n.k Tovuti hizi zinakupa nafasi ya kutengeneza wasifu wako (profile), kisha unaweka dhumuni lako la ukusanyaji wa fedha (Fundraising goal) kisha unatangaza wazo lako. Kumbuka kwamba njia hii itakuwa na msaada mkubwa endapo utahusisha mitandao ya kijamii, hivyo ni vyema uka-share wazo lako pia kupitia Facebook, Twitter n.k
Ufanyaji wa matamasha/matukio (Organizing events), matamasha kwa kiasi kikubwa yanasaidia kujenga mahusiano na wafadhili na hata wanajamii ambako mradi/Taasisi yako inajikita kishughuli. Kuna aina mbalimbali za matukio (events) ambazo huweza kutumika katika kutangaza wazo lako la mradi; kwa mfano matembezi ya hisani (sponsored walk), chakula cha usiku cha jumuia (Community dinner event/Tea party) n.k
Uombaji kwa kutumia andiko la mradi (Fundraising through grant proposal). Taasisi binafsi (private foundations), mashirika ya kimataifa (multi-lateral organizations) na serikali mara nyingi hutoa fedha kwa ajili yautekelezaji wa mradi kupitia andiko la mradi (proposal) Kabla ya kuziendea hizi taasisi ni vyema ukafahamu kwanza vigezo vyao (criteria)na taratibu zao za uomabji wa fedha (guidelines). La kuzingatia zaidi katika utafutaji wa fedha kwa njia hii; ni kuwa na andiko lenye ubora.
Chanzo cha pesa kutoka kwako mwenyewe (Fund from your own), kabla hujawafuata wafadhili ni vyema ukajiuliza Ni kwa kiasi gani umechangia mradi husika?, hii itakuwezesha kujiamini katika kumfuata mfadhili. Mara nyingi wafadhili hupenda kufadhili mradi ambao mhusika/wahusika wametoa mchango wao.
Kukusanya pesa kutoka kwa watu (Solicit money from individuals) Kabla ya kuwafuata watu; angalia/zingatia kwanza “interests” zao kama zinaendana na lengo la mradi wako, pia angalia uwezo wao wa kuchangia, kwa mfano huwezi ukamfuata Mr X afadhili mradi wako uliojikita katika masuala ya kilimo wakati “interest” yake ipo katika kusaidia watoto yatima. Ili kufanikisha hili, inakupasa kutumia muda mwingi kukaa na hawa watu ili kujua “ interests” zao na kuweza kuwauzia wazo lako la mradi.
The Consult ; +255 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania