Fahamu mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia ili kunenepa au kuongeza uzito wa mwili (Kilo)

stevoh

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
2,921
1,104


BAADHI YA MASWALIYALIYOULIZWA KUHUSU JAMBO HILI
Wadau jamani mimi najiona nimekonda nataka kunenepa kiasi flani hivi embu naombeni ushauri wenu''
---
---

UFAFANUZI WA JUMLA WA JAMBO HILI

JINSI YA KUONGEZA UZITO AU UNENE BILA KUDHURU MWILI WAKO
Kama unataka kuongeza uzito na unene basi ni mhimu kwamba unafanya jambo hili kwa njia salama ambazo hazitakuletea madhara baadaye.

Kunywa soda, kula maandazi au chipsi za vibandani ni vitu vinaweza kukuongezea uzito na unene kwa haraka lakini wakati huo huo vinaweza kuharibu afya yako.

Kama uzito wako upo chini ni mhimu kuzingatia umhimu wa kuongeza uzito sambamba na misuli na siyo kuongezeka uzito pamoja na tumbo au kitambi.

Wapo watu wengi tu wenye uzito sawa na bado wanaugua kisukari aina ya pili, ugonjwa wa moyo na matatizo mengine ya kiafya yanayohusiana na uzito kuwa juu.

Hivyo ni mhimu kwamba bado unaendelea kula vyakula vyenye afya na kuishi maisha yenye afya kila siku.

Tuangalie sasa njia za kuongeza uzito na unene kwa haraka bila kuharibu afya yako:

1. KULA ZAIDI
Jambo la mhimu unaloweza kulifanya ili kuongeza uzito ni kula zaidi ya unavyohitaji mwili wako. Bila hivi ni vigumu kuongezeka uzito.

Kama ulikuwa unakula mara 2 au 3 kwa siku sasa anza kula mpaka mara 5 kwa siku. Muda wote tumbo liwe limejaa. Siyo kiasi cha kuwa kero lakini kuwa makini.

2. KULA ZAIDI VYAKULA VYENYE PROTINI
Lishe moja mhimu zaidi katika kuongeza uzito ni ile yenye protini kwa wingi ndani yake.

Mishipa inatengenezwa na protini na bila kuwa na protini ya kutosha sehemu kubwa ya nishati ya mwili huishia kuwa mafuta.

Tafiti zinaonyesha kuwa wakati unaongeza kiasi cha chakula unachokula, lishe yenye protini nyingi kile kiasi kinachozidi huweza kubadilishwa na kuwa misuli ya mwili.

Hata hivyo elewa hili tena, chakula chohcote chenye protini nyingi huwa na uwezo wa kukupunguzia njaa au hamu ya kutaka kula chakula.

Hili linaweza kukuletea shida tena kuendelea kula zaidi kama moja ya mahitaji mhimu ili kuongeza uzito na unene kwa ujumla.

Hivyo wakati ukiendelea na lishe yenye protini ni mhimu pia kuongeza mbinu za kuongeza njaa ili uendelee kula zaidi.

Vyakula vyenye protini kwa wingi vinajumuisha nyama, mayai (mayai ya kienyeji) maziwa freshi, karanga, mbegu za maboga (kama unahitaji mbegu za maboga zilizokaangwa tayari kwa matumizi niachie ujumbe WhatsApp +255769142586), samaki, korosho nk.

Hivyo protini ni mhimu ili kutengeneza misuli na mishipa kwa ujumla, kula protini ya kutosha ni mhimu ili kuongezeka uzito unaobaki kama misuli na siyo mafuta.

3. KULA ZAIDI WANGA NA MAFUTA
Kula kwa wingi vyakula vyenye wanga na mafuta kama shida yako ni kuongezeka uzito na unene. Ni vizuri katika mlo ule vya kutosha vyakula vyenye wanga, mafuta na protini kwa matokeo mazuri zaidi.

Vyakula vyenye wanga kwa wingi ni pamoja na viazi vitamu, ugali wa dona, wali, mkate, chapati, maandazi, tambi (pasta), maembe, viazi mviringo (chipsi), ndizi, tende, pizza, nk.

Mafuta mazuri yanapatikana katika parachichi na mafuta yake, mafuta ya zeituni, siagi ya karanga, mayai, mafuta ya samaki, mafuta ya nazi, mafuta ya mawese, ufuta na mafuta yake nk.

Hakikisha unakula mara 3 mpaka 5 kila siku mlo wa aina hii.

4. KULA VYAKULA VYENYE NGUVU ZAIDI
Ni mhimu tena kula vyakula vya asili zaidi na vyenye nguvu zaidi. Kama ni ugali kula ugali wa dona na si sembe, kama ni mkate kula mkate wa unga wa ngano ambayo haijakobolewa.

Kwa kifupi tu usile vyakula vilivyokobolewa au vya madukani kama unataka kuongezeka uzito na unene kwa njia salama kwa afya yako.

Pia ongeza viungo zaidi kwenye hivyo vyakula ili kuongeza hamu ya kutaka kula zaidi. Ongeza iliki au mdalasini na viungo vingine vitakavyokufanya upende kula zaidi hicho chakula.

Kula zaidi vyakula hivi kwa kupata nguvu zaidi; lozi, jozi, korosho, karanga, tende, zabibu kavu, maziwa freshi, mtindi, mafuta ya zeituni, parachichi, nyama ya kuku wa kienyeji, nyama ya ng’ombe, nyama ya nguruwe, nyama ya mbuzi, viazi, viazi vitamu, siagi ya karanga nk.

Vingi ya hivi vyakula vina kawaida ya kukupotezea njaa na hamu ya kula hivyo itakulazimu wakati mwingine kujilazimisha tu ili ule zaidi kwa siku.

Pia siyo wazo zuri kula sana mboga za majani kama shida yako ni kuongeza uzito hii ni kwa sababu zitaziba nafasi inayohitajika kukaliwa na vyakula hivi vyenye nguvu zaidi. Pia matunda iwe kidogo labda tunda moja tu hasa parachichi au ndizi moja tu basi.

5. NYANYUA VITU VIZITO
Ili kujihakikishia kuwa hicho kiasi cha chakula ulichoongeza kula kinakwenda kwenye misuli na si kukuletea mafuta na pengine tumbo au kitambi ni mhimu ufanye mazoezi ya kunyanyua vitu vizito.

Nenda gym na unyanyuwe vyuma mara 3 mpaka 4 kwa wiki, anza na uzito mdogo na uongeze uzito kidogo kidogo kadri unavyoendelea.

Kama shepu yako ipo nje kabisa yaani haieleweki ni vizuri ukafanya mazoezi hayo ukiwa na mwalimu wa kukuelekeza kwa matokeo mazuri zaidi.

Ni vizuri pia kuonana na daktari kama una tatizo lolote la uti wa mgongo au mifupa kwa ujumla kwa ushauri mzuri zaidi kabla hujaanza mazoezi haya.

MAMBO MENGINE 10 MHIMU ZAIDI
Pamoja na mbinu tano hizo hapo juu, ni mhimu kuzingatia yafuatayo kwa matokeo mazuri zaidi na ya haraka:


1. USINYWE MAJI KABLA YA KULA. Kunywa maji kabla ya kula kutafanya tumbo lako liwe limejaa na hivyo kuziba nafasi ya chakula ambacho ndiyo mhimu kwa ajili ya kalori zinazohitajika ili uongezeke.

2. PATA USINGIZI WA KUTOSHA. Kupata usingizi wa kutosha na mtulivu kila siku ni mhimu ili uweze kunenepa na kuongeza uzito na kukua kwa misuli, tena ukiweza lala nyakati za mchana masaa mawili.


3. KULA MBOGA ZA MAJANI MWISHONI. Kama unapokula utakuwa na mboga za majani pia basi hizi ule mwishoni baada ya kuwa umekula protini, wanga na mafuta na hii inaenda pia kwa matunda.


4. ACHA SIGARA. Wavutaji wengi huwa na uzito pungufu, acha kuvuta sigara pia bangi na tumbaku yoyote. Mara nyingi ukiacha tu kuvuta utaona afya yako inaimarika na kuongezeka sana.

5. RIDHIKA. Kama unataka kunenepa na kuongezeka uzito basi uwe mtu wa kuridhika.

Nikuambie tu maisha ndiyo haya haya na furaha ya kweli haipo kwenye mali, usisubiri mpaka uwe tajiri ndiyo uwe na furaha, kila siku ukiamka salama shukuru Mungu ni neema tu na zawadi umeamka salama.

Kumbuka tulikuja watupu na hakuna tutakachoondoka nacho.

KONGEZEKA UZITO LINAWEZA KUWA SIYO JAMBO RAHISI KWA WENGINE
Hii inaweza kuwa ni kwa sababu baadhi ya watu miili yao inaweza kuwa imejiwekea kikomo fulani cha uzito wa kuubeba ambapo hujisikia vizuri zaidi katika uzito huo kuliko zaidi.

Utakapojaribu kwenda juu au chini kidogo ya kiwango hicho cha uzito ambao mwili wako umejiamulia utaona tu njaa yako inapunguzwa au kuongezwa pia mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula nao utawekwa sawa ili kusiwepo na kuongezeka wala kupungua kwa mwili wako.

Utakapojaribu kula zaidi tegemea mwili wako kukupunguzia hamu ya kutaka kula na kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, hili hufanywa na ubongo wenyewe ukisaidiwa na homoni ijulikanayo kama ‘leptin’.

Kwahiyo tegemea kazi hii kuwa siyo rahisi kwa baadhi ya watu na hivyo ni mhimu kujilazimisha zaidi ili kufikia lengo lako.

Mwisho wa siku jambo hili linahitaji muda na siyo jambo la siku 2 au 3 hata hivyo ukiwa na nia hakuna linaloshindikana.

BAADHI YA MAONI NA USHAURI KUTOKA KWA WADAU WA JF
---
Asubuhi kunywa chai maziwa na sukari, mkate uliopakwa butter na jam mayai ya kukaanga (kama utaweza). Mchana ugali nyama au wali nyama. Usiku kiepe na mirinda ya baridi. Bila kusahau matunda na Mbita mboga pamoja na kunywa maji,
---
---
---
---
---
---
---
 
wadau jamani mimi najiona nimekonda nataka kunenepa kiasi flani hivi embu naombeni ushauri wenu''

Shinikizo la shemeji? ukiongozana naye unaonekana kama houseboy? unakunywa bia? jibu hayo nikusaidie fasta fasta.
 
Dawa ya kunenepa ni kula bila mpangilio yaani usiruhusu utumbo uake na bila chakula,kila kipitacho mbele yako kula au kunywa ,utakuja kuniambia.....
Tahadhari,kunenepa ni rahisi kliko kukonda
 
Ni kweli Stevoh inatakiwa mtu uzito wake uendane na kimo chake kiafya. Kama wewe umeshafanya vipimo na ukashauriwa kuongeza uzito ni muhimu sana kwa ajili ya afya. Mimi ninazo products zilizoandaliwa kiasilia na zisizo na kemikali kwa ajili ya kuongeza uzito na afya njema. Ukihitaji unaweza kuniandikia kwa email: healthwealthfirst@gmail.com pia waweza kunipigia kwa namba 0713889162
 
Kapime ngoma kwanza ili uwe na uhakika kwamba huko kukonda si matokeo ya maradhi, baada ya hapo ndiyo utafute ushauri wa jinsi ya kunenepa.

kunenepa na ngoma vitu viwilitofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…