Fahamu mambo ya kujenga heshima kwa jamii

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
51,741
68,633
Hakuna ubishi wowote, heshima ni moja ya kitu ambacho karibu kila mtu anakitafuta katika maisha yake. Hakuna mtu ambaye hataki asiwe wa kuheshimika, heshima inatafutwa na watu wengi sana.

Ndio maana utakuta kuna watu wanatumia pesa au mbinu nyingi sana kuweza kujenga heshima. Hali hiyo yote inaonyesha kwamba heshima ni mojawapo ya kitu cha thamani na kinachokubalika sana katika jamii yoyote ile.

Pamoja na umuhimu wa heshima kwa wengi, sasa kitu ambacho tunatakiwa tujiulize mimi na wewe ni kwamba, je, kati yetu ni wangapi hasa wanajua namna ya kujenga heshima zao katika jamii?
Je, pesa peke yake ndio ina uwezo wa kujenga heshima? Au ni kitu gani ambacho unatakiwa uwe nacho ili kikusaifdie kuweza kujenga heshima kubwa katika jamii na kujikuta ukikumbukwa pengine vizazi na vizazi?

Kama nia yako ni kutaka kujenga heshima na ukawa mtu wa kuheshimika, fahamu mambo haya;-

1. Toa thamani.

Ili uweze kujenga heshima kubwa kwa jamii inayokuzunguka, toa thamani, fanya vitu ambavyo vinagusa maisha ya watu. Haijalishi unafanya kitu gani lakini lilokubwa fanya kitu ambcho kinagusa maisha ya watu, kina mchango wa kubadili maisha ya wengine.

Siku zote haijalishi una pesa za kiasi gani, lakini je, kupitia hizo pesa wewe binafsi unatoa mchango gani kwa wengine kufanya maisha ya yakabadilika? Watu wote wanaotoa thamani na kuweza kubadili maisha ya wengine ni watu wa kuheshimika.

Kama unafikiri natania kuhusu hili angalia watu waliokuwa wakipagania uhuru, heshima zao zikoje katika jamii zao, utagudua heshima zao ni kubwa sana. Hivyo hiyo inatuonyesha njia mojawapo ya kujiwekea heshima toa thamani kwa kugusa maisha ya watu.

2. Wakubali watu.

Mbali na kutoa thamani, njia mojawapo nyingine ambayo inaweza kukujengea heshima ni kuwakubali watu. Kubali mawazo yao wanayotoa ila kama kweli yanasaidia kujenga jamii au kuwasaidia wengine.

Kama unahitaji kuwakosoa, tafadhari usiwakosoe hadharani, jitahidi ukosoe kwa pembeni. Hiyo pia ni njia nzuri ya kukusaidia kujua au kutambua kwamba yapo makosa ambayo umeyaona na ni muhimu kurekebishwa.

3. Unapokosea, omba msamaha.

Hakuna mtu ambaye tunaweza tukasema yupo kamili kwa asilimia zote. Hivyo, unapokosea iwe kwa jamii yako au kwa watu wako wa karibu, hebu kuwa mwepesi wa kuomba msamaha.

Msamaha ni kitu kidogo sana lakini utakusaidia kukujengea picha kwa watu wengine kwamba una busara. Kwa sababu ya busara zako utajikuta ukiwa ni mtu wa kuheshimika karibu na watu wote.

4. Usijifanye unajua kila kitu (Mjuaji)

Katika jamii yetu kuna watu baadhi wanajifanya kila kitu wanajua yaani kwenye nyanja zote wao wapo, iwe siasa, afya, michezo, uchumi, mapenzi, teknolojia n.k.. Ni vyema kitu ambacho hukijui ukauliza ufahamishwe kuliko kujifanya unajuajua tu. Hii itakutengenezea heshima katika jamii kuliko yule ambaye anajifanya kila kitu yeye ni mtaalamu..Zingatia hili sana kama unataka uheshimike.

Hizi ni mbinu muhimu ambazo mtu yoyote anayataka kuheshimika katika jamii yake anaweza akazitumia kama njia mojawapo ya kumsaidia kumjengea heshima kubwa katika jamii yake.

Kama kuna mbinu nyingine unaweza kuongezea..Karibuni



Credits: Jicholetudotcom & Myself
 
Hakuna mtu ambaye hataki asiwe wa kuheshimika

Dah mkuu nilitaka nikae mimi hapa kwenye siti ya pili umekaa wewe mtoa mada tena,anyway sio kesi.
kuhusiana na uzi,naamini kuna wachache ambao hawathamini heshima nadhani umewahi kuwaona watu wa namna hii hawajali lolote wao ili mradi wanaishi hawana tabu.Hawathamini heshima katika namna ambayo haiko direct,ujinga wao ndio unaowafanya wasistahili heshima na wanajijua kwamba ni wajinga,
Imagine mtu mgomvi,mmbeya,mnafiki,malaya na wengineo wanajua hizi tabia zinatosha jamii kukudharau lakini wao hawana habari hivo wanakuwa wanakataa heshima

Kuna sehemu imenenwa HESHIMA HAIMPASI MPUMBAVU
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom