Fahamu Malengo Mahsusi ya Mradi (Project Objectives)

Fahamu Malengo Mahsusi ya Mradi (Project Objectives)

The Consult

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2017
Posts
220
Reaction score
252
1552643023658.png

Uandaaji wa malengo mahsusi ya mradi yaani " project objectives" ni hatua ya awali kabisa katika uibuaji wa mradi (project planning). Malengo mahsusi ya mradi ni matokeo shikika/onekana yanayotarajiwa pindi mradi unapokamilika (expected tangible result or end product). Malengo haya huweza kuwa kwa ajili ya miradi itekelezwayo na serikali, kampuni za kibiashara na asasi za kiraia. Malengo mahsusi ya mradi ni lazima yafafanuliwe vizuri (should be well defined) na kukubalika kwa wana timu ya mradi. Malengo ya mradi ni lazima yawe na sifa zifuatazo;
  • Uhalisia (relevant); yanaendana na lengo mama la taasisi (align with overall organization goal)?
  • Timilizika (achivable); upatikanaji wa rasilimali (watu, fedha na vifaa) katika utekelezaji wa mradi huo.
  • Mahsusi (specific); yanapaswa kuonyesha nani atafanya nini( Who), kwanini atafanya (why) atafanyaje (How) atafanya wapi (Where) atafanya lini (When)
  • Pimika (measurable); yanapaswa kuonyesha vipimo vya muda na kiwango
Mradi unaweza ukawa na lengo moja tu, au mawili au zaidi, malengo haya hutafsiriwa kiuwanda (in terms of scope), kiratiba (in terms of schedule) na kigharama (interms of cost) kwa maana ya kwamba; ni lazima malengo haya yaonyeshe kuwa mradi utamalizika kwa gharama maalum na ndani ya muda maalum, kwa mfano; "Kupeleka sokoni jiko la kisasa la kupikia chakula litumialo umeme ndani ya kipindi cha miezi 10, kwa kutumia kiasi cha shilingi Milioni 35 ambalo litakidhi vigezo vya ubora."

Lengo mahsusi kama " kumaliza ujenzi wa nyumba" ni pana sana na tatanishi (ambiguous); kwa sababu mteja na mhandisi wanaweza wakawa na mtazamo tofauti juu ya dhana ya "kumaliza ujenzi wa nyumba" hivyo ili lengo hili kuwa katika ubora ni vyema lisomeke "Kukamilisha ujenzi wa nyumba eneo la Mikocheni ifikapo May 2020 kwa kutumia bajeti ya shilingi milioni 120 kwa kufuata mchoro na viwango vya ubora vilivyoainishwa kwenye makubaliano"

Malengo mahsusi ya mradi ni lazima yawe sahihi (clear); ijapokuwa kuna kipindi malengo ya mradi hubadilishwa/boreshwa baada ya mradi kuanza. Mabadiliko ya malengo mahsusi ya mradi yanapaswa kuwasilishwa na kukubalika kwa pande zote mbili yaani watekelezaji wa mradi na watoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.
FAHAMU KWAMBA; mabadiliko yoyote katika malengo ya mradi yanaathiri uwanda wa mradi (project scope), ratiba (project schedule) na gharama (project cost)

KUSHINDWA KUTENGENEZA MALENGO MAHSUSI YA MRADI KWA USAHIHI, HUPEKLEKEA MRADI WAKO KUWEKWA PEMBENI

Kabla ya fedha/ruzuku kutolewa, maandiko yote yaliyowasilishwa hupitiwa/huchambuliwa; mchakato huu hujulikana kama "Project Evaluation" Kila mfadhili ana taratibu na vigezo vyake katika kuchambua maandiko ili kupata yaliyo bora. Miongoni mwa vigezo vinavyozingatiwa na wafadhili wengi ni pamoja na uzoefu wa muombaji (experience), kukidhi matakwa (compliance) na namna andiko lilivyoandaliwa; hapa kwa kiasi kikubwa huangaliwa malengo mahsusi, ikiwa hayajatayarishwa vizuri ni rahisi andiko lako kuwekwa pembeni; kwa sababu mkanganyiko katika malengo mahsusi hupelekea mradi kutofanikiwa (project failure)


The Consult: +255 719 518 367
E-mail ; theconsult38@gmail.com
Dar es Salaam
Tanzania

Home of Project Management, Strategic Planning and Fundraising Strategy
 
Back
Top Bottom