Fahamu majina usiyoyajua

MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
16,947
10,498
1. KOLOMIJE.

Inasemekana mahali hapo alifika Mzungu aliyeitwa James, hivyo huyu Mzungu akataka watu wamwiite "J" badala ya kutamka jina lote. Hivyo akawaambia CALL ME J, wabantu wakatamka KOLOMIJE na kutengeneza jina la eneo hilo.

2. KARIAKOO

Hii ilitokana na neno #Carrier_crop ambalo lilikuwa ni jina la wabeba mizigo wa eneo hilo la sokoni, lakini Waswahili walishindwa kulitamka jina hilo hivyo wakasababisha kutokea kwa jina la Kariakoo.

3. MSASANI.

Hili jina lililotokana na Bwana mmoja aliyeitwa Musa Hassan ambaye alikuwa ni Mnyapara aliyekuwa akisimamia mashamba ya katani ambaye asili yake ni Ntwala, wamakonde wengi wakaamua kuja kumuomba kazi na kwa kwa kuwa walikuwa hawajui anapoishi waliuliza kwa Mucha Hachani, na wakaendelea kuunga unga mpaka kusababisha kutokea kwa jina la Msasani.

4. KAWE.

Hili lilitokana na neno #Cow_Way, barabara maarufu kwa kusagwa ng'ombe kufikishwa hapo Tangaynyika Packers kwa machinjo.

5. KIGOGO

Ilitokana na kigogo halisi kabisa cha kuvuka pale kigogo mwisho kila jumamosi walikuwa wanakusanyika kukiweka "jamani leo siku ya kigogo" (leo pamejengwa daraja).

6. TABATA

Palikuwa na Muarabu aliyekuwa ananunua korosho kwa mali kauli na kuwaahidi wachuuzi waje siku fulani watalipwa kwa kuwaambi "hapana tabu tabata (utapata pesa yako) akabatizwa jina la Mwarabau Tabata, na mwishowe mahali hapo napo pakaanza kuitwa Tabata.

7. ILALA

Jina hili linatokana na makaburi ya pale Karume ambako hakukua na mengine hivyo kila alasiri watu walikuwa wakienda kuzika na wimbo wa Haila Illallah! na mwishowe mahala hapo pakaanza kuitwa Ilala.

8. UBUNGO

Majina yafuatayo: bungoni, mikoroshini, na mabibo yote haya yalitokana na uwepo wa miti mingi ya matunda hayo kupatikana maeneo hayo.

9. KIBORILONI

Kiboriloni ni neno lililotokana na maneno mawili KIBO na ALONE. Hii ilikuwa sehemu ambapo wazungu walisimama na kuona kilele cha Kibo pekee bila kukiona kilele cha Mawenzi, Kibo na Mawenzi ni vilele vya Mt. Kilimanjaro.

10. KIBOSHO

Lilitokana na maneno KIBO na SHOW, hii ni sehemu ambapo Kibo kilionekana vizuri zaidi.

11. MWANANYAMALA

Hapo kitambo mitaa ya MwanaNyamala kulikuwa na mapori na wakabaji, kwa hiyo kina mama wa kizaramo walivyokuwa wakifika mitaa hiyo wakawa wanawaambia watoto wao "Mwana Nyamala" maana yake "Mtoto Nyamaza" ili wasisikiwe na maharamia.

12. TABORA

Kambi ya Wafanyabiasha. Walikuwa wakipita na bidhaa zao wanakuta viazi vitamu vilivyopikwa na kukatwakatwa vipande na kuanikwa. Hapo huliwa makavu (Chewing gum) au kupikwa na kuliwa. Haya huitwa Matobolwa au Matovola. Hivyo wakapaita kambi ya Matobolwa au Matovolwa. Hii ilikuwa kugeuka na kuwa Tabora.

13. SUMBAWANGA

Wenyeji wa maeneo hayo walikerwa na vitendo vya ushirikina (tofauti na mtazamo wa watu wengi kwamba wenyeji wanaendekeza ushirikina). Kutokana na kero hiyo waliamua kuwapiga mkwara watu wanaoingia katika mji huo kwamba kama unataka kuja huku, basi Tupa Uchawi i.e Sumba (Tupa) Wanga (Uchawi), ukitupa na kuuacha uchawi wako huko uliko unaruhusiwa kuja hapo Sumbawanga.

14. MTONI KWA AZIZ ALI.

Mtoni kwa Aziz Ali pamepata jina kutokana na mkazi mmoja aliyekuwa maarufu (alwatani) sana marehemu Aziz Ali. Mzee huyu alifariki miaka kadhaa iliyopita.

15. KWA BIBI NYAU.

Kwa Bibi Nyau kulikuwa na ajuza mmoja alikuwa anafuga paka wengi sana.

16. NEWALA.

Waingereza walipofika Mtwara walikuta kisima kilichojengwa na wajerumani ambacho kilikuwa cha kizamani kwa wakati Huo , Hivyo walijenga kisima kipya na kukiita NEW WELL, watanganyika wakatamka NEWALA, hatimaye likawa jina la ile sehemu.

17. CHEKERENI[MOSHI].

Hili ni eneo ambapo barabara inakatiza kwenye reli.Sasa wazungu waliweka alama ya bararani ya tahadhari kabla ya kuvuka reli CHECK THE LINE, watu wakatamka CHEKERENI na kuliita hivyo lile eneo hadi leo.

18 . MAKONGOLOSI

Inatokana na neno la kiingereza MAKING LOSS - Zamani waingereza walipata hasara kutokana na shuguli za uchimbaji wa madini eneo la Makongolosi wilaya ya Chunya mbeya ndipo eneo hilo kubatiswa jina hilo .

19 . GODIMA

Ni kijiji kimoja wapo kilichopo wilaya ya Chunya ambacho jina lake lilitokana na kiingereza ambalo ni GOLD MINE ( Mgodi wa Dhababu .
 
Marekani kule.massachusaset wakati wanapigana vita ya jamhuri kibosile akiwa kwenye farasi akamuuliza mtumishi wake how do we call this place? Mtumishi akasema oh...the master chooses it......ndio ikawa jina la pale hadi leo
 
Idodomya-DODOMA kulikuwa na tindiga nasikia tembo alizama hapo wenyeji wa huko wakapaita idodomya ambayo ni DODOMA
 
Kiboriloni linatokana na eneo hilo kuwapa taabu wazungu wakati wa kupima mipango mji enzi hizo.Wakapaacha kwa kusema KEEP IT LONG wakiwa na maana waendelee warudi baadae kuendelea na upimaji.Wenyeji waliposikia wakashindwa kutamka kiingereza hicho na kutamka Kiboriloni
 
Chekereni ni sehemu reli inakatiza barabara ambapo madereva wanatakiwa kuwa waangalifu CHECK RAIL wenyeji wakashindwa kutamka kimombo hicho na kutamka Chekereni.
 
Hata hivi visiwa vya ukanda wa tanganyika vilikuwa vikavu yaani havikuzungukwa na maji mengi ya bahari, kiasi kwamba watu waliweza kutembea hata kwa mguu, sasa hivi visiwa vilikuwa vinatumika kwenye shughuli ya kilimo, na walikuwa wanapata mavuno mengi,
sasa kutokana na watu wengi sana kumiminika kuelekea visiwani kulima, watu wakawa wanawauliza kwanini mnapenda kwenda kulima visiwani? Wakajibu kwasababu UNGO HUJAA(unguja)..
Sasa hilo neno likapata umaarufu UNGOJAA... na ndio likatokea neno UNGUJA
 
Kuna wana Jf wengine waseng e sana afu wako kama wanawake.
Mwenzake katoa darasa zuri...yeye anasema ujinga.
Basi atoe yeye yake ya maana tuyasikie.
Mpumba.vu weeee
Mxiyuuuuu!!!!
 
Pana vita vilipiganwa sehemu za usukumani huko sasa kulikuwa na mzungu alikuwa na bunduki moja matata sana inatema njugu mfululizo na ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kuitumia sasa ilivyokuwa inawapukutisha na kuwaangusha watu akawa anaisifia kwa kusema kwa sauti kubwa "this is hell magazine "wasukuma kusikia hivyo wakasema "mzungu kasema iselamagazi "
Nb :iselamagazi kwa kiswahili ni umwagikaji wa damu.
 
Back
Top Bottom