Kwa uvimbe wa titi, kipimo kizuri cha kufanya kuweza kufahamu kama ni kansa au hapana ni kufanya ni kukata sehemu ya kiuvimbe hicho na kukiotesha (biopsy); kipimo hiki ndio hutoa majibu kwa asilimia 100 kama ni kansa au si kansa...
Aksante sana Dr Wansegamila kwa elimu nzuri sana.Naomba elimu juu ya hili tatizo linalonisumbua.Nilishauriwa niwe natumia mito miwili ya kulalia kutokana na tatizo la Acid Reflux.Baada ya mwezi likanianza tatizo la maumivu makali ya shingo na kichwa kwa nyuma.Wakati mwingine yanapenya pande zote za kichwa kuelekea mbele kama short ya umeme.
Nilienda Hospital kubwa Dar wakanipiga X-Ray ya shingo na Fuvu.Fuvu halikuwa na tatizo lolote.Shingo wakasema kuna Muscle sparms.Wakanipa dawa za kutuliza maumivu tu.Maumivu yamepungua ila hayajaisha kabisa.
Tatizo hili nililipata Dec 2015.Kichwa kwa nyuma kinauma kama kiko karibu na moto,maumivu yanakuja na kutoweka.Kuna siku nakaa siku nzima bika maumivu na pia siku nyingine maumivu yanakuwa kwa muda mrefu.
Hasa mchana.Namshukuru Mungu,maumivu hayaniamshi usiku,nalala tu vizuri.Naomba ushauri ma-Dr.
Kiasi cha mionzi anayoipata mgonjwa kwa kufanya ct scan imepunguzwa sana kulinganisha na miaka ya nyuma kwa kuongezeka kwa teknolojia. Kwa hiyo kwa sasa teknolojia iko hapo, na kiukweli kiasi cha mionzi hiyo ni kidogo sana, kiasi kwamba ni kidogo kuliko ile mtu anayoipata akisafiri angani kwa ndege kwa muda wa masaa nane. Hivyo basi kisayansi mtu anaesafiri long flight kwa ndege (zaidi ya masaa 8 anapata mionzi zaidi kuliko anaefanya CT scan)...
CT scan kwa hospitali za umma nafahamu iko muhimbili,kcmc, bugando,pia peramiho(songea),
MRI kwa hosp za umma nafahamu ipo muhimbili (ilikwepo na ile hosp mpya ya dodoma,ila nasikia ndo imehamishiwa muhimbili baada ya MRI ya muhimbili kuharibika).