FAHAMU KUHUSU ARTIFICIAL INTELLIGENCE ?
Neno artificial intelligence tunaweza sema ni "Akili bandia" ule uwezo wa teknolojia kufanya mambo mbalimbali ambayo kwa kawaida uhitaji kutumia uwezo wa akili kama wa binadamu kuweza kutambua vitu, watu, lugha , sauti , kufanya maamuzi, kujifunza, kutabiri, kutafsiri na nk.
Watu wengi wakisikia Artificial intelligence huwa wanafikiri inahusisha labda maroboti na teknolojia zenye nguvu zaidi kupindukia Ambazo mtu anafikiri kuwa hajawahi kutumia Kwenye Maisha yake.
AI Hipo Kwenye teknolojia kubwa pia ziko Kwenye teknolojia za kawaida kila siku Kwenye Maisha yetu.
Watu wengi duniani tunatumia mifumo hii ya artificial intelligence Kwenye Maisha yetu kila siku nazani [emoji3]umeshtuka kidogo sio relax , najua unatumia google , Instagram , Twitter , facebooks , bolt , kamera za simu , online payment, YouTube, Gmail nk
Mifano [emoji116][emoji880]
โข ๐ฌ๐ผ๐๐ง๐๐ฏ๐ฒ[emoji271]
Unapotizama au unapotafuta kitu huwa YouTube wanapendekeza kuangalia video nyingine zinatokea hivyo utaona wanakuletea video inayoendana na kitu ulichokitafuta apa AI inafanya kazi ya kukusaidia kutambua na kukusogezea video zinahusiana na unachokitafuta.
โข ๐ธ๐ฎ๐บ๐ฒ๐ฟ๐ฎ ๐๐ฒ๐๐ ๐๐ฎ ๐๐ถ๐บ๐ [emoji991]
Ukifungua kamera Kwenye simu Yako ukitaka kujipiga picha utaona kuna wakati Kuna msaada unakuja wa kuchagua effect ambayo inaenda na mazingira unayotaka kupiga picha au unapotaka kujipiga selfie utaona kitu kinatokea kuzunguka USO wako apa AI inatambua uwepo wa USO wako Kwenye kamera.
โข๐๐ผ๐ผ๐ด๐น๐ฒ ๐๐ฒ๐ฎ๐ฟ๐ฐ๐ต [emoji361]
Unapotafuta kitu Kwenye Google mifumo ya Artificial Intelligence inakusaidia kuweza kukuletea majibu ya kile unachokitafuta ivyo google Utumia teknolojia ya Artificial Intelligence.
AI inatumika pia Kwenye masuala ya mawasiliano ,viwandani , Huduma za afya ,usalama , biashara , kilimo na nk.
Ebu tuachie maoni Yako ukisikia Artificial Intelligence ulikua unawaza kitu gani [emoji3] tuambie tujue ?
Teknolojia ni yetu sote [emoji110]