Fahamu kigezo bora kuliko vyote kwa mwanamke wa kuoa

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
4,464
11,338
Habari za uzima wakuu,

Leo ningependa tupeane marifa kidogo kuhusu Mada tajwa hapo juu,

Kila siku tumekuwa tukisikia matukio mbali mbali yanayofanywa na dada zetu/ndugu zetu/mama zetu (wanawake), matukio hayo ni kama,
1.Kumwagia maji ya moto watoto wao
2.Kumuwekea mume sumu/limbwata
3.Kuvunja ndoa za watu na kusambalatisha familia za watu kwa kupenyeza maneno ya uongo
4.Kumfitinisha mume kwa ndugu jamaa na marafiki kwa kupandikiza maneno ya uongo(kwenye hili mimi ni shuhuda namba moja).
5.Kudhuru watu kwa nguvu za giza(uchawi)

Ni mwanamke gani hutenda hayo yote?

NI MWANAMKE MWENYE ASILI YA KUTOKUWA NA HURUMA,
Mara nyingi furaha yake ni kuona watu wengine wakiteseka,
Kundi hili ni kubwa kwa asilimia 60,
Ndio maana wachawi wengi ni wanawake kuliko wanaume,

Wanapofanya yote hayo sio wao bali ni SHETANI(mapepo, nguvu za giza) NDANI YA MWANADAMU, na huwa hawajutii bali huhisi furaha mioyoni mwao,

Wanawake wasio kuwa na huruma ni waigizaji wazuri sana kiasi kwamba kumtambua mpaka uwe makini (uzoeane naye kwa muda mrefu)

Wanauwezo wa kumshawishi mwanaume asisaidie ndugu zake na akakubali kwa moyo mmoja. Wanaupendo fake kwa ndugu wa mwanaume pale anapo kuwepo tu akitoka hali hubadilika.

Kinga ni bora kuliko tiba,
KABLA YA KUOA CHUNGUZA KWANZA KAMA ANAHURUMA NA HOFU YA MUNGU.

NB: Huruma nayo izungumzia hapa ni ile hali ya kuguswa na matatizo ya watu wengine na kuhisi uchungu kihisia vile vile kufurahia maendeleo ya watu wengine ikiwemo kuonyesha nia ya kuwasaidia kwa moyo mmoja (pasipo wewe mwanaume kuwepo)

Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom