Fahamu jinsi ya kuandaa CV bora

Big Phil

Member
Nov 20, 2019
50
338
Curriculum Vitae ama CV ni utambulisho wako wa uzoefu wa kazi, elimu pamoja na sifa zako ambazo mara nyingi tunaitumia kwenye kuomba ajira kwenye mashirika, serikali pamoja na taasisi zingine.

Kuna aina nyingi za CV. Kuna zile CV za watu ambao hawana uzoefu (fresh from school), wenye uzoefu wa miaka kadhaa (experienced candidate).

CV bora inatakiwa iwe na vitu vifuatavyo:

1. Jina lako kamili - mara nyingi huwa kwa herufi kubwa.
2. Taarifa zako za anuani pamoja na mawasiliano yako ya simu na email address.
3. Uzoefu wako wa kazi kama unao kama hauna unaweza kuweka sehemu ulizowahi kujitolea au hata field kama wewe ni fresh from school.
4. Elimu - unaanza kwa mpangilio wa elimu yako ya juu kwanza na kushuka chini (chronological order)
5. Semina ana workshop ambazo ulishawahi kushiriki.
6. Referee - mara nyingi uwa 2 ama 3 ambao wanakufahamu na mara nyingi uwa walimu wa chuo, marafiki ama watu ambao tushafanya nao kazi na kwenye hili akikisha unawasiliana na referee wako mara kwa mara ili kupunguza sintofahamu kama kubadilisha namba ya simu ama email address.

Hakikisha CV yako inabadilika kutokana na kazi husika (job descriptions) and responsibilities lakini husidanganye sanaa

Kila la Heri on your job searching
 
Mimi la saba B niwapea watoto wa wajomba, kaka na dada kazi pasipo hizo cv. Zina umuhimu gani kwani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom