Gari iliyoundwa na immobilizer kuna uwezekano wa kutoa huo mfumo usifanye kazi ili utumie ufunguo wa kuchonga
Mueleweshe kuwa ukipoteza ufunguo kuna code wamekuandikia unaituma japan wanakuletea funguo nyingine. Kusema za ukweli hii ni ulinzi tosha wa gari na wengine imetusaidia sanaInawezekana,ila itahitaji mpaka ubadili mfumo mzima wa umeme wa gari na uweke mfumo mwingine kutoka kwenye gar ambayo haitumii immobilizer
Mueleweshe kuwa ukipoteza ufunguo kuna code wamekuandikia unaituma japan wanakuletea funguo nyingine. Kusema za ukweli hii ni ulinzi tosha wa gari na wengine imetusaidia sana
Inawezekanaje?Sasa hivi haina haja ya kutuma japana,kwan hata hapa kwa dar inawezekana
Out of topic!nataka kubadilisha funguo na ikiwezekana vitasa vyote vya milango vya gari yangu inawezekana boss ...
Mkuu kama mtu anahitaji kuchonga ufunguo mwingine ni mpaka akawekewe hiyo sensor? ndo itaweza kuiwasha garihusika?Je ulishawahi kusikia watu au fundi anakuambia gari limeingia kwenye immobilizer na ukashindwa kufahamu nini?
Immobilizer ni mfumo wa security ya funguo katika gari. Mfumo huu umewekwa ili kudhibiti wizi wa magari, kwani mtu akichonga funguo aina sawa na gari hawezi kuliwasha.
JINSI MFUMO UNAVOFANYA KAZI
Mfumo huu unafanya kazi kutokana na sensor(transponder) ambayo inakua kwenye funguo wa gari husika, sensor hii hutumika kama utambuzi wa funguo ni sahihi wa gari hilo au la,kama ni sahihi basi sensor hiyo hutoa signal kwenye immobilizer, na immobilizer huruhusu mfumo wa mafuta, spark na ignition kufanya kazi na kuwezesha gari kuwaka.
Kama funguo itakua ni tofauti, basi immobilizer hupata signal tofauti, hivyo basi huzuia mfumo wa mafuta, spark na starter kufanya kazi na kupelekea gari kuto kuwaka.
VITU VINAVYO SABABISHA GARI KUINGIZA FAULT YA IMMOBILIZER
Kwanza kabisa ni ufunguo wa gar kupotea, hii husababisha gari kutokuwaka hata pale utakapochonga ufunguo sawa na wa mwanzo. Kwani inahitajika kuprogram sensor nyingine ambayo itawekwa kwenye ufunguo ili kuwezesha gari kuwaka.
Kudondosha funguo mara kwa mara hii husababisha sensor kuvunjika kwa ndani, pia funguo kuingiliwa na maji kwani hua yanatengezeza unyevu ambao pia una haribu ile sensor na kusababisha gari kuto kuwaka.
BAADHI YA ALAMA ZA TAA KWENYE GARI ILI KUJUA GARI KAMA IMEINGIA KWENYE IMMOBILIZER
*KAMA UNA SWALI USISITE KUULIZA*
Mkuu kama mtu anahitaji kuchonga ufunguo mwingine ni mpaka akawekewe hiyo sensor? ndo itaweza kuiwasha garihusika?
Mkuu kama mtu anahitaji kuchonga ufunguo mwingine ni mpaka akawekewe hiyo sensor? ndo itaweza kuiwasha garihusika?
Kwaiyo sensor zinauzwa mkuuKama ukichonga ufunguo mwingine itabidi uitoe sensor kwenye ufunguo wa zaman uweke kweny hio uliochonga. Ila kama uta taka kutumia funguo zote mbili hapo itabid upate sensor ingine na ifanyiwe program.
Je,kama nataka funguo ya spare
yenye sensor,kampuni yako inasaidiaje?
Naweza kuja na funguo ya kwangu original
mkanitengenezea au kuna utaratibu gani mkuu?
asante.
Dah, hii ishu ilinitoka laki 3.5 hivi hivi kizembe zembe,..nilimrushia funguo muosha magari akashindwa kuidaka ikaanguka, utumbo wa ndani ukatoka. Kaiokota kairudisha fresh tu, kujakuiwasha gari ngoma haiwaki (inatekenyeka lakin haipokei). Kwenye dashboard kuna kialama cha funguo kina blink. Kumbe kuna kidude kidogo sana ndio sensa kimepotea funguo ilipo anguka. Laki3 na nusu hivi hivi zikanitoka ili fundi kuchokonoa control box na kuiprogram upya. Niliumia sana kwa uzembe wangu.
Nadhani hapo immobilizer haina kazi maana mijizi ikiiba tuvitz twetu wanakuja kwenu TWAFAAAAATuna machine zenye uwezo wa kufanyia programming hizo sensor na kuwezesha gari kuwaka