Fahamu dalili za mtu aliyeachwa katika mahusiano na mtu aliyempenda zaidi

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,182
3,547
KUACHWA NA MTU ULIYEMPENDA ZAIDI SIO MCHEZO ZIFUATAZO NI DALILI ZA MTU ALIYEACHWA

~ Muhanga wa tatizo hili hukosa utulivu wa akili katika kufanya na kukumbuka mambo yake binafsi na hata ya kijamii. Hushindwa kufanya maamuzi katika masuala mbalimbali yanayomtaka yeye kuamua.

~Mtu hujihisi mkosaji, asiye na faida wala msaada katika familia na jamii kwa ujumla. mara nyingi mtu wa namna hii hujiengua na kujiweka mbali na watu wengine na mara nyingine hufikiria na kujihisi hana hadhi.

~Mtu mwenye tatizo hili, hukosa tumaini la maisha, huona kila kitu kwake ni kibaya au kila jambo haliendi sawa, hujihisi kua na mkosi katika kila jambo analofanya. hujihisi kila mmoja ni adui yake anamuonea na kumg'ong'a.

~Wagonjwa wengi wenye dalili za tatizo hili, hukosa usingizi na huwahi kuamka asubuhi . Mwili hukosa nguvu pia na afya ya mwili kudhoofika.

~Mgonjwa hukosa hamu ya kufanya mambo muhimu tena ya furaha ,vitu kama vile kushiriki kufanyq kazi za kumuingizia kipato, kushiriki sherehe au hata michezo na shughuli mbalimbali za kijamii.

~Mtu hukosa hamu ya kula,kila chakula hutoa ladha mbaya mdomoni mwake na huona hakuna faida ya kukila chakula hicho.hii nayo huchangia mgonjwa kudhohofika kwa mwili.

~Wakati mwingine mtu mwenye tatizo hili,hujihisi maumivu ya kichwa na mwili mzima,hii ni kutoka na kufikiria sana kwa muda mrefu.

~Mtu mwenye tatizo hili asipopatiwa matibabu kwa muda mrefu hufikia hatua ya kufikiria kujitoa uhai. Mara nyingi utamuona akizungumzia kupotea hapa duniani, kutoa uhai wake mwenyewe. Mtu huyu asipopata uangalizi wa kutosha huweza kujitoa uhai wake mwenyewe.

HAYA ENDELEA KAMA ZINGINE UNAZIFAHAMU

1620648095573.png
 
Ukubwa raha siku hizi siumizwi na haya madude yanaitwa mapenzi. Usiponitafuta siku mbili eti mi kila siku ndo wa kwanza kukutafuta kha! Nakuzoom tu , hakuna cha kuumiza moyo wakati wengine sio kwamba tunakuwa tunawapenda kiviiiile ni basi tu ,ni umemzoea + kumvumilia = umejikuta ktk hali ya kumpenda.

Hivyo basi trh 28 nenda kapige kura, bila kukosa kazi ya kuzilinda sio yako. Mwenye nazo atazilinda usitake kujua kivipi.
 
Mkuu, minafikiri bado haujapona desperation kwa kuachwa.
Bado upo stressed chief..
 
Ukubwa raha siku hizi siumizwi na haya madude yanaitwa mapenzi. Usiponitafuta siku mbili eti mi kila siku ndo wa kwanza kukutafuta kha! Nakuzoom tu , hakuna cha kuumiza moyo wakati wengine sio kwamba tunakuwa tunawapenda kiviiiile ni basi tu ,ni umemzoea + kumvumilia = umejikuta ktk hali ya kumpenda.

Hivyo basi trh 28 nenda kapige kura, bila kukosa kazi ya kuzilinda sio yako. Mwenye nazo atazilinda usitake kujua kivipi.
Hujapenda ww!!
 
Mama wawili una mambo 😅😅😅 sema nakupenda umekuwa so frank. Inabidi uingie kwenye list ya zile namba B za mahaba tele
 
Mwisho kabisa ukishapona utajicheka na kujiona ulikuwa bonge la falaa.

Tunasisitiza tu, wanaume tuendelee kutafuta pesa, Pesa si kila kitu lakini husaidia kupunguza fedheha kama hizo.

Let's meet at the top, cheers 🍻
 
Ukubwa raha siku hizi siumizwi na haya madude yanaitwa mapenzi. Usiponitafuta siku mbili eti mi kila siku ndo wa kwanza kukutafuta kha! Nakuzoom tu , hakuna cha kuumiza moyo wakati wengine sio kwamba tunakuwa tunawapenda kiviiiile ni basi tu ,ni umemzoea + kumvumilia = umejikuta ktk hali ya kumpenda.

Hivyo basi trh 28 nenda kapige kura, bila kukosa kazi ya kuzilinda sio yako. Mwenye nazo atazilinda usitake kujua kivipi.
Aisee una akili sana mkuu uliwai kusoma na nyerere ni dada mkubwa
 
Unahitajika kuachwa ujifunze for once and for all ili kuzoea tukio hilo.
Penda na tafuta pesa, huyo pesa mpenzi na ndio nguzo za furaha duniani, unaweza ukaachwa na mrembo, ukapata mlimbwende kwa pesa,
Ila jifunze kupenda a simple lover for your forever love.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom