Fae ambrose from hero to zero

Fae ambrose from hero to zero

MKATA KIU

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
3,481
Reaction score
8,597
Heshima Kwenu Wadau..

Nina imani Wengi tumeona Beki wa Nigeria Ambrose alivyokimbiza kwenye AFCON.. Na kuonesha yupo serious na Soka Alisafiri jumatatu Straight From South Africa to Glasgow kuiwahi game Ya champions League knock out stage... Celtics vs Juventus na kweli akawahi na Kocha wake O neil akampanga kwenye kikosi cha Kwanza...

Na katika hiyo Mechi yeye alionesha Makosa mengi sana Ambayo yaliisababishia kipigo cha 3 kwa 0 kwenye uwanja wao wa nyumba Celtic park..

Nimejifunza Mpira wa Africa ni mrahisi sana ukilinganisha na wa ulaya Maaana Africa Beki wanafanya makosa lakini Washambuliaji Hawatumii makosa ya Mabeki kufunga magoli na ndo maana Afcon ilikuwa na Sare nyingi sana..

Lakini jana Ambrose makosa yake yote Yaliadhibiwa kwa Kufungwa magoli na washambuliaji wa Juventus mpaka Kocha wa Celtic o neil akakubali kwamba Hakuna chochote watachofanya kwenye marudiano maana kuruhusu Goli 3 kwa bila nyumbani ni ujinga wa hali ya juu na akakubali alifanya Worst decisions kumpanga Ambrose kwenye ile mechi.. Na hata mkenya Victor Wanyama alishindwa ku Couple na Speed ya washambuliaji wa Juventus...
 
Mkuu Mkata Kiu heshima kwako!
Lakini mie nina swali kuhusu kauli yako, "Nimejifunza Mpira wa Africa ni mrahisi sana ukilinganisha na wa ulaya"

Naomba kutofautiana:
-Ikiwa mpira wa Afrika ni mrahisi, mbona timu nyingi husononeka kuwakosa wachezaji wao wanapokuja huku AFCON?
-Ikiwa Ambrose ni "zero" na Wanyama si kitu, mbona walisaidia kuifunga Barcelona?
-Mabeki si wachezaji pekee uwanjani, viungo wako wapi? Washambuliaji wako wapi?

Ni vizuri kuwa "realistic" tunapochambua mambo au kulinganisha wachezaji.
-Mbona "Wazungu" kibao hufanya makosa ya "Kiafrika", au hujaona?
:confused2:
 
Mkuu Mkata Kiu heshima kwako!
Lakini mie nina swali kuhusu kauli yako, "Nimejifunza Mpira wa Africa ni mrahisi sana ukilinganisha na wa ulaya"

Naomba kutofautiana:
-Ikiwa mpira wa Afrika ni mrahisi, mbona timu nyingi husononeka kuwakosa wachezaji wao wanapokuja huku AFCON?
-Ikiwa Ambrose ni "zero" na Wanyama si kitu, mbona walisaidia kuifunga Barcelona?
-Mabeki si wachezaji pekee uwanjani, viungo wako wapi? Washambuliaji wako wapi?

Ni vizuri kuwa "realistic" tunapochambua mambo au kulinganisha wachezaji.
-Mbona "Wazungu" kibao hufanya makosa ya "Kiafrika", au hujaona?
:confused2:

Sijasema wachezaji wa ki africa hawana umuhimu,,, nachojaribu kusema ni kwamba Waafrica hatujui kutumia makosa,, hata kwenye Afcon mabeki walikuwa wanafanya makosa mengi lakini walikuwa hawajutii makosa yao sababu washambuliaji walikuwa hawafungi magoli...

Sasa kama jana Ambrose kafanya makosa mawili tu lakini yote yakafungwa magoli ndo maana wachambuzi wa soka hata jana wa DSTV wakina Kofur waliongelea hicho kitu kama uliwasikiliza after the game...

Mashindano ya kiafrica ni mepesi kulinganisha na ulaya na Washambuliaji wetu hawako makini kutumia nafasi...

Kocha wa Celtic ndie aliesema Wanyama ameshindwa ku couple na Speed ya kina Pirlo na akaruhusu mipira mingi mirefu iwe inapigwa na Viungo wa juventus ambayo ilileta madhara kwao..

Kaka nina imani una hoja nzuri lakini nakuomba upitie vyombo vya habari vikubwa kama goal.com, the sun, espn soccernet na kama una Dstv home naomba uangalie Soccer net press pass ya leo saa mbili usiku uone Ambrose blander itavyozungumziwa..

Makosa kama yale yale angeyafanya africa si ajabu yasingefungwa magoli maana washambuliaji wetu sio wazuri kutumia nafasi
 
MKATA KIU, uko sahihi bro, lakini mie sipendi hiyo dhana "mpira wa Afrika mrahisi".
Je, unalinganisha Africa v/s Ulaya au unalinganisha na Ulimwengu mzima?

Ikiwa Unalinganisha Africa v/s Ulaya, uko sahihi!
Mpira umenza kuchezwa Ulaya kabla ya Africa!
FA, ina umri wa miaka 150! Siwezi kukataa hilo!

-Ubora wa Washambuliaji ni kweli. Hiyo husababishwa na watu unaocheza nao!
Mfano: Leo Messi hafanyi vizuri akiwa Argentina kama anavyofanya Barcelona.

Huwezi kum-rate mtu kwa kumpa ZERO, labda kama ni jokes!
Ferdinand, Terry, Vidic etc, hufanya makosa makubwa ambayo hutumiwa na washambuliaji kupata magoli.
"Mpira ni mchezo wa mokosa" je, unaamini msemo huo? Bila makosa ya mabeki mshambuliaji hawezi kufunga..au MKATA KIU unasemaje kwa hilo..By the way na-respect maoni yako mkuu!
 
Back
Top Bottom