Kalumbesa
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 1,013
- 356
Arsenal wanaonekana kuwa waliongea na Luis ama agent wake kabla ya kupata ruhusa kutoka Liverpool( Hii ni kinyume na taratibu za usajili) na kuelezwa Suarez ana "release clause" ya paundi 40m, hivyo waka submit bid ya paundi moja zaidi(40,000,001 paundi) ya hiyo clause wakiamini watampata Luis Suarez. Bahati mbaya sana imethibitika paundi 40m siyo release clause bali mkataba umeweka wazi ni kiasi ambacho timu yoyote inayomtaka Suarez iki bid zaidi ya hapo basi Liverpool wanapaswa kumueleza Suarez na kukaa mezani na hiyo timu kuzungumzia usajili wa Suarez kwenda hiyo timu..na si kwamba hiko kiasi ndio bei ya kumuuza Suarez. Kwa maneno mengine Suarez hana "buyout release clause"..Hivyo Liverpool wanaweza ku demand kiasi chochote kwa timu inayomtaka Suarez kwa jinsi wao wanavyo mtathmini mchezaji wao!!..Liverpool wanaenda mbali zaidi na kusema hawawezi kumuuza Suarez kwa timu yoyote pinzani EPL..Hii sio sababu hasa ya msingi sana,ila kwa hali ilivyo ili Suarez atue Arsenal,basi inabidi Arsenal wa submit a mega offer, bid ya kushiba ambayo hata Liverpool watashikwa na kigugumizi kusema NO!!si kawaida ya Arsenal kujilipua na "high flying bids" lakini hatuwezi kujua wanamhitaji kiasi gani El - pistolero!!
