Facebook hizi .... !

Lee2

Member
Mar 6, 2014
46
95
Nimeshuhudia kituko.
Sidhani kama naweza kukiona/kukishuhudia tena.
Leo Nimesafiri na bint tukiwa siti jirani, da...! ni mrembo si kwa sura tu, bali hata mavazi yake. Anasitahili kuitwa mrembo.

Nilimkuta akiwa amekaa, kumsalimia akaitikia kwa nyodo sana da..! nikaachana naye.

Ndani ya safari ilikuwa kero kwani kila baada ya kama dakka30, alikuwa akipokea simu na kila alipopigiwa aliongea lugha ambayo iliashiria kuongea na mpenzi wake tena kwa sauti ya juu, wakimaliza kuongea wanaaza kuchati kwa sms zilizoendana na vicheko.

Ilifikia hatua ikawa kero siyo kwangu tu hata majirani walianza kumwangalia kwa nyuso zilizoashiria kukereka, maana bila aibu, binti alikuwa anatumia lugha ya kimahaba tena kwa sauti ambayo kwa mtu asiye rimbukeni wa mapenzi hawezi kuitumia mbele ya kadamnasi. Mfano(han nipo jian..., usijar nipo kwa ajir yako, mpaka na kukisiana ndani ya basi ....da!).

ilifikia hatua nikakosa uvumilivu nikamweleza angalau awe anapunguza sauti pindi awasilianapo" biti akaniambia nimkome.

Iliniuma ila nikakaa zangu kimya,
Safari iliendelea mpaka kufika, tukashuka,

binti alikuwa ameshapiga simu kwa mshikaji kuwa amefika.

Kama nusu saa hivi ikapita nikiwa bado, maeneo ya stendi nikaona kama sitofahamu ya watu wawili, kucheki vizuri, ni yule binti na kamsela kafupi kichizi (asili ya mbilikimo),nikasogea binti kuniona si kaaza kuniita kaka nisaidie....
Tatizo kubwa kamsela kanadai kurudishiwa gharana ya pesa kalizokuwa kanamtumi kama laki 5 hivi, kisa kakakataa na hataki kuondoka nako na kameng'ang'ania bengi lake.
Anakabembeleza kuwa atakarushia hela mara arudipo kajamaa kanadai atakadhurumu....!

ukweri binti alikuwa anatoa machozi na aibu kubwa kutokana na uwingi wa watu waliokuwa wanamzomea na kukashabikia kajamaa kamchukue, binti ikabidi kunibembeleza nikalipe kajamaa pesa ili aje kunirudishia tukirudi.

kwa sababu na mimi sikuwa na pesa yote hiyo,ilibidi akape simu na lak 330,000/TSH ambazo nilimkopesha, nilizokuwa nazo. Kajamaa kukapa hela kakabadilika tena, heti hakataki hela bali kanataka demu wake..!

kakaaza kulia na kudai nimekanyang'anya demu , watu si wakaaza kukashabikia tena heti kanirudishie hizo hela na mimi nikape demu wa kenyewe, kajama kakaaza kumpigia magoti mwanamke akasamehe kama kamemkosea da ilikuwa patashika.,. Yaliisha lakini mi mwenyewe nilioja cha moto kwa kuzomewa na wapiga dembe wa stendi.

Baadaye kukaa naye binti faragha anadai walifahamiana kwa njia ya Facebook. Na ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kutembeleana.

Nilitumia simu yangu kuingi kwenye akaunti yake kamsela kaliweka picha za jamaa wengine kwenye profile.
 

Tarime one

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
2,249
2,000
Wabongo wengi tulishazoea kufake life, hatuko real na tunaona kawaida, sometimes price ya kufake life huwa ni kuvuna aibu.
 

MO11

JF-Expert Member
Mar 23, 2014
17,482
2,000
hii stori ina 99 asilimia ya uongo hivyo peleka huko facebook
 

Lee2

Member
Mar 6, 2014
46
95
Mtu ulikutana nae kwenye "basi"

Halafu ukakubali kutoa 330,000

Aiseeee ....

Hii hata kale ka jogoo kangu pale nyumbani hakawezi kukubali!

unabahati unakajogoo nyumbani, ingekutokea hata Tsh 100 sikupi.
 

thinky

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
2,121
0
hahahaha sipati picha demu alivyoshtukizwa mambo.... haha.....afu ninyi mnaosema uwongo bongomovie ni kweli
 

masai dada

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
14,048
2,000
hii hadisi nzuri sana

mwa,bie muhusika aliekopesha hela ilikuwa maka gani MAANA KWA ULIMWENGU HUUU SIJUI
 

NullPointer

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
3,467
2,000
Yani ukatoa 330,000 ukampa?
Kilaini hivo! em tupe sababu ya msingi labda tutakuelewa....
umeonyesha jinsi gani ulivo kichwa mbovu, kama ni mpango ulikua umepangwa kukutapeli? afu unakuja JF kwa kujiamini na unaandika bila hata kujishtukia ukidhani bac watu wata-appreciate kua unatoa msaada hela fasta tu.. What a douche!!
Wabongo mmekuaje?? hii story nahisi imetungwa
 

Lee2

Member
Mar 6, 2014
46
95
Yani ukatoa 330,000 ukampa?
Kilaini hivo! em tupe sababu ya msingi labda tutakuelewa....
umeonyesha jinsi gani ulivo kichwa mbovu, kama ni mpango ulikua umepangwa kukutapeli? afu unakuja JF kwa kujiamini na unaandika bila hata kujishtukia ukidhani bac watu wata-appreciate kua unatoa msaada hela fasta tu.. What a douche!!
Wabongo mmekuaje?? hii story nahisi imetungwa

kumbe unahisia tu? Ruksa...!
Ni hivi binti tumetoka naye (wilaya moja) na kabla sijampa hizo hela nilimdadisi vya kutosha mpaka kumwamini, mfano kunadadayake (dadayake namfahamu hata mimi ni nesi hospital ya wilayani kwetu) ilibidi tumpigia na kumwambia ukwer kilichotokea na yeye kaniomba nimsaidie mdogo wake. Unajua huwezi ukaandika kla ktu hum jf.
Na kwa taarifa binti tumerudi naye na dadayake kashanirudishia hela zangu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom