Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa Victoria , Ezekia Wenje , mmoja wa Wahanga wa Uchaguzi wa 2020 , ambaye Mkutano wake wa mwisho wa Kampeni Ulimiminiwa risasi utadhani Ukraine , na kumuua Kaka yake , sasa amejitokeza nchini ili kuimarisha chama chake .
Wenje baada ya tukio lile alilazimika kukimbia na kujificha kusikojulikana ili kuokoa uhai wake , na wala hakushiriki mazishi ya kaka yake , maana yeye ndiye alikuwa Target ya waliotumwa kummaliza.
Utukufu wa Mungu ni wa Ajabu sana , leo wenye amerudi na kushiriki Chadema Digital kwenye kanda yake , HATIMAYE SHETANI AMESHINDWA .
Mytake : Kuwasamehe walioshiriki unyama wa uchaguzi wa 2020 ni Sawa ngamia kupita kwenye Tundu la Sindano , Sidhani kama inawezekana .
TUOMBE SANA MUNGU .
=====
Wenje aunguruma Sengerema
Muktasari:
- Mbunge wa zamani wa Nyamagana (Chadema), Ezekiel Wenje amesema Serikali imewatekeleza wananchi katika jambo la mfumo wa bei hasa upande wa mahitaji muhimu ya wananchi hususani chakula na kuwaweke wananchi njia panda.
Sengerema. Mbunge wa zamani wa Nyamagana (Chadema), Ezekiel Wenje amesema Serikali imeshindwa kudhibiti mfumuko wa bei na kuwaacha wananchi wa Tanzania walikia na kutaabika.
Wenje ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Victoria, ametoa kauli hiyo leo Oktoba 20, 2022 kwenye mkutano maalumu wa chama hicho wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.
Amesema Serikali imewatekeleza wananchi katika jambo la mfumo wa bei hasa upande wa mahitaji muhimu ya wananchi hususani chakula na kuwaweke wananchi njia panda.
“Wanakalia kuumiza wananchi kwa tozo zisizo na ulazima wanashindwa kuangalia jambo linalogusa maisha ya watanzania,” amesema Wenje.
Amesema wananchi sasa wanatakiwa kusimama na kuamua kufanya mabadiliko ya kweli ndani ya nchi ili wapate unafuu wa maisha na jambo hilo litaletwa na Katiba ambayo ni chaguo la wananchi.
Hivi sasa hapa nchini, wananchi wanalia kutokana na mfumuko wa bei, hii imesabibishwa na wafanyabiashara kupandisha bei ya vyakula, hali inayowafanya wananchi kulia na hali hiyo.
Sambamba na hilo, Wenje amesema zama zimebadilika, walikimbia nchi sasa wamerudi kuisuka Chadema, hivyo wanachadema wanapaswa kuungana kwa pamoja ili kuwasaidia wananchi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Pambalu amesema nchi hii wananchi wanatakiwa kufanya mabadiliko ili kuwaondolea msongo wa mawazo waliyonayo kutokana na mfuko wa bei.
Mabaliko haya nikudai katiba mpya ambayo nimkombozi wa Watanzania wote, hivyo wanatakiwa kuwa wamoja ili wasonge mbele.
Paul Lufungulu ni mjumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ya Sengerema, amesema wako tayari na wamejiandaa kutembea kwa kila kijiji kutoa hamasa kwa wananchi juu kilio cha katiba mpya.
Maye katibu mwenezi wa Chadema Jimbo la Sengerema, Stanley Kakele amesema wamejipanga kuhakikisha jamii inapata elimu juu uwepo na wakatiba mpya.
Chanzo: Mwananchi