Kingunge ni mwanasiasa wa zamani inapaswa tumheshimu.
Tunaweza tusimpende mtu au mawazo yake lakini hoja zetu zisiwe za kumlenga yeye binafsi kutokana na umri, jinsia, imani au vitu kama hivyo. Hayo ni masuala binafsi
Waziri Kalala,
Ninapenda kukupongeza kwa kuwakumbusha wachangiaji wengine kuwa kitu muhimu ni kujadili hoja ya Mzee Kingunge na wala siyo kutoa maneno ya kejeli juu yake kwani hayasaidii lolote. Vilevile tukumbuke kuwa Mzee Kingunge ni mwanasiasa mkongwe na aliyebobea kati propaganda, kwahiyo wakati anaongea hayo anajua huo mzigo wa kulumbana anaupeleka wapi.
=ochu;278141]Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM), kitahakikisha kinawashughulikia wapinzani na kuhakikisha wanaumaliza kabisa upinzani. Kingunge ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, aliyasema hayo mjini Dodoma wakati wa hafla ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pancras Ndejembi.
Kauli hiyo hapo juu nadhani ni kauli muhimu sio tu kwa wana-CCM bali hata kwa wapinzani, kwani kila upande unaoshindana hutarajia ushindi. Ni sahihi kwa Mzee Kingunge kuweka tambo za kisiasa kama hizo. Ni jukumu la wasio wanachama wa CCM kuweza kujijenga na kujiimarisha kukabiliana na changamoto hiyo ya CCM. Msikae hata siku moja kama CCM itasema itasaidia kuviimarsha vyama vya upinzani, that will be an ugly statement of the decade.
Kingunge alisema nguvu ya chama kwa sasa inaelekezwa kwa wapinzani lengo kuu likiwa ni kuwamaliza licha ya kuwa tayari chama chake kimeshafanikiwa. "Sasa hivi hakuna kitu na tumefanikiwa kwa sababu ya kuwaunganisha wanachama wetu na kuwa kitu kimoja na haki ndiyo inayowaunganisha na ndio maana tumefanikiwa," alisema mkongwe huyo.
Kwa wasio wanachama wa CCM hii pia ni kauli nyingine ambayo pia inatakiwa kuchukuliwa kama changamoto kwani kama vyama vya upinzani vitawaunganisha wanachama wao basi ni dhahiri kuwa vitapata mafanikio
Alisema iwapo kiongozi wa CCM atashindwa kupambana na upinzani, ni lazima uongozi wake utakuwa na dosari na hivyo atanyang'anywa madaraka. Akimzungumzia Ndejembi, alisema ni vyema viongozi wa CCM wakatambua kuwa CCM imetoka mbali kwa historia ndefu ili iendelee kuwapo, ni vyema wakajivunia viongozi waliopita na kuwaenzi.
Alisema pamoja na hilo, pia CCM inaamini kuwa kazi kubwa ya kiongozi ni kuunganisha watu anaowaongoza na si kutenganisha watu au kutafuta vikundi vyake na kama kiongozi wa CCM atafanya hivyo, huyo hafai kuongoza chama hicho. Kingunge aliwataka viongozi ndani ya chama hicho kuwa wavumilivu na wasikivu na kuzisikiliza jumuiya zote ni nini zinataka na si kulazimisha na kufanya vile ambavyo yeye anataka.[/QUOTE]
Maneno ya Mzee Kingunge ni ya maana sana kwa kila mwanasiasa awe ni wa CCM au opposition. CCM watayachukuwa wayafanyie kazi na ninyi wapinzani pia myachukue kwani yatawasaidia sana. Asiyeona hilo, naomba atafakari kwa kina. Tujadili hoja za Kingunge.