EYE SPY: Time to retire, Mzee Kingunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

EYE SPY: Time to retire, Mzee Kingunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Aug 31, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,679
  Likes Received: 82,531
  Trophy Points: 280
  EYE SPY: Time to retire, Mzee Kingunge

  Adam Lusekelo
  THIS DAY
  Dar es Salaam

  HE was once a Marxist communist. He never believed in God the Almighty. And in the swearing-in ceremonies and taking oath for many an office, he would never touch the Holy Bible or the Holy Koran.

  Those were the days of the late founding Mwalimu Julius Nyerere. Kajetan Kingunge�Ngombale Mwiru would simply raise his right hand and pledge to serve the United Republic of Tanzania to the best of his ability. He never said: So help me God because he never believed in deity.

  Some of us were in secondary school then. Our heroes were Fidel Castro of Cuba, Ernest ’Che Guevara’, an Argentinean revolutionary who fought with Castro.

  Others were Walter Rodney who was at that time teaching at the Chuo Kikuu in Dar es Salaam- when the University of Dar es Salaam was a real chuo kikuu. These the were revolutionaries then. Locally we had the likes of Kingunge Ngombale Mwiru, Jenerali Ulimwengu and other socialist cadres in the ruling TANU party.

  But times have changed. The once radical socialist cadre have come of age. Most would rather worry about what they will have for dinner, rather than worry about socialist dogma. Some of them are now plain thieves in the ruling party, the CCM. Some have retired from politics and some are not with us anymore (RIP).

  Anyway we were revolutionaries then. Ready to die for the revolution. Most of us wore berets, like Che Guevara. You see, if you are not a revolutionary at 20, then there must be something very wrong with you. And if you still are a revolutionary at 50, two decades later, then there is also something very wrong with you.

  With age you go on mental time warp. That’s why you hear your grand father say: ’’In our days, if you fancied a girl you go and see their family.’’ We the grand-kids had to accept that. In Kiswahili we say; ’’Amepitwa na wakati.’’

  When you are a grand-dad it is more fun to sit down and reflect on life, read and re-read some agreeable books over a drink and play with your grandchildren. It is definitely not a time to go into the rough and tumble of today's politics.

  Kingunge, now a sexagenarian, has always been a one-party politics man. The tragedy is he still thinks Tanzania is a one party state. Worse is Mzee Kingunge thinks that party loyalty should come supreme even if that one party has been turned into a den of thieves.

  But in that one party it is not all rot. There are some mavericks who love their party and want to cleanse it. Kingunge thinks that those in the party who abhor its thieving ways should immediately be shot at dawn.

  Within CCM there are stars like MPs Anne Kilango and Alloyce Kimaro who insist that the only way to bring whatever credibility which is left into ruling CCM party is to go on vigorous house cleaning.

  But Mzee Mwiru thinks that MPs within the ruling CCM, who question the badly tainted party, are disloyal. How can you be loyal to a group of people who are basically crooks.

  The ’real’ CCM revolutionaries have pooh-poohed Mzee Mwiru’s call for their purge from the party. They have simply dismissed his politics as those practiced back in 1977, when Tanzania was strictly a one-party country, ruled by the CCM.

  Maybe Mzee Mwiru should take a reflection in 2008. The majority of Tanzanians are not really impressed by the way CCM has been running the show. They actually are angry and disgusted with its scandal-ridden government.

  Maybe our former Marxist socialist, Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru should retire. He should relax and order a drink or two, read books and play with his grand kids. It should be more fun for him than Tanzania's politics of 2008.

  mail:mbwene2@yahoo.com
   
 2. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2008
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  I simply like this guy - Adam! And last week he was in hospital! Tell them Adam!
   
 3. W

  WembeMkali JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2008
  Joined: Jun 16, 2007
  Messages: 282
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Socialism system siyo system mbaya kama westerners wanavyotangaza.Ndiyo maana utaona Spain na Latin America wameamua kurudi tena kwenye hiyo system baada ya kuwa na Capitalism for a quite sometime.
  Che Guevara,Castro,Ulimwengu,Nyerere,Rodney na wengine wengi bado wataendelea kuwa hereos katika kupigania haki na usawa for the weak.
  Tatizo la Kingunge siyo usocialism bali ni Usisiem(U-CCM).Ni U-CCM ndiyo unaomfanya awe hivyo.Lakini kama kweli angeweza kuelewa japo punje ndogo ya misingi mikuu ya socialism asingeweza kutetea mafisadi au kuzuia wabunge wanaohoji juu ya ubadhirifu wa mali ya umma.

  Wembe.
   
 4. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kingunge azidi kukosolewa

  na Deogratius Temba


  WANASIASA na wanaharakati wa haki za binadamu, wamemkosoa mwanasiasa mkongwe na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale - Mwiru, kuwa matamshi yake yanachafua upepo wa kisiasa nchini na hayana ukweli kwa wananchi kwa vile yanalenga kutetea ufisadi ndani ya chama hicho.

  Wamemtaka afahamu kuwa Watanzania wanajua kuwa ndani ya chama hicho kuna ufisadi unaoibuliwa sasa na wabunge wa vyama vya upinzani, na hapaswi kuwatisha wabunge wa CCM wanaochukia ufisadi.

  Kauli hizo zimekuja baada ya Kingunge kupokea maandamano yaliyoandaliwa na CCM, Mkoa wa Dodoma juzi, kwa lengo la kupongeza hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa bungeni mwishoni mwa wiki iliyopita.

  Akizungumza kwa mahojiano maalumu na Tanznaia Daima Jumapili, Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu, alisema Kingunge anapaswa kutulia kwa kuwa ameshazeeka.

  “Kingunge ameshindwa kuonyesha mapenzi kwa nchi hii na Watanzania, atajikuta hata kwa chama chake hana mapenzi, kwa sababu atachangia kuiua CCM. Kwa jinsi anavyotetea uongo hadharani wakati akijua kuwa hata watoto wadogo wanajua kuwa kuna ufisadi ndani ya chama hicho,” alisema Prof. Baregu.

  Alisema kiongozi wa zamani kama Kingunge, anapaswa kuwa makini na matamshi yake ili kulinda heshima yake badala ua kuropoka na kukitetea chama ambacho kimeshapoteza mwelekeo, heshima, maadili na kugubikwa na rushwa kila mahali.

  Alimuasa Kingunge kuwa na mapenzi na maisha ya Watanzania na taifa kwanza kabla ya chama chake, kwa sababu Watanzania ni watu na wanahitaji kulindwa.

  Akizungumzia maandamano ya kuunga mkono hotuba ya Rais Kikwete, alisema wananchi wanasukumwa kuandamana na watu wenye vijisenti.

  Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Wilfred Lwakatare, kwa upande wake alisema Kingunge ana mawazo ya kizamani na hapaswi kuendelea kutoa michango ya mawazo kwa sasa kwa vile akili yake imechoka na haiendani na wakati huu wa mabadiliko ya kisiasa na mfumo wa vyama vingi.

  “Asijidhalilishe kwa kutokwenda na wakati, anyamaze kimya, hakuna atakayemlazimisha kuongea, hakitakii mema chama chake, anasaidia kukiua kwa kauli zake,” alisema Lwakatare.

  Alisema kila Mtanzania anafahamu kuwa kero na maovu yote ya serikali ya CCM yameibuliwa na wapinzani bungeni, lakini CCM inachanganyikiwa na kupora hoja hizo huku ikijigamba kuwa imeziibua.

  Lwakatare alisema Kingunge anasahau kuwa hata Spika wa Bunge, Samuel Sitta na wabunge wengine ndani ya chama hicho, sasa wanakiri kuwa serikali imeshindwa kuwadhibiti mafisadi.

  Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Ananilea Nkya, alisema watu kuandamana ni tatizo ambalo limesababishwa na serikali kuruhusu mtu mmoja kuwa na fedha nyingi kupita kiasi, hivyo kuwa na uwezo wa kununua watu na kuwafanya waandamane.

  “Serikali imebana pesa kwa raia wa kipato cha chini, wachache wanayo mabilioni, wanakuwa na jeuri ya kununua watu wengine, wanakuwa na uwezo wa kufanya chochote katika nchi.

  “Siamini kama Watanzania ni watu kidogo vile kama hao wanaoandamana, ninachojua ni kwamba ufisadi una nguvu ya kufanya chochote. Rais anawaogopa hawa kwa sababu ya kiasi cha fedha walizonazo. Hayati Mwalimu Nyerere hakukubali hata siku moja mtu mmoja kumiliki fedha kiasi hicho ambacho mafisadi wanamiliki sasa,” alisema Nkya.

  Nkya alisema kuwa umefika wakati sasa kwa Watanzania wote kuuliza kwanini watu wanampinga rais waziwazi, na kila mtu ajitahidi kusikiliza hotuba za viongozi na azichambue na kujua nini kinaendelea ili kuepuka kudanganywa na mafisadi.

  Kingunge akihutubia waandamanaji wachache mjini Dodoma juzi, alisema wapinzani wanataka umaarufu kwa kutumia kashfa na aliwakemea wabunge wa CCM ambao wamekuwa wakiunga mkono sera za wapinzani za kupambana na ufisadi.
   
 5. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  kingunge ni mmoja wa watu waliolifikisha taifa hapa lilipo kwa kukumbatia mawazo yalioshindwa na kukariri kama kasuku sera za akina max na wengine, akaja hapa nchini akafaulu kuteka mawazo ya watu , hajajijua kuwa ni failure tayari.

  wakati wa enzi za zidumu fikra sahihi zilishapitwa na muda. na kama ni fisadi huyu mzee ni nambari wani, kile kituo kikuu cha ubungo kwa ufisadi wake ndoo kwanza kinazeeka naye
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Huyu mzee hana hata chembe cha kuwajali wadanganyika. Ni mnafiki mkubwa huyu kavaa ngozi ya kondoo lakini ni mbwa mwitu huyu.
   
 7. c

  chikira Member

  #7
  Sep 1, 2008
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haka kazee kamechoka.Ninachoamini ni kwamba kila mtu mwenye akili timamu anakapuuzia,ingawa ni kweli kanachafua hali ya hewa ya kisiasa.Ni bora kakanyamaza,kwa vile watanzania hawatakasamehe na historia itakahukumu.
   
 8. Lighondi

  Lighondi JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 585
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huyu mzee hivi ana matatizo gani?!! Hivi hajui kwamba ufisadi wa TZ hauhitaji hata elimu ya chekechea kufahamu! Sijui anajisikiaje kuendelea kutuchefua ! Ananiuziiiiiii!!!!

  Hajui tuuuu!!!!
   
 9. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM), kitahakikisha kinawashughulikia wapinzani na kuhakikisha wanaumaliza kabisa upinzani. Kingunge ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, aliyasema hayo mjini Dodoma wakati wa hafla ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pancras Ndejembi.

  Kingunge alisema nguvu ya chama kwa sasa inaelekezwa kwa wapinzani lengo kuu likiwa ni kuwamaliza licha ya kuwa tayari chama chake kimeshafanikiwa. “Sasa hivi hakuna kitu na tumefanikiwa kwa sababu ya kuwaunganisha wanachama wetu na kuwa kitu kimoja na haki ndiyo inayowaunganisha na ndio maana tumefanikiwa,” alisema mkongwe huyo.

  Alisema iwapo kiongozi wa CCM atashindwa kupambana na upinzani, ni lazima uongozi wake utakuwa na dosari na hivyo atanyang’anywa madaraka. Akimzungumzia Ndejembi, alisema ni vyema viongozi wa CCM wakatambua kuwa CCM imetoka mbali kwa historia ndefu ili iendelee kuwapo, ni vyema wakajivunia viongozi waliopita na kuwaenzi.

  Alisema pamoja na hilo, pia CCM inaamini kuwa kazi kubwa ya kiongozi ni kuunganisha watu anaowaongoza na si kutenganisha watu au kutafuta vikundi vyake na kama kiongozi wa CCM atafanya hivyo, huyo hafai kuongoza chama hicho. Kingunge aliwataka viongozi ndani ya chama hicho kuwa wavumilivu na wasikivu na kuzisikiliza jumuiya zote ni nini zinataka na si kulazimisha na kufanya vile ambavyo yeye anataka.
   
 10. w

  waziri kalala Member

  #10
  Sep 2, 2008
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HAKIKA wajamaa wa jana waliogeuka mabepari sidahni kama wana jipya la kutuambia.
  Haya kama ndio maoni ya mshauri wa mambo ya kisiasa wa CCM basi tutatumbue kuwa chama hicho hakina sera, visheni wala misheni kubalifu kwa watanzania hivi sasa.

  Kwa kuwa Watanzania wa leo kuliko ilivyokuwa huko nyuma wanauhitaji upinzani ili kudhibiti ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na kuuzuia ubia wa wanasiasa na wafanyabiashara kuwamaliza Watanzania wa kawaida.

  Mwananchi lazima atambue upinzani uko kwa faida yake na sio kwa faida ya upinzani wenyewe. Kutokuwa na chama cha upinzani kilicho na nguvu na uwezo katika jamii ni kukaribisha ufisadi, matumizi mabaya na ya kifahari ya fedha za umma, udikteta na wakubwa na jamaa zao kujipendelea na hivyo kuurudisha usultani au ufalme kwa mlango wa nyuma huku watoto wa walalahoi wakisota ile mbaya na kudanganya kwa ahadi ambazo mpaka wanakufa hazitatimizwa!
   
 11. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2008
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mzee ngoja kufa tu muda wako umekwisha. Badala ya kufikiria ni jinsi gani mtaimarisha maisha ya watanzania Kingunge anafikiria jinsi ya kumaliza wapinzani kwa kusema maovu ya wafisadi. Mungu alikuuliza umefanya nini ulipokuwa na nafasi kusaidia wananchi wako masikini utasemaje wewe mzee? Tubu zambi zako na badilisha maisha yako kwani huu si wakati wa kufikiria siasa na muda wako umekwisha.
   
 12. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2008
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Huyu mzee ni wa ajabu sana. Mbona hakubali kuwa muda aliopewa kukamilisha mbio umekwisha? Mawazo aliyonayo kwa sasa hayaendani na kizazi kilichopo wala hayaongezi chochote kwenye mchakato tulionao, kwa ushauri ni bora akae kimya ama akacheze na wajukuu, hana jambo jipya kwenye mambo yahusuyo taifa letu.
   
 13. w

  waziri kalala Member

  #13
  Sep 2, 2008
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SISI sote tutakufa ninadhani si muwala kutumia lugha kama hii ya kumwambia mtu wewe ngoja kufa!!! Au mnasemaje wenzangu. Kingunge ni mwanasiasa wa zamani inapaswa tumheshimu.

  Tunaweza tusimpende mtu au mawazo yake lakini hoja zetu zisiwe za kumlenga yeye binafsi kutokana na umri, jinsia, imani au vitu kama hivyo. Hayo ni masuala binafsi. Na ndio maana mgombea mwenza wa McCain mwenye umri wa miaka 17 kazaa nje ya ndoa lakini Republicans wanaikubali hiyo ndio sera yao ya kujisaidia wenyewe na KUTUSAIDIA mafikiri kama sisi ili tusahau maendeleo kwa kuwaza tu habari za ngono.

  Huyu bwana enzi zake angeweza kuwa na majibu muafaka kwa wakati na suala husika. Lakini hivi sasa CCM haina mtu wa kuwaza ili ina watu wa kubeza mawazo ya wengine; CCM haijui nchi ilikoelekea kwa hiyo wanawakaribisha Wamarekani wanaofikia ukingoni -Republicans- kutuonesha njia!!! CCM inatuambia nchi inaendelea lakini maendeleo ukiyatafuta katika nyumba zetu utakuta ndio kwanza sasa mtu hamudu kulitoa gari lake ndani-kisa petroli; waliokuwa wakila kuku mara moja kwa wiki sasa wanakula mara moja kwa mwezi kwa bahati bahati; wenye miradi yao imekwama maana mabenki na taasisi za fedha zimegeuka nyumba za kuwachuna wasio nacho ili wafanyakazi wao wawe na maisha bora kuliko Watanzania wengine kama walivyo wale wa makampuni ya mafuta.

  USTAARABU tumwambie tu mzee atuite vijana atupe usia jinsi gani nchi hii inaweza kuwa ama ya chama kimoja tu kama ndivyo anavyotaka au jinsi gani vijana wa upinzani na wa CCM tunaweza kuwa kitu kimoja kama vile mwenyekiti wa chama chake anavyopenda ili tuiletee nchi sio tu amani na umoja bali pia maendeleo kutokana na utofuati wetu!
   
 14. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2008
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Upinzani is the essence of democracy. Finish off upinzani, the you usher in dictatorship. It seems as if some people are living in their own worlds and need a wake up call!!
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Dhamira ya Rais, ambaye ndiye mwenyekiti wa chama cha Kingunge, ni kutouua upinzania. At least hivyo ndivyo alivyosema wakati wa hotuba yake Bungeni Desemba 2005. Sasa kama chama chake kinadhamiria kuufuta upinzani, tuelewe nini; kwamba rais, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama kinachotaka kufuta upinzani, hakusema hayo kwa dhati ya moyo wake? Au kuna mapambano ya dnani ya CCM ambako limezaliwa kundi la akina Kingunge ambao wanataka kuua upinzani tofauti na dhamira ya rais?
   
 16. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #16
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Waumalize upinzani ili iweje? Imetokea wapi duniani kitu cha namna hiyo? Yaani katika mikakati yao yote moja wapo ni hilo la kuumaliza upinzani?

  Oh, Mungu aingilie kati. Kuwa na viongozi wa namna hiyo ni jambo la hatari sana, na ndo maana uwanja wa siasa hapa kwetu hauko sawa-theres no fair play.
   
 17. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #17
  Sep 2, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  siasa za TZ ni kama michezo ya kuigiza. ndo maana wananunuana kila siku utasikia huyu kahamia huku nk. kuna kitu kama hicho US au Uk?
   
 18. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #18
  Sep 2, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Hili kenge bado linakimbizana na chama kweli linazeeka vibaya

  maulana msitiri kiumbe shako asiende jehanam na uzee huu

  kama dhambi wabebe wanae wakina kinje na uhuni wao mwokoe maulana
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyu Mzee tulisha sema apumnzike kumjadili jadili tunampa kichwa sana huyu mzee..kwani kesha jichokea anajiongelea hadithi za kale na huku anasahau dunia sasa inabadilika yeye naona anachelewa sana kubadilika.
   
 20. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  bado ana mawazo ya chama kimoja enzi za zidumu fikra za mwenyekiti hata kama anamuwaza mkewe
   
Loading...