Extreme Social

PetCash

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2012
Posts
1,995
Reaction score
2,017
Habari za jioni wanajamvi.

Kuna mtu wa karibu yangu (Naomba kumhifadhi ila ni ndugu upande wa wife..). Huyu yani ni member wa kila social network nnayoijua. Hi5, myspace, facebook, whatsapp, badoo, viber, imo, instagram( I seriously doubt kama na huku hayupo).

Sasa imekuwa kama maisha yetu ni public. Tukiwa tunakula mezani msoc ulishauplodiwa zamani...we unaona tu few seconds ago.
Mara my family, mara my home, mwanangu my baby, yaani wife asije na kitu kipya tayari kimeshapanda.

Nimejaribu kumuonya lakini wapi. Ataitikia kesho kama kawaida. Anabadilisha ID anatuondoa kwenye list ya friends anaendelea. Nikaona ni shida bora wife apambane naye.

Sasa juzi kaingia period kaupload picha instagram na caption anaumwa (taarifa aliniletea wife). Sasa mimi najua shule haendi kwa sababu anaumwa kumbe ni hivyo.

Hivi wanawake, ni sahihi kweli watu wakujue kiasi hicho?

Yaani sometimes I hate kuishi naye kwa sababu ya ku publicize kila kitu na haiwezekani tusiishi naye.

 
haya ni machungu? hizi ni hasira umekuja kuzimalizia humu? ama unaandika misitari ya nyimbo?

nimesoma sijaelewa kitu.
 

Uko sahihi sana ndugu Petcash, hii tabia binafsi huwa siipendi na ni matumizi mabaya ya mitandao...yaani siku hizi imekuwa kama ugonjwa vile mtu anapost kila kitu au kila tukio hata kama linahitaji privacy. ni vizuri tukashare matukio na picha mbali mbali lakini tuwe tunaangalia na mazingira yenyewe.. huwezi kutuma picha yenye watu zaidi mmoja waliopiga nawe kwenye mtandao maana hujui jinsi gani watu hao watajisikia kwa kitendo hicho.

mbaya zaidi siku hizi mtu akipata ajali bara barani au akifikwa na tatizo lolote MIJITU inakimbilia haraka kwenye tukio kama vile inaenda kutoa msaada ila yakifika hapo unakuta yamening'iniza simu zenye kamera yana record ili yapate cha kupost.. mnaboa sana nyie watu. Mbona mmekuwa waandishi wa habari msio na mipaka.... tuwe na staha kwa kweli mnakera sana watu wa aina hii.
 
Owh you hate kuish nae??? Hakuna wa kumface humu ndani kumwambia the way you feel kwake. Ni wewe baba mwenye nyumba nenda mfate ongea nae face to face tia mkazo kua unafanya hiki upo kwangu fata rules za hapa hutaki go pack yo things and leave....hutaki unakuja kusema huku anyway tunakushauri tu ila ukweli mwambie kaeni naw chini mwmbie halaf wife kamshindwa how old is yo wife??? Huyo anaewatia joto ana umri gani??? Hiv nyumba yenu wenyewe mnapandwa.vichwani kama mmepangisha!!!

Mengine hayanipati kwa kweli bora ndugu wanione nina gubu ila naish na mume wangu kwa amani.
 
Mie huwa nabaki nimepigwa na bumbuwazi tu kwa jinsi watu wanavyojianika hadharani kwa watu ambao hata hawawafahamu nabaki kutoa macho tu :A S-eek: :A S-eek: :A S-eek:..... Nooooo you did not write this!!!! kisha huwa nasepa zangu kimya kimya bila kutoa neno. Watu tunatofautiana sana hapa duniani.


 
Mbona hata humu tumejaa, na tunajijua tumegeuka limutuz...oh sorry nimejikuta tu sijamaanisha.
 
I can imagine your frustration. Huo ni ugonjwa bwana; unaitwa selfiosis nadhani.
Dawa ni kuweka mguu chini. Mbona mie nimeweza kuwachapa mkwala ndugu na marafiki kuwa huko fb staki sura yangu ionekane? Its ok kutoa picha za ubwabwa, ila mambo ya checked in sijui na family yote kwa majina, ni umasai wa hatari sana.
Mfano ukikataa asiwapige picha itakuwaje?
 
Ni ulimbukeni tu unamsumbua na posibly yuko under 25 hajajielewa vya kutosha. Kwa ulimbuken huo naimani atapata wanaume wa mitandaon na watampiga mimba jiandae kumtunza akiwa mjazito
 

hata nimewaza inamaana hizo picha anapiga kisirisiri au
 

Hivi hujasoma amesema ameshamkanya mara nyingi na anaahidi kubadilika lakini baada ya siku moja?? Aongee nae kwa lugha gani sasa?
 

Hahahaa duuh....umasai??
 
Hivi hujasoma amesema ameshamkanya mara nyingi na anaahidi kubadilika lakini baada ya siku moja?? Aongee nae kwa lugha gani sasa?

Hatujaelewana nimesema achukue maamuz kama mwenye nyumba kusema na mtu husikiii ndo ukae uridhike??? Hakusikii kwa hiyo unamfanyaje na ndo mana nikasema amwambie afate rules za nyumban.kwake la binti hataki asepe pale sio kwake n yy ndo mwnye mamlaka napo upo
 
Anapiga wazi lakini huwezi kudhani atakimbiza fb ama insta. Dawa ni kutoa disclaimer kabisaa jamani mi staki mambo yangu huko fb. Hata nikishare picha ya sceneries staki kusema wapi coz i aint a travel consultant!

Shigdddeh!
hata nimewaza inamaana hizo picha anapiga kisirisiri au
 
Hajajielewa huyo! Akisha kuwa mtu mzima kichwani automatically utamuona katoka kwenye mitandao mwenyewe!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…