father-xmas mimi nakubaliana na wewe kwamba uhalisia kamili wa biashara hauzungumzwi.
Mimi nina miti ya teak niliipanda 1994, watu wanasema miti ya teak inatafutwa sana. Lakini mi nimetafuta hao wanunuzi mpaka sasa sijapata. Maneno tu meengi lakini ukweli wenyewe tofauti
Hongera sana mkuu.(
Sina lengo la kum discourage yeyote,hii ninayoongelea ni expirience yangu.
Hebu naomba uniambie wewe ulilima wapi,umevuna gunia ngapi kwa ekari,umeuza bei gani kwa gunia na uliuzia wapi.
Mkuu sifalima kwa simu kama unavyodai,nilikwenda mwenyewe front line.
Halafu pia ungeweza kutoa hoja bila kutumia hiyo ´wtf´
Pole sana, kilimo ni kigumu sio kirahisi kama watu wengi wanavyosema, mfano mm nililima mahindi na nimeshavuna bei iliyopo sokoni kwa sasa ni ya kutupa, nimeyaivazi (gharama za kuyaivazi pia ni kubwa) nione adi mwakani mwezi wa kwanza bei itakuwaje
kaka tafadhali naomba kuwasiliana nawewe kwa kina juu ya kilimo hiki,nataeajia kuingia ktk kilimo hicho msimu huu,so if possible naomba unisaidie kwa swala la mbegu bora na mchanganua wa gharama,tafadhali kaka naomba tuwasiliane,mimi nipo Morogoro,contacts zangu ni 0714 808196,0765781288.
Mkuu naogopa kukupa maelezo kwa sababu nikikuelezea njia nilizotumia mimi mwisho wake na wewe utaishia kupata hasara kama niliyopata mimi.
Mimi na wewe tunahitaji darasa kutoka kwa wataalam wetu kina Malila.
Kuhusu mbegu bora sidhani kama mbegu niliyotumia ni bora maana ingekua bora nisingepata mavuno machache kiasi kile.
Mimi mbegu nilinunulia kule kule shambani na niliamiwa ni mbegu nzuri na hata ilipoanza kuota watu waliisifia sana ile mwisho wa siku ikawa hasara.
Bado sijajua nilikosea wapi,sijui tatizo ni mbegu au kuna kingine nilichofanya kimakosa.
Nitalima tena,ila kabla sijalima tena lazima nijue nilichokosea ili nisirudie kosa.
Ruaha mbuyuni hapafai, vibarua shida, wanaolima wengi, badili location, kitunguu kitakutoa. Nenda japo mbeya au dumila au hata kifaru moshi
Heshima kwenu viongozi wangu.
Wakuu natumai hamjambo na mnaendelea vyema na shughuli za ujenzi wa taifa letu.
Wakuu baada ya kusikia wengi wetu wakisifia sana kilimo cha vitunguu nikapata muamka na mimi nikaingia katika kilimo cha vitunguu.
Nilikodisha ekari sita pale Ruaha Mbuyuni.
Kwa kweli sitaki kusema mengi ila ninachoweza kusema ni kwamba kutajirika kwa kilimo cha vitunguu LABDA inawezekana lakini sio kiurahisi kama wengi wetu wanavyohubiri humu.
Kwa EKARI ZOTE SITA nilizolima nilivuna gunia mia moja na tano tu.
Gunia moja niliuza kwa shilingi elfu thelathini tu.
Nilivuna mwezi wa saba mwaka huu ,2014.
Nilitumia shilingi karibia MILIONI KUMI NA TATU kulima ekari zote sita halafu nilipovuna nikapata shilingi milioni tatu laki moja na elfu hamsini hivi.3,150,000 kutoka kwenye mavuno ya ekari zote sita.
Nilikua makini sana kutimiza mahitaji yote niliyoambiwa nikitimiza nitavuna na kupata faida.
Anayetaka kuingia kulima na aingie ila tuwaeleze wenzetu ukweli,hichi kilimo ni very risky.
Anyway,mwakani nitalima tena maana jamaa wamenishawishi sana wakidai hasara ya mwaka huu isinikatishe tamaa.Nashindwa kusema kama kinalipa au hakilipi kwa sababu nimelima mara moja tu.Matokeo ya mwaka kesho ndio yatanipa uamuzi wa kujikita kwenye kilimo au kujitoa na kuwaachia kina Malila.
Kitu nilichogundua ni kuwa watu wengi humu hawasemi ukweli kuhusu hichi kilimo.
Nimekutumia simu ya mdau mwenzako aliyepo Iringa ambaye naye amekutana na kadhia hiyo msimu huu. Jaribu kupata mawazo yake ili usirudie kosa.
Ila kwa mawazo yangu, nadhani tatizo liko kwa vijana/wazee wa kazi ulio watumia. Kuna wafanyakazi mabingwa wa kuwaliza watu, hata mimi nimekutana nalo hilo pale Mkuranga,lakini baada ya kubadili njia ya kupata wafanyakazi afya ya shamba inaimarika sana.
Tanzania watu wanafanya kitu kwa kusikiliza story za watu
Mkuu hebu acha uongo bana. Au unaogopa watu wengi wataanza kulima soko lifurike vitunguu? Nilidhani umelima Kwa simu watu wakakuibia huko na kukudanganya. Lakini kama ulikuwa unakwendaa mwenyewe na kila hatua muhimu ulikuwepo huwezi kuvuna gunia 18 Kwa ekari moja, NARUDIA kusema huwezi kuvuna magunia 18 Kwa ekari moja. Kama ulisimamia mwenyewe namna ile na ukavitunza vitunguu lazima upate gunia si chini ya 60 Kwa ekari moja NARUDIA kusema kama ulisimamia hatua muhimu mwenyewe na kila wiki ulikuwa huko huwezi kukosa gunia 60 Kwa ekari moja. Hapo ungekuwa na gunia 360 na Kwa bei ya chini ya 50,000 Kwa gunia Kwa uchache ungepata milioni 18. Vilevile nina mashaka na matumizi ya milioni 13 kwenye ekari 6 si kawaida.Shukruni mkuu.
Nilikua nakwenda kila wiki.
Kila lilipofanyika jambo la muhimu mfano kutia mbolea kumwagilia madawa au palizi nilikuwepo mwanzo hadi mwisho.
Wakati wa kuvuna mpaka kuuza nilikuwepo.
Kwa kifupi sijapoteza pesa tu,bali nili invest muda wangu mwingi sana.
Mkuu hebu acha uongo bana. Au unaogopa watu wengi wataanza kulima soko lifurike vitunguu? Nilidhani umelima Kwa simu watu wakakuibia huko na kukudanganya. Lakini kama ulikuwa unakwendaa mwenyewe na kila hatua muhimu ulikuwepo huwezi kuvuna gunia 18 Kwa ekari moja, NARUDIA kusema huwezi kuvuna magunia 18 Kwa ekari moja. Kama ulisimamia mwenyewe namna ile na ukavitunza vitunguu lazima upate gunia si chini ya 60 Kwa ekari moja NARUDIA kusema kama ulisimamia hatua muhimu mwenyewe na kila wiki ulikuwa huko huwezi kukosa gunia 60 Kwa ekari moja. Hapo ungekuwa na gunia 360 na Kwa bei ya chini ya 50,000 Kwa gunia Kwa uchache ungepata milioni 18. Vilevile nina mashaka na matumizi ya milioni 13 kwenye ekari 6 si kawaida.
Mkuu umenikumbusha kilichonipata mwaka jana nilipolima pale RUVU. Wenyeji walinipa moyo sana kuwa nitavuna lakin hakuna nilichoambulia. Iliniuma sana lakin maisha yanaendelea...!!
Mkuu malila unatisha kwelikweli nimesoma michango yako mingi humu JF.....niwe muwazi kuwa unasaidia sana. pointi zako zina kilo nyingi. mi bila shaka najipanga ili nianze kupanda miti huko maeneo umesema yanapatikana. kama utapata mda naomba uni-pm contacts zako.Miti ya Teak ina maelezo ya hivyo mengi sana, ila ninachojua ni kwamba, ni kwa scale kubwa ndio unaweza pata soko la maana. Sasa kama una scale ndogo ya shamba itakuwa taabu kidogo. Mfano eka kumi za Mitiki kule Kigoma, mnunuzi anayetaka magogo kama laki moja atakuja kweli? Kwa small scale, teak ni hasara sababu inachukua miaka mingi sana mpaka kukomaa,ndio maana kwa watu binafsi ni mtihani kidogo.
Habari ya mitiki kama unaitaka hasa, basi nenda Longuza Tanga, Kilombero na Lindi ktk misitu ya serikali ambako hata mvunaji anaweza leta mitambo toka nje akijua atapata faida.
Mkuu malila unatisha kwelikweli nimesoma michango yako mingi humu JF.....niwe muwazi kuwa unasaidia sana. pointi zako zina kilo nyingi. mi bila shaka najipanga ili nianze kupanda miti huko maeneo umesema yanapatikana. kama utapata mda naomba uni-pm contacts zako.
natanguliza shukrani nyingi kwa kazi nzuri. mana tukizubaa wakenya watamaliza maeneo na tuishie kulalamika.