Expansion joints kwenye miradi ya Ujenzi ni kitu gani? Tuendelee kujielimisha

Ki Mun

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
3,443
4,384
Jamani mimi na umwakalinga wangu najiuliza tu - hivi hizo expansion joints tulizoelezwa na wazee wa TBA kwa kawaida zinapaswa kuwaje, zig-zag vile kama tulivoona hizi za Dr Magufuli Hostels au zinapaswa kuwa straight???

MIMI sijui lolote kuhusu tasnia ya ujenzi japo nina kakibanda changu nilichojengewa na rafiki yangu mmoja anaitwa Engineer Jo - japo sijui lolote lakini sikumwacha afanye anavotaka na kakibanda hakina expansion joints zozote zile, potelea mbali kakishindwa kuhema na kashindwe tu

Swali la msingi: expansion joints, kama ni lazima ziwepo kama TBA walivyotarajia ziwepo, zapaswa kuwa zig-zag or straight, or vyovyote?
 
Na hizo expansion joints ni aje...ni miradi ya nyumba tu au hata barabara? Je hii barabara hapa ni effects za hizo expansion joints au niaje?
DQNiT50XcAImXyH.jpg
 
Ni physics ya form 3 hiyo expansion na contraction
Ndio mana kwenyen madaraja kuna uwazi mdogo sana inapoishia lami na inapoanzia daraja,halikadhalika kwenye reli lazima iachane kidogo baada ya mita kadhaa
Alichozungumza yule muhandiIsi,kinadharia yupo sahihi japo hoja yake ingepata nguvu sana kama angeonesha drawings
 
Yani alichomaanisha bwana mhandisi/msemaji wa TBA ni kwamba ujenzi wa kisasa ni wa kuta kutanuka na kusinyaa. Sasa na kesho zile kuta mkikuta zimemwagika chini, msishangae, mjue huko kutakuwa ni ujenzi wa kupwa na kujaa kwa kuta.
Ndio maana hata waandishi wa habari walipofika eneo la tukio walikuta zile nyufaa zinesinyaa tofauti na yule dogo wakati anazipiga picha zilikuwa zimetanuka (expansion of joint) muda ule.
Mkumbuke tupo kwenye sela ya viwanda.

Msipofunikwa na vifusi "mkanya" hawamu hii sijui.
 
Hapo hakuna cha expansion joints wala nini! Kitu kimebuma tu wala wasidhani kuwa watafanikiwa kutudanganya! Je hiyo expansion joint IPO kwenye structural design na ikiwa zig zag hivyo! Maisha ya watoto yanawekwa rehani Kwa ajili ya kulinda nafasi za watu hapa! Kesho na kesho kutwa likibuma zaidi mtakuja na story IPI?
Napendekeza watoto wahamishwe toka kwenye hilo ghorofa na yafanyike marekebisho makubwa!
 
Kuna maeneo mengine udongo wake ukijenga nyumba Lazima kutatokea nyufa.....
Udongo kama huo kabla ya kujenga kuna taratibu/namna ya kufanya na ukajenga na hakuna nyufa itatokea

Ova
Kwenye ujenzi kuna kipengele kinaitwa defects liability time,sababu ni kama hizo
Hata bara bara ya mwendo kasi kuna sehemu kama sio korogwe au bucha imeoza
Ni jukumu la mkandarasi kurekebisha hali hiyo
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kwenye ujenzi kuna kipengele kinaitwa defects liability time,sababu ni kama hizo
Hata bara bara ya mwendo kasi kuna sehemu kama sio korogwe au bucha imeoza
Ni jukumu la mkandarasi kurekebisha hali hiyo
Swali?kwanini kabla ya ujenzi hawakebisha hizo mambo
Ndomana nasema ni uzembe tu

Ova
 
Jamani mimi na umwakalinga wangu najiuliza tu - hivi hizo expansion joints tulizoelezwa na wazee wa TBA kwa kawaida zinapaswa kuwaje, zig-zag vile kama tulivoona hizi za Dr Magufuli Hostels au zinapaswa kuwa straight???

MIMI sijui lolote kuhusu tasnia ya ujenzi japo nina kakibanda changu nilichojengewa na rafiki yangu mmoja anaitwa Engineer Jo - japo sijui lolote lakini sikumwacha afanye anavotaka na kakibanda hakina expansion joints zozote zile, potelea mbali kakishindwa kuhema na kashindwe tu

Mods msiunge huu uzi wataalamu watuelimishe hapa...swali la msingi: expansion joints, kama ni lazima ziwepo kama TBA walivyotarajia ziwepo, zapaswa kuwa zig-zag or straight, or vyovyote?

Swali:
Naomba kufahamishwa kuwa ni apartment ngapi zina share EXPANSION JOINTS?
><br />
 
Back
Top Bottom