Service hii ya Exim ni ya siku nyingi...This is a direction this country must use!
NMB, CRDB, NBC mko wapi??
Service hii ya Exim ni ya siku nyingi...
Wala si Credit Card, ni Debit Card.
Niliwahi kutumia Gold na niliumia vibaya (more than a year ago), card zinakuwa rejected sehemu nyingi!
CRDB wao nasikia inafanya kazi vizuri, tatizo usi-deal na branches za nje ya Jiji la Dar es Salaam kama una-apply, nenda Premier Branch (Benjamin Towers) na wambie unachotaka kufanya, wao watakupa maelekezo ambayo naamini yatakusaidia kwa urahisi. Tatizo matawi ya mabenki yetu ni kuwa na customer service isiyojali wateja, wengine hata services hizi hawajui kama zipo na hata kuzielezea hawawezi.
You can read this topic:
Using PayPal and MoneyBookers with CRDB VISA Card
Nimejaribu kufuatilia suala la credit cards za Exim na kupewa utaratibu wao kwa muhtasari. Ingawa wamejitahidi sana kutoa hiyo huduma, bado nadhani kuna vitu ambavyo wanatakiwa kutuelimisha. Kwa sasa ningeomba wenye uzoefu watusaidie ili tupanue ufahamu wetu na tuweze kuchangamkia hii huduma.
Inawezekana kuna taarifa nyingine lakini hizo ndizo nimekumbuka. Naomba kupata michango yenu wadau.
- Wanatoa kadi za aina mbili (Silver na Gold)
- Ili uweze kupata Silver, lazima uweke fixed deposit ya Tshs 1m (or $1000) na unaweza kutumia kwenye credit card yako hadi 80% ya hizo pesa ulizoweka kwenye fixed deposit. Kwa upande wa Gold, fixed deposit ni 5m ($5000). Pia unaweza kutumia hadi 80%.
- Kuna gharama ya kujiunga (kama sijakosea ni 25000) na kuna gharama nyingine nimesahau. Pia unatakiwa kulipa 50,000/- kwa mwaka.
- Ukitumia kununa vitu hakuna gharama ila ukichukua pesa kwenye ATM au cash machine yoyote unalipishwa 3%.
- Utaletewa muhtasari wa matumizi kwa mwezi na ukichelewa kulipa utalipishwa penalty ya Tsh 2500/- kila siku.
Service hii ya Exim ni ya siku nyingi...
Wala si Credit Card, ni Debit Card.
Niliwahi kutumia Gold na niliumia vibaya (more than a year ago), card zinakuwa rejected sehemu nyingi!
CRDB wao nasikia inafanya kazi vizuri, tatizo usi-deal na branches za nje ya Jiji la Dar es Salaam kama una-apply, nenda Premier Branch (Benjamin Towers) na wambie unachotaka kufanya, wao watakupa maelekezo ambayo naamini yatakusaidia kwa urahisi. Tatizo matawi ya mabenki yetu ni kuwa na customer service isiyojali wateja, wengine hata services hizi hawajui kama zipo na hata kuzielezea hawawezi.
https://www.jamiiforums.com/busines...pal-and-moneybookers-with-crdb-visa-card.html
Kiongozi ni kweli.
Ni majuzi tu hapa nimeenda tawi la CRDB la Mlimani City kuulizia kuhusu upatikanaji wa credit card mhusika anayehusika na kadi akanambia eti huduma ya credit card haipo CRDB! Nikapoteza appetite ya kuwa mteja wao. Naamini bongo kila kona wamejaa watu incompetent.