"Ukiona mwenzako ananyolewa, nawe tia maji", Bakili wa Muluzi utasumbuliwa sana unapoutaka tena uRais, japo kunaweza kuwa kuna ukweli katika mashitaka yako. Ila Afrika tunatafutana zaidi karibia na uchaguzi. Kumbuka yaliyompata Mzee wa kitambaa cheupe (Kenneth Kaunda) alipotaka kugombea tena uRais, aliishia kuwekwa ndani kama si juhudi za Mwalimu Nyerere kwenda kumuombea atolewe na kumshauri aachane na wazo la kugombea tena, jamaa (Kaunda) hatujui wangemfikisha wapi.