EWURA yatangaza kushuka kwa bei ya mafuta

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
20160301045253.jpg

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi amesema ‘kuanzia tarehe 2 Machi bei za mafuta zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la Februari 2016.

Kwa Machi 2016 bei ya rejareja za petroli imepungua Tsh 31 kwa lita sawa na 1.70%, Diesel imepungua Tsh 114 kwa lita sawa na 7.10% na mafuta ya taa yamepungua kwa Tsh 234 kwa lita sawa na 13.75%’

‘kwa kiasi kikubwa, kupungua huku kwa bei za mafuta kwenye soko la ndani kumetokana na kuendelea kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia‘
 
...kupungua huku naona hakuna maana sana,kwa sababu km mwezi huu inapungua,mwezi ujao inaweza ongezeka.Hivyo issue za msingi km kushuka kwa viwango vya nauli inakuwa haiwezekani,na mwananchi wa kawaida anaendelea kuumia tu,binafsi sioni maana ya wao kututangazia hizo bei zao kila mwezi.!!
 
Zaidi wanafaidika wenye magari
 
Duh! Naona ni heri kumiliki Cruiser kabisa sasa maana Diesel inashuka kwa kasi sana huku Petrol inajigusa kiduuchu mno hata tofauti siioni...
Hivi kwa nini inakuwa hivyo? Huwa najiuliza sana bei ya petrol kuwa juu zaidi ya diesel.
 
Ajabu sana, vituo vyote mji wa Mafinga vinauza mafuta ya petrol chini ya tsh 1710 hadi 1650tsh, leo hii EWURA wanasema bei ya mafuta kwa eneo hilo hilo imeshuka hadi 1800, only in Tanzania!
 
Mkuu dawa ni kuvuta Cruiser tu 1ltr/6 km ya diesel maana ukipiga hizi gar za petrol 1ltr/11km halafu ufanye mahesabu ya bei ya petrol inakuwa hamna ulichosave...Halafu nyingi huwezi kuvuruga nayo pori kama Cruiser.
 
Pamoja na kushusha bei, 51% na zaidi ya vituo vya mafuta vinapunja mafuta. Ukienda na kidumu maeneo mengi utakuta sh 10,000 unapata mafuta pungufu au sawa sawa na lita 5 ambayo inakuwa ni bei ya 2,000/- kwa lita.

EWURA wafanye uchunguzi kwa kuanzia na vituo vya OilCom, CamelOil na vingine vingi vya DSM.
 
Ajabu sana, vituo vyote mji wa Mafinga vinauza mafuta ya petrol chini ya tsh 1710 hadi 1650tsh, leo hii EWURA wanasema bei ya mafuta kwa eneo hilo hilo imeshuka hadi 1800, only in Tanzania!

Mafinga sitaisahau CamelOil ya hapa mwanzoni kabisa kabla ya kuingia mjini ukitokea Iringa, waliniwekea mafuta machafu siku moja, dah kidogo niue chombo.
 
Mkuu nmeliona hlo kuna kituo kimeandkwa offer petrol 1600 nilishtuka sana
 
Haiwezekani bei ya petrol ikapishana namna hii ni diesel kwa shs. 325/= hapa kuna usanii. Ewura acheni hii mambo mnakula na wafanya biashara nini maana miaka yote tofauti ya diesel na petrol ni wastani wa shs.100/=
 
Mafinga sitaisahau CamelOil ya hapa mwanzoni kabisa kabla ya kuingia mjini ukitokea Iringa, waliniwekea mafuta machafu siku moja, dah kidogo niue chombo.
Ndio maana nasema ni ajabu! Only in Tanzania!
 
Haiwezekani bei ya petrol ikapishana namna hii ni diesel kwa shs. 325/= hapa kuna usanii. Ewura acheni hii mambo mnakula na wafanya biashara nini maana miaka yote tofauti ya diesel na petrol ni wastani wa shs.100/=
Usanii wa Magu huo, uko kwenye wese si wametoka juzi tu kushtukiza ina maana hawaelewi kinachoendelea hapo?

Nchi ya kisanii hii, kama Rais msanii watendaji lazima wawe wasanii na wananchi lazima waige usanii huohuo ili maisha yaende kwa sababu ndiyo style aliyohalalisha Rais
 
Haiwezekani bei ya petrol ikapishana namna hii ni diesel kwa shs. 325/= hapa kuna usanii. Ewura acheni hii mambo mnakula na wafanya biashara nini maana miaka yote tofauti ya diesel na petrol ni wastani wa shs.100/=
Hata mie hapa sipaelewi kwa kweli. Sababu gani inayofanya petrol ishuke sh 31 wakati dizel 325? Huu uwiano wa unahitaji maelezo.
 
Ngoja Faiza Foxy aje hapa atoe ufafanuzi zaidi juu ya tofauti ya bei ya petrol na diesel kuwa zaidi ya Tshs 300. Yeye ni mbobezi kwenye nyanja ya mafuta na gesi kwa zaidi ya miaka 32.

Cc: Faiza Foxy
 
Back
Top Bottom