EWURA yatangaza bei mpya: Petroli yashuka, diseli yapanda

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza mabadiliko ya bei za mafuta nchini zitakazoanza kutumika kuanzia kesho, huku mafuta ya petroli yakionekana kushuka.

Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli, dizeli na ya taa zimebadilika ikilinganishwa na beo za Machi Mosi mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo katika Makao Makuu ya ofisi za EWURA, Meneja Mawasiliano ma Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo amesema, bei ya reja reja ya petroli imepungua kwa Shilingi tatu kwa lita ambayo ni sawa na asilimia 0.13, pianbei ya jumla imepungua kwa Shilingi 5.65 kwa lita sawa na asilimia 0.29.

Aidha Kaguo amesema bei ya rejareja ya Dizeli imepanda kwa Shilingi saba kwa lita sawa na asilimia 0.36 wakati bei ya jumla ikiwa imepanda kwa Shilingi 3.68 kwa lita sawa asilimia 0.21.

"Hii shilingi tatu inaweza kuonekana ni ndogo lakini ina impact () kubwa sana kwa jamii, kwa kiasi kikubwa mabadiliko haya yametokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia, mfumuko wa bei, pia gharama za usafirishaji ikilinganishwa na mwezi uliopita," amesema Kaguo.

Chanzo: Habari leo
 
Back
Top Bottom