EWURA yashusha bei za umeme kwa watumiaji wa viwango tofauti

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,629
34,172


TANESCO.JPG


Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji EWURA imetangaza kushusha bei za umeme kuanzia leo kwa watumiaji wote wa viwango tofauti.

Kushuka huko kwa bei ya umeme ni kutokana na ombi la Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kutaka bei za umeme zipunguzwe sambamba na hilo gharama za huduma kwa baadhi ya wateja zimeondolewa.


Chanzo: ITV
 
tanesco%284%29.jpg

Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji EWURA imetangaza kushusha bei za umeme kuanzia leo kwa watumiaji wote wa viwango tofauti.Kushuka huko kwa bei ya umeme ni kutokana na ombi la Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kutaka bei za umeme zipunguzwe sambamba na hilo gharama za huduma kwa baadhi ya wateja zimeondolewa.
Source:ITV
hongera. hii ni ya kufurahia sana. mm nikinunua luku(hiyo service charge) mpaka machozi yana lengalenga.....
 
hongera. hii ni ya kufurahia sana. mm nikinunua luku(hiyo service charge) mpaka machozi yana lengalenga.....
Service charge mbona nasikia walikataa?
Nilisikia wanapinguza 1% na ile 5000 na ushee ya kununua fomu ya maombi ya kuweka umeme kwa mara ya kwanza ndo wanatoa. Nilisikia hivyo.
 
Duh! Wajinga day au?
Pamoja na kuwa leo inalazimishwa kuitwa siku ya wajinga lakini mwezi wa tatu mwaka huu TANESCO waliwasilisha kwa EWURA ombi la kupunguza gharama za umeme kwa awamu ikiwa ni pamoja na monthly service charges. TANESCO, EWURA, REA, EWURA Consumers Consultative Council na wadau wengine mbalimbali waliendesha mjadala wa pendekezo hilo na mabadiliko ya bei hizo yalitakiwa yaanze leo tarehe 1 April 2016. Kwa hiyo hii taarifa japo haijatoa maelezo zaidi lakini itakuwa na ukweli.
 
ewura wanapunguza kidogo sababu wao wanapata kamisheni ya 1% ya bei ya umeme unayonunua ndio maana wanajilipa mishahara ya ajabu
 
Ingekua jambo la kheri kwa sababu tarehe kumi na tano nilinunua umeme wa 20000 nikapewa unit 35 tu
 
Back
Top Bottom