EWURA imetangaza bei mpya za Mafuta, yamepanda bei tena

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,517
8,442
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA BIDHAA ZA MAFUTA YA
PETROLI KUANZIA JUMATANO, TAREHE 1 MEI 2024

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano, tarehe1 Mei 2024 saa 6:01 usiku. Kwa mwezi Mei 2024, bei za rejareja na za jumla katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ni kama zinavyoonekana katika Jedwali
Na. 1 na 2, mtawalia.

JEDWALI 1: BEI KIKOMO ZA REJAREJA (SHILINGI/LITA)

Mkoa wa Dar es Salaam Petrol 3,314, Dizeli 3,196 Mafuta ya Taa 2,840

Tanga 3,360 3,242 2,886
Mtwara 3,317 3,200 2,913


 
Sasa vyombo vinavyotumia petrol kama magari yenye cc kubwa used yatauzika kweli?
 
Ukiona bei ya mafuta inapanda kwa kasi ya ajabu kila mwezi! Halafu ukipita kila sehemu (mpaka kwenye makazi ya watu) unakuta vituo vya mafuta navyo vinajengwa kwa kasi ya ajabu! Kwa mtu mwenye akili timamu, unapata majibu sahihi ya nini kinachoendelea nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…