EWURA: Bei ya umeme kupungua wakati wowote

EWURA: Bei ya umeme kupungua wakati wowote

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,486
Wakala wa Udhibiti na Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), umetangaza kuwa wakati wowote kuanzia sasa serikali itapunguza bei ya umeme baada ya gharama za mafuta kupungua katika soko la dunia.

Tanesco inauza 'uniti' moja ya umeme kwa Shilingi 306 na pia hutoza tozo la Shilingi 7,000 ambalo halina kuhojiwa wala kupingwa likidaiwa ni la kuendesha shughuli za Ewura, Wakala wa Umeme Vijijini (REA) na kodi ya VAT.

Kaimu Mkurugenzi wa Umeme wa Ewura, Godfrey Chibulunje, alisema wakati wa mkutano wa wadau wakiwamo viongozi vya vyama vya siasa visivyo na wabunge.

Alitoa ufafanuzi huo baada ya viongozi hao kuwabana wataalamu hao na watendaji wa wakala huyo, Shirika la Umeme la Tanesco kueleza kwa nini hawashushi bei za umeme wakati mafuta yameshuka.

Aidha, Chibulunje alisema serikali ipo katika mchakato wa kupitia mwenendo wa kupungua kwa bei ya mafuta kwa lengo la kuangalia namna ya kuwapunguzia mzigo wananchi.

‘’Muda si mrefu wananchi wataona matokeo ya kuanguka kwa bei ya mafuta, tunachokifanya ni kupitia gharama ya ununuzi wa mafuta mazito na kiasi gani wananchi wanaweza kuondokana na mzigo wa kununua umeme,” alisema.

Walihoji pia sababu za kuuza umeme ghali wakati kampuni binafsi ya kuzalisha umeme ya IPTL imeshusha bei. Chibulunje alisema hana taarifa kuwa IPTL imepunguza bei ya umeme inaouza Tanesco.

“Kama serikali tulisikia taarifa hizo kwenye vyombo vya habari, tunachojua IPTL inauza umeme kwa bei ya zamani, hizo taarifa ya kushusha hatuna na kama zipo hazijatufikia kiofisi,” alisema Chibulunje.

Alifafanua kwamba kiutaratibu kama kampuni au shirika linataka kupunguza au kupandisha bei ya huduma lazima inawasilisha mapendekezo ofisini kwake kwa ajili ya kufanyia kazi, hata hivyo haikufanyika jambo kama hilo.

Awali, Mwenyekiti wa makatibu wa vyama 12 vilivyoshiriki katika mkutano huo, Ali Kaniki, alisema wanasikitishwa na hali ya wananchi kuendelea kuteseka na kubebeshwa gharama kubwa ya huduma hiyo wakati kuna baadhi ya kampuni zimeanza kushusha bei ya umeme.

Chanzo: Nipashe
 
sioni credit yoyote kwa CCM na serikali yake kwani hakuna intiative yao katika hilo!!!
 
sioni credit yoyote kwa CCM na serikali yake kwani hakuna intiative yao katika hilo!!!

Ewura sio wakweli, ni bora tu wakakaa kimya kuliko kuleta matumaini ambayo hayapo! Tanesco waliambiwa wafanye recalculation bei ishuke wao wakaleta!
 
Duuuh! Kweli kampeni za urais zimeanza
 
Zile za Escrow zimewatosha maccm? Hatuamini lolote mpaka uchaguzi upite. Hapa hakuna shirika lolote la kukamua kama Tanesco hivyo kupunguza bei ya umeme ni kuikosesha ccm pesa ya kununulia kofia na flana zenye picha ya nambari one.
Uongo huo, kawaambie lumumba pale.
 
Sitaki kusikia ahadi yoyote ile toka ccm kwa sasa.
 
Sitaki kusikia ahadi yoyote ile toka ccm kwa sasa.

Mkuu wewe sikiliza tu usipate shida, kwani hizo ni Kampeni zao. Sisi wanamageuzi ikifika mwezi October nchi tunawakabidhi UKAWA. CCM hata washushe umeme kwa mwezi tuwe tunalipia elfu 5 lakini kura hatuwapi mwaka huu. CCM wajiandae kukabidhi nchi kwa wapinzani.
 
Kama bei ya mafuta katika soko la dunia ingelipanda na hivyo kuhitaji kupandisha bei ya umeme mngelisema msubiri mpitie makaratasi na sijui documents gani? tena kwa kusukumwa? siku ya pili tu mngetoka na bei ya unit isiyo na kichwa wala miguu. Lakini leo kwsbb inahusu punguzo la bei eti msubiri mupitie makaratasi yenu tena kwa mwaka mzima, wezi wakubwa nyie tanesco, EWURA na IPTL. Hata mkishamaliza hizo calculation zenu muje na porojo zenu mafuta yashapanda tena.
 
Sidhani kama hili litatekelezeka!

Uzalishaji wa umeme hautegemei mafuta peke yake, hivyo kushuka kwa bei ya mafuta si kigezo pekee cha kuangalia katika kushusha bei ya umeme.

Si bado tunategemea umeme unaozalishwa na maji pamoja na gesi?! Hivi navyo vimeshuka bei?!
 
mafuta hayapandi tena labda itokee vita kubwa
 
Bunch of ------ yaani tukinyamaza wananchi yanaendele kutuibia tu, bei ya matuta yenyewe mpaka timuhoji na yanashuka kwa kusua sua nchi nyingine walisha shua bei siku nyingi
 
Sidhani kama hili litatekelezeka!

Uzalishaji wa umeme hautegemei mafuta peke yake, hivyo kushuka kwa bei ya mafuta si kigezo pekee cha kuangalia katika kushusha bei ya umeme.

Si bado tunategemea umeme unaozalishwa na maji pamoja na gesi?! Hivi navyo vimeshuka bei?!

Gesi ni moja Ya product Ya mafuta
 
Back
Top Bottom