Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,289
- 2,472
Ulisema wewe ni mtumishi wetu na sisi ni marais! Ulisema. Sasa tusikilize na ufanyie kazi utakayosikia. Wakati wa harakati za Baba wa Taifa, aliwahi kuainisha maadui watatu; ujinga, umasikini, na maradhi. Ili kukabiliana na maadui hao, vilihitajika vitu vinne; watu, ardhi, siasa safi, na uongozi bora. Basi! Kama hamjui hiyo ndio dira ya Taifa. Tusipopita humo, iwe ni ccm au chama kingine pinzani ni kwamba tunapigana na kivuli tu.
Kwani hadi leo nusu karne tumefanikisha lipi kati ya hayo? Magonjwa yapo palepale. Tunahangaika tu na kwa hisani ya watu wa Marekani kutuletea neti. Ujinga ndio usiseme. Juzi tumewapoteza wataalam wa masuala ya ardhi kisa imani za kijinga za unyonyaji damu. Wakachomwa moto hadi kufa. Si wa kulaumiwa kiasi hicho. Wawakilishi wao walishindwa kupeleka elimu ili waondoe ujinga. Umasikini ndio ada yetu.
Watu tupo. Tunatumikaje? Au matumizi yetu ni wakati wa kampeni na uchaguzi tu? Au ndio hao kina vi.laza wanaobezwa. Mkuu juhudi zako tunaziona, lakini hazitoshi. Delegation of power ni jambo la msingi sana. Ni sehemu ya dira ya taifa. Kauli zako zisiwe ndio tamati. Umeteua wasaidizi kufanya kazi kwa niaba yako sehemu mbalimbali nchini. Waache wafanye kazi. Mfano leo utasema wamachinga waondolewe. Wanaondolewa kweli na wanakamatwa na kuwekwa ndani kwelikweli. Kesho unasema waachiliwe wafanye buashara kwa uhuru. Wanaachiwa kweli na wanasumbua kweli mfumo rasmi wa ufanyaji biashara. Unawasumbua wafanyabiashara wanaolipa kodi hakali. Unawasumbua wateja maana njia zao zinazibwa na wafanyabiashara. Unapoteza trust kwa wafanyabiashara na wateule wako. Kazi yao ni ipi? Watu. Watumie watu kwa manufaa ya taifa na sio kikundi fulani.
Ardhi siisemei sana maana ni kelele za kila leo. Tunashindwa kutenga ardhi kwa wafugaji na wakulima. Tunashindwa kuingia mikataba ya maana na wawekezaji juu ya ardhi yetu. Mtu mmoja anamiliki ardhi ukubwa sawa na nchi. Si sawa.
Siasa safi. Hapa mtumishi ndio umefeli kabisaa. You cannot hold other things constant while you practise others. Haya mambo yanaenda sambamba. Siasa zikiwa mbovu, watu lazima wawe hovyo hovyo tu. Tunajua ni kwa jinsi gani unatamani kufanya kazi zako bila rabsha za upinzani na kukosolewa. Ukaanza na kufungia shughuli za kisiasa hadi 2020. Ukaona haitoshi ukatamani mitandao ya kijamii ifungiwe. Siasa ni kama kikohozi. Huwezi kukizuia. Utakohoa tu. Sugu alisema huwezi kuzuia mvua. Itanyesha tu. Sasa watu wamekatazwa siasa za majukwaa ulidhani watalala? Ndio wamehamia kwenye mitandao sasa. Zuia mitandao ndio utashuhudia kina Shekau wakiibuka.
Siasa safi si kutokuwa na upinzani. Ni kujua namna ya kuishi na upinzani. Nguvu yao ndio matokeo yako leo. Kama uliweza kufaulu mitihani kwa kuikabili kwa hoja na kuwa Daktari, unashindwaje kujenga hoja dhidi ya wapinzani? sasa hapa tunaanza kuamini kuwa tatizo si upinzani bali ni mfumo.
Wakati niko A level kuna kitabu cha non fiction cha fasihi tulisoma. Kinaitwa Soledad Brothers. Kitabu kinawahusu wamarekani Ndani yake kuna msamiati mmoja unaitwa internecine violence. pale ambapo mtu anamalizia hasira kwa vitu/watu wengine baada ya kushindwa kukabili tatizo linalomsibu. Hawa wamarekani walikuwa wanafanyiana fujo pamoja na kuuana ikiwa ni matokeo ya kushindwa kumkabili mzungu.
Hii leo ndio yanayotokea kwetu. Ccm inashindwa kukabiliana na mzimu wake mwenyewe. Wanatokea wapinzani ( ukawa) wanaonyesha tatizo lilipo. Mtawala anashindwa kukabiliana na tatizo hilo maana ni sawa na kujibandua ngozi. Mtawala anaamua kumkabili mjumbe na kumfungia siasa na kuacha tatizo likiendelea. Hizo sio siasa safi. Siasa safi ni kushindana kwa hoja na si kuwekeana visasi na vitisho. Unaanzaje kujisifu kupambana na mtu aliyefungwa pingu halafu wewe una ngao, helmet, mjeledi, risasi n.k? Ni ujinga wa hali ya juu.
Uongozi bora ni pamoja na kuwajibika na si kusubiri kuwajibishwa. Ni pamoja na kusikiliza mashauri ya wataalam na kuyafanyia kazi. Ni hekima. Wananchi wanaiona hekima ndani ya viongozi wao? Uongozi ni ushawishi na si vitisho. Ni utawala wa sheria na si kupindisha sheria. Ni kusikilizana na si kusikilizwa tu. Uongozi ni subira. Ni kuainisha vipaumbele. Uongozi ni mipango na maono ya mbali kwa wakati uliopo.
Mfano kulikuwa na uharaka gani wa kununua hizi ndege sasa hivi? Tuna mashurika kama fastjet na precision air. Mashirika ambayo yanafanya safari za anga za ndani ya nchi. Kwa nini serikali inataka kushindana nao? Kwa nini serikali isingevuta subira kidogo ikakusanya hela na kununua boeing kama mbili kwa ajili ya masafa marefu? Kipaumbele ni viwanda, ndege, au kupambana na ufisadi?
Ningemsifu sana mtumishi kama angekuwa anasema kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji, na akaendekea kuchapa kazi. Kwani kinachoshindikana ni nini? ni ngumu kuelewa. Wachache wataelewa kuwa uongizi huu unataka kuficha madhambi. Wanazuia hadi bunge. Mwisho atazuia na hotuba zake akiamini zitawanufaisha wapinzani.
Dira ya taifa ni watu, ardhi, siasa safi, na uongozi bora. Mwenye hekima na asikie. Mwenye kisasi na alipize