Ewe Mtanzania na Mpiga kura Ifahamu Nchi yako Tanzania

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,459
29,157
Haya ndio mambo nayoyafamu kuhusu TANZANIA
1. Tz ilipata uhuru mwaka 1961 ina miaka 54 tangu ipate uhuru ikiwa ni ya kwanza afrika mashariki.

2. Tz Kwa miaka 38 hii inchi imeongozwa na ccm peke yake ambayo ni zao TANU na ASP.

3. Tz ni nchi ambayo hajawahi kupata majanga makubwa kama matetemeko ya ardhi,magonjwa ya mlipuko kama ebola,mafuriko na vimbunga au ukame.

4. Tz ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho nnchi za Africa zimekikosa AMANI kwa miaka yote 54 ya uhuru hajawahii kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.

5. Tz ina ukubwa ukubwa wa 945,000 km square yani sawa na uchukuwe Denmark,France,United kingdom(uk),Netherland,Ireland ujumlishe zote kwa pamoja.

6. Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424 kilometers bahari inaleta fursa za usafirishaji,uvuvi,utalii na nyinginezo.

7. Tz ni nchi ambayo imepakana na nchi za (Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, Drc congo) ambazo zinategemea bahari yetu kwa usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu

8. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine madogo mengi.Maziwa matatu makubwa yako kwenye kumi bora za ukubwa duniani na Maziwa makubwa matatu yote yapo Tanzania..Ziwa Victoria ni la tatu kwa ukubwa duniani(la kwanza afrika) na ziwa Tanganyika ni la sita kwa ukubwa(la pili afrika) na la kwanza kwa kuwa na kina kirefu duniani.Ziwa nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani(ni la tatu afrika).

9. Tz ina mito mikubwa kumi ambayo ni mto kagera,mto Ruvuma,mto rufiji,mto wami,mto maragarasi,mto mara,mto pangani,mto mara,mto gombe,mto mweupe wa nile.na ina mito midogo mengi kama mto kilombero,mto mbemkuru n.k

10. Tz ndiyo nchi ya kwanza afrika kuwa na maji mengi yasio na chumvi yaliyokuwa kwenye uso wa dunia(fresh surface water) kutokana na kuwa na mito na maziwa mengi na kupitiwa na bonde la ufa.

11. Tz ni nchi ya nne kwa uzalishaji dhahabu afrika baada ya afrika kusini, ghana na mali na ipo top 20 duniani. Kuna migodi nane inayochimbwa dhahabu na miwili imefungwa. migodi inayochimbwa ni Buzwagi gold mine-(Shinyanga), Geita gold mine-(Geita), Golden pride gold mine-Nzega(tabora), Bulyanhulu gold mine-(Shinyanga). New leuka Gold mine-(Mbeya), Tulawaka gold mine-(kagera), North mara gold mine-(mara). Iliyofungwa ni Kirondatal gold mine-(Shinyanga), Senkenke gold mine-(Shinyanga).

12. Tz ina madini ya almasi yanayopatikana mwadui shinyanga mgodi huo umeanzwa kuchimbwa tangu mwaku 1940 mbaka leo ado unachimbwa,unamilikiwa nakampuni ya wingereza.

13. Tz ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee inayozalisha madini ya tanzanite duniani.mkufu wa kuva shingoni unatengenezwa na tanzanite na almasi unauzwa hadi milioni 25 za kitanzania.

14. Tz ina madini ya chuma yanayopatikana mchuchuma,ludewa- njombe mgodi unamilikiwa na wachina mgodi huo una hifadhi ya madini ya chuma tani milioni 122 ambayo yanawezwa kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 100.

15. Tz ina madini ya makaa ya mawe yanayochimbwa kule kiwira mbeya,mchucuma na liganga njombe unamilikiwa na wachina pamoja na ngaka kule mbinga-ruvuma unamilikiwa na kampuni ya tancoal ya Australia.hifadhi ya madini ya makaa ya mawe iliyopo ni tani bilioni 2.makaa yam awe ndio chanzo cha pili ya umeme wabei nafuu duniani baada ya maji.

16. Tz ina hifadhi ya madini ya uranium kule Dodoma(bahi) na mgodi ambao unamilikiwa na warusi pia madini haya yanapatikana pia Namtumbo (Mkuju), Galapo, Minjingu, Mbulu, Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea, Tunduru, Madaba and Nachingwea.

17. Tz ni moja ya nchi tatu Africa pamoja Zimbabwe na madagascar kwa kuwa madini mengi ya graphite madini haya yapo Tanga,Mahenge-Morogoro,mererani-manyara.Madini ya graphite ndiyo yanayotumika kutengenezea betri za simu,kwenye injini na brake za gari na kwenye karamu ya risasi(pencili)

18. Tz ina madini ya nickel yanayopatikana kule kabanga kagera,milima ya ulurugulu-morogoro,north mara,Ngasoma-mwanza.

19. Tz ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na hifadhi kubwa ya magadi soda mengi duniani baada ya marekani na uturuki.magadi soda hutumika kutengeneza vioo vya aina zote vyo nyumbani hadi magari pia kutengeneza sabuni na dawa mbalimbali za usafi

20. Tz ina hifadhi na mgodi wa madini ya niobium uliopo Panda hill mbeya ambao ndio utakuwa mgodi mkubwa wa kwanza Africa na wanne duniani,mgodi huu unamilikiwa na kampuni ya uastralia.Madini ya nibioum ni magumu sana hutumika kutengeneza mabomba pamoja na madini chuma pia hutumika kutengeneza baadhi ya sehemu za injini za ndege na vyombo vinavyoenda nje ya uso wa dunia,vioo vya computer na lenzi za camera.

21. Tz ni nchi ya kwanza Africa na ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii duniani ya kwanza ikiwa brazil. Nchi zilizokuwa kwenye tano bora kwa utalii Afrika ni Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Kenya na Zambia.

22. Tz ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga maarufu kuliko zote duniani Serengeti na mbuga iliyopakana na bahari saadani na mlima mrefu kuliko wote Africa Kilimanjaro.

23. Nadhani kila mtz anajua juu ya sifa ya Tanzania kwenye swala ya kuwa na ardhi ya rutuba inayofaa kwa kilimo

24. Tz ina gesi ya asili ya carbon dioxide(CO2) inayovunwa kule kyejo, Rungwe-mbeya na kampuni ya TOL, gesi ya asili ya cardon dioxide inatumika sana kutengenezea vinywaji laini kama soda,bia, na pia kutengenezea madawa, kwenye viwanda vya makaratasi na kutibia maji.

25. Tz ina gesi ya asili inayopatikana katika kisiwa cha songo songo mkoa wa lindi gesi hii imekuwa ikichimbwa na kusafirisha Dar as salaam tangu mwaka 2004 na inayomilikiwa na kampuni ya songas ya uingereza

26. Tz imengundua gasi ya asili yenye ujazo wa zaidi ya trioni 55.3 cubic meter iliyongungulika katika maeneo ya bahari ya lindi na mtwara.

Pamoja na sifa zote hizi Lakini Tz ni nchi iliyo kwenye kundi la nchi maskini duniani ambao asilimia kubwa ya raia wanaishi chini ya dola moja na hali ya huduma za kijamii zikiwa duni.

TATIZO NI NINI?NI NANI ALIYESABABISHA HUU UMASKINI WA TAIFA HILI?
 
Back
Top Bottom