Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,723
hapo kwenye underline kuna maswali, ni majuzi tu nimesikia kitu ambacho sikuwahi kukijua hapa kabla, kuwa TFF ya uongozi uliopita ilikuwa ikipanga PPF Tower (???) na hii ya sasa wameamua kuiachia hiyo ofisi na kurudi 'nyumbani' yaani uwanja wa Karume. Je, hii habari ni kweli au nilisikia vibaya!?Evodius Mtawala ameachia ngazi ya ukurugenzi wa sheria na wanachama wa shirikisho la mpira wa miguu nchini -TFF, Taarifa kutoka ndani ya shirikisho hilo zinasema katibu mkuu huyo wa zamani wa Simba SC zinasema ukilitimba uliokithili ndani ya shirikisho hilo ikiwa ni pamoja na miundo mbinu mibovu ya utendaji ndani ya TFF ndio chanzo cha mwanasheria huyo kuamua kujiweka pembeni.
Sijapata kufuatilia kwa undani zaidi ila ukweli kaachia ngazi,nimeonana na ndugu yake wa karibu kanithibitishia hilo.Pia suala jingine alilosema ni kuhusu usajili wa Okwi kwa jinsi ulivyogubikwa na sintofahamu.
Huwezi kukataa moja kwa moja. Inawezekana Simba wamewekeza matumaini yao kwake juu ya swala hili, naye anahisi ni mzigo mkubwa kwake. Kuliko kusubiri lawama, huenda ameona ni vyema kujiondoa.Suala la Okwi bado halijajadiliwa, anaachiaje ngazi?! Lazma kuna sababu nyngne na si Okwi.
Huwezi kukataa moja kwa moja. Inawezekana Simba wamewekeza matumaini yao kwake juu ya swala hili, naye anahisi ni mzigo mkubwa kwake. Kuliko kusubiri lawama, huenda ameona ni vyema kujiondoa.
inawezekana pia kwamba anahisi Simba haitendewi au haitatendwa haki kwenye swala hilo, na kwa hivyo hataki kuhesabika kama Mwanasimba aliyechangia kuiuma Simba.
Mtu unalazimika kuamini hivyo kwa sababu kabla ya hapo hatkupata kumsikia akilalamikia uendeshaji ndani ya TFF. Tulichosikia ni wafanyakazi kulia njaa kwa kukosa mishahara. Lakini hili si miongoni mwa sababu alizozitaja za kuondoka kwake.
Bwana Evodius Mtawala hadi ninaandika post hii ni mfanyakazi wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania na anaendelea na wadhifa wake wa Mkurugenzi wa sheria na vyama wanachama.
Wewe ndiye au ni mtu anatumia id ya raisi
Kaka unabishana na Muajiri wake? unaamini maneno ya rafiki yako?mmmmh pole sana.Jamal Malinzi, Itanichukua muda kuamini maneno yako,habari hizi nimethibitishiwa na ndugu yake wa karibu ambaye ni rafiki yangu pia.Ni bora kuweka wazi suala hili kuliko kuendelea kukumbatia uongo.