GE2025 Eveline: Mkichagua NCCR-Mageuzi usalama kazini ni uhakika

GE2025 Eveline: Mkichagua NCCR-Mageuzi usalama kazini ni uhakika

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea mwenza wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha NCCR–Mageuzi, Dkt. Eveline Munisi, amesema kuwa endapo wananchi watamchagua mgombea urais wa chama hicho, serikali yao itaweka mazingira bora na salama kwa watumishi wa umma katika kipindi chote watakapokuwa madarakani.

Akizungumza katika muendelezo wa kampeni za chama hicho jana tarehe 30 Septemba 2025, akiwa katika Jimbo la Temeke, mkoani Dar es Salaam, Dkt. Munisi amewahakikishia wananchi kuwa usalama utaimarika kwa kiwango cha juu na kutakuwa na ulinzi wa kutosha wakati wote wa uchaguzi.

Aidha, amewaasa wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025, huku akisisitiza umuhimu wa kushiriki katika zoezi hilo kwa amani na utulivu, na kurejea nyumbani salama baada ya kutimiza haki yao ya kikatiba.

Katika hatua nyingine, Dkt. Munisi amewataka wananchi kudumisha amani ndani ya nchi, akieleza kuwa Tanzania imekuwa kimbilio la watu kutoka mataifa mengine wanaokimbia machafuko.

Pia Soma: GE2025 - Mgombea urais NCCR, Dkt. Munisi: Amani ya taifa letu ni dhamana yetu sisi wenyewe usisubiri askari aje kwaajili ya amani
 
Back
Top Bottom