Europa League: Chelsea hai,Newcastle hoi

Europa League: Chelsea hai,Newcastle hoi

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,347
Reaction score
26,153
Jana,timu ya Chelsea iliitandika mabao 3-1 timu ya Rubin Kazan katika mchezo wa Europa League. Mabao ya Chelsea yamewekwa kimiani na Torres-2 na Victor Moses. Nayo Newcastle ilibamizwa mabao 3-1 na Benfica ya Ureno. Ilikuwa inacheza ugenini Ureno.

Wakati huo huo, Tottenham Hotspur ilibanwa mbavu nyumbani na kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na FC Basel ya Uswis.Basel waliwahi kuwatupa nje Man United katika michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya kabla ya Man United kupigwa kumbo na Atletic Bilbao ya Uhispania katika Europa League.

Katika mchezo huo wa Hotspur,Gareth Bale aliumia na aweza kukaa nje ya dimba kwa majuma kadhaa. Katika mechi ya nne,Lazio ilizabwa mabao 2-0 na Farnabache ya Uturuki kwa mabao ya Webo na Kuyt.

Michuano yote hiyo ilikuwa ni michezo ya kwanza ya robo fainali za kombe la Europa.
 
Back
Top Bottom