Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,450
- 5,278
Bunge la Rwanda limelaani vikali azimio la Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) lililotaka kuachiwa huru kwa mwanasiasa wa upinzani Victoire Ingabire, likisema hatua hiyo ni kuingilia uhuru wa mahakama na mfumo wa kidemokrasia wa nchi hiyo.
Katika kikao cha pamoja cha Baraza la Wawakilishi na Seneti, wabunge wamesema azimio hilo, lililopitishwa Septemba 11, 2025, linakiuka misingi ya kimataifa ya kuheshimu uhuru wa mahakama na mamlaka ya kitaifa.
Bunge la EU lilitaka Ingabire na wanasiasa wengine wa upinzani walioko kizuizini waachiliwe mara moja bila masharti, na kwamba mashtaka ya kisiasa dhidi yao yafutwe. Ingabire, ambaye anaongoza chama cha upinzani cha DALFA–Umurinzi (ambacho hakijasajiliwa rasmi nchini Rwanda), alikamatwa Juni 19 mwaka huu kwa amri ya Mahakama Kuu kupitia Ofisi ya Upelelezi wa Rwanda (RIB), akihusishwa na wafuasi wake wanaotuhumiwa kujaribu kuangusha serikali.
Anakabiliwa na mashtaka sita, ikiwemo kujihusisha na kundi lenye nia ya kupindua serikali, madai anayoyakana. Bunge la Rwanda limeeleza kuwa kesi hiyo ni mpya na haina uhusiano na mashtaka ya zamani yaliyompelekea kufungwa miaka 15 mwaka 2010, kifungo ambacho alimaliza baada ya kupewa msamaha wa Rais Paul Kagame mwaka 2018.