dalalitz
JF-Expert Member
- Sep 6, 2013
- 3,418
- 1,980
Wa salaam,
Imeibuka tabia kama si mwenendo wa hovyo kwa wenye Mamlaka/Madaraka ama nyadhifa mbali mbali Nchini kukurupuka na kuchukua ama kutoa matamko au maamuzi 'Mkurupuko' ambayo mara nyingi wala haihitaji Elimu ya juu kubaini kuwa maamuzi HATUA zinazoamrishwa na Mamlaka hizo kuwa hazikidhi matakwa ya KISHERIA na hivyo kuwa batili.
Mara nyingi hatua ama maamuzi yaliyotolewa baadae hubatilishwa na Mamlaka za juu ya aliechukuwa hatua awali na matokeo ni Mamlaka za chini kuzodoka.
Hata hivyo, inapatokea kubatilishwa kwa tamko, amri au adhabu mara nyingi inakuwa tayari kuna watu waliohusiswa na kadhia husika wanaugulia Hasara ya Mali au pengine usumbufu usiokuwa wa lazima.
Kinachoshosha zaidi hakuna hatua za ama kufidiwa Hasara iliyoambatana na hatua ikiyobatilishwa au hata neno la Samahani tu kutoka upande wa Serikali.
Umefika wakati sasa huu ujima tuutupe Kapuni.
Kodi za wananchi zinaunguzwa Bila sababu za msingi na hakuna wa kuwajibika.
Fikiria: Anakamatwa Mtuhumiwa wa tuhuma nyepesi kama ya mashairi tu ya Wimbo Nje ya Dar,
Anasafirishwa kwa gharama za serikali hadi Dar,
Analazwa Lupango, Siku ya Pili,
Waziri anatangaza Msanii hana Hatia na inaagizwa aachiliwe huru, Hilo linatekelezwa Bila kuchelewa,
Unajiuliza ina maana hawa Waliomkamata walihemkwa na kuamua tu Msanii akamatwe kisha Mamlaka za juu ndio zieleze nini kosa?
Nimechefuliwa.
Hii Siasa ya hovyo, Kama si uongozi nyanya, Yaani majitu hayajiamini na yanachofanya.
Unayo haki wewe kama kiongozi ya kutekeleza Kazi zako kwa kufuata sheria unapocheza ngoma ya Waziri kwakuwa yeye kasema tu Msanii aachiwe na kama wewe mwanzo uliona ipo hoja ya kujibu inadhihirisha ni kwa kiasi gani wewe ni mzigo.
Haki iko wapi? Waziri au hata Rais ndio sheria? Vipi wewe unafanya Kazi kwa Uoga, Au unaendeshwa?
Hujitambui.
Na Mtu makini anaejitambua angeendelea na Charges.
Hakuna alie juu ya sheria,
Ni u-hovyo kumuachia mliejiridhisha kuwa na ana tuhuma za kujibu kwa Waziri amesema aachiliwe.
Ni ukweli ulio wazi ni kuwa,
Lugha Iliyotumika kwenye wimbo husika si rafiki kwa huo unaosisitizwa kila siku kuwa ni Utamaduni wetu Ila tu kwa kuwa wenyewe wameamua waliyoyaamua sawa twende hivyo hiyo watakavyo.
Hoja yangu hata hivyo inajikita kutengeneza nidhamu ya dhati na uwajibikaji pasi na shurti wala uoga.
Ni wazi wenye Mamlaka wengi hivi sasa wanatekeleza Majukumu yao kwa Uoga kama kukamata watu pasi kufuata taratibu na matokeo yake ni mzigo usio na faida kwa serikali.
Sasa, suluhisho, kuwawajibisha kwa kulipa gharama kwa Kiongozi mhusika alieamrisha kukamatwa kwa Huyu Msanii.
Na Huyu Msanii na wengine waliosababishiwa Hasara na usumbufu usio wa lazima nadhani ni wakati wa kui-Shitaki serikali sasa ili kudai fidia.
Kwa upande wa Serikali iwabane watendaji wake wakurupukao kufanya maamuzi yanayoingizia gharama ikiwezekana iwakate mishahara yao na kusitisha overnight za watendaji walipofuatilia kesi zote zisizo na kichwa wala miguu.
Haiwezekani unikamate Mkoani Nafanya yangu, Unisafirishe hadi Dar, Unilaze Selo, Kisha eti, Boss wako aseme 'Naona wimbo ni Mzuri' - Nuachieni, kisha mimi nakenua meno tu kutoka Selo.