Eti wanataka mahari ya Tshs. 2,000,000... kipindi hiki cha Magu...

baba anjela

JF-Expert Member
Mar 17, 2013
430
310
Hivi hizi familia nyengine zimelogwa..wazazi wanadi mahari ya 2,000,000... Katika maisha haya ya leo...

Baada ya kuwaomba wakashusha mpaka 1,800,000. Tukaomba kuondoka na kuileta hiyo pesa....siku nyengine.

Tulipofika nyumbani tukampigia simu huyo mke mtarajiwa, Tukamwambia , wewe unaijua kazi ya mumeo dereva ...hiyo pesa inatoka wapi...sasa kazi kwako kuwashusha..zilizopo hapa 400,000 tu na hapo wanafamilia tumeongeza 200,000 kutimiza 400,000.ikishindikana basi...

Cha kushangaza baada ya dakika kama kumi baba yake akapiga simu..wanangu leteni tu mlichonacho...

Sasa walikuwa wanatujaribu au... Ina maana mtoto wao akuwaeleza wazazi wake ukweli kuusu kipato cha mume wake mtarajiwa.

Wewe mume wako dereva...wewe mke kazi/biashara huna... Nyumba ya mumeo kapanga vyumba 2. Mahari 2,000,000. Wanawake elezeni ukweli nyumbani mnapotaka kupeleka wachumba nyumbani...
 
Acha gubu kama mke mwenza, wewe umeambiwa mpeleke laki 4 unachokaa kuilalamikia hiyo milioni 2 ni nini???!!!Hao wazazi wangekua na tamaa unafikiri wangekubali hiyo laki 4 yenu, afu thamani ya ule uchungu wa kuzaa watoto kisha wanabeba majina ya baba zao unaijua wewe? Hiyo laki nne yenu inaweza hata kulinganishwa na ule uchungu wanaoupata wakati wa kujifungua!!??
 
Hivi ukishamuoa ina maana huna msaada tena nyumbani kwa mke? Hivi ukishamuoa mkeo anavunja undugu na ukoo wake?? Hivi mama au baba wa mke wakiumwa hutakiwi kuwasaidia??
Mkuu ni vyema suala la mahari ileweke kuwa sio fidia ya matunzo wala si fidia ya kuzaa mtoto bali ni shukran tu, ni alama ya committment na si vinginevyo. Siungi mkono watu wanaopanga mahali kama vile wanawauza mabinti zao.
 
Kwani hao wengine hambao hawa kutolewa Mahari walijifungua bila uchungu..!???
 
Hivi ukishamuoa ina maana huna msaada tena nyumbani kwa mke? Hivi ukishamuoa mkeo anavunja undugu na ukoo wake?? Hivi mama au baba wa mke wakiumwa hutakiwi kuwasaidia??
Mkuu ni vyema suala la mahari ileweke kuwa sio fidia ya matunzo wala si fidia ya kuzaa mtoto bali ni shukran tu, ni alama ya committment na si vinginevyo. Siungi mkono watu wanaopanga mahali kama vile wanawauza mabinti zao.
Mkuu mahari ni utamaduni tu haina uhusiano na return ya kitu chochote, sema vijana mkishasoma soma mnaajidai kuanza kukosoa utamaduni
 
SERIKALI IWEKE KIMA CHA JUU CHA MAHALI.
kuna wengine mtoto wa kike asikilizwi wao wanaamua bila kujali wewe unafanya kazi au huna.
Hizi mahali zingeingizwa kwenye kundi la mila potofu...
 
Tuongee ule ukweli Mahari kubwa zipo kwa sisi wa Upande wa Ukristo kuliko wenzetu waislamu.

Mtu anaambiwa atoe mahari Milion 4 kisa eti bint amesoma mpaka Chuo kikuu, huku ni kumuuza bint yako na Sio heshima.

Mahari ni Shukrani tu na haitakiwi kuzidi Milioni 1 hiyo Milioni moja huwa hawatoi yote.
 
zama zimebadilika , me nadhan ifike wakati tusiwe kama tunakomoana hasa kwenye mambo ya msingi
Ukwel ni kwamba wanaume hasa waoaji wamekua ni wachache mno...!
Wito wangu kwa wazazi hasa wa mwanamke waliangalie sana suala la mahali maana kwa namna moja ama nyingne limewafamya mabinti wengi either wapigwe mimba kabla ya ndoa au wanyamyasike hasa pale kiwango cha mahali kimapokua kikubwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom