Eti wababe nao US, Russia na China waongozwe na Wabeijing akina Hayanga

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,958
7,512
Hii dunia ina tabu sana kusema kweli, na shida hizi zinakuja zaidi kwa vi nchi maskini ama kwa nchi zisizo na malengo yoyote ya kuikamata Dunia hii, kKwa kifupi wale waliyotayari kuendelea kuwa wanyonge wa wengine.

US wakili wa demokrasia alipata uhuru 1776, China ndiyo ulikofanyika mkutano wao wa Beijing huku wakisisitiza masuala ya wanawake, Russia mwenyewe ana karne yake naye anadunda.

Hawa vidume wana ramani zao juu ya ulimwengu huu na wanapambana kuwateka wengine (giants) kwa kila aina ya maendeleo hapa duniani, najaribu kujiuliza ni kwanini hawajathubutu kuongozwa na Wabeijing?

Ama kule kwao hawapo? Lakini majuzi tu hapa H. Clinton alitoka kupambania na akabwagwa na Mdemocratic mwenzie B. Obama. Katika hili nikiri wazi nalo liliniduwaza kidogo, kwamba wazungu wakaona aheri Mwafrika (mwanaume) na si Mzungu mwenzao (mwanamke).

Sasa ndugu zangu tuulizane, ni kwanini haya mataifa makubwa na na yenye mikakati Duniani hayako tayari kuongozwa na Wabeijing, kwani wao wanaona nini hasa? Na ni kwanini sisi tunaoonekana sukuma twende tusiyo na mikakati ndiyo tunazingatia zaidi Ubeijingi na Wabeijing hasa pale juu (☝)?

Nawatakia maandalizi mema na uvumilivu wa kutosha hapo 2025.
 
Hatujawahi kumchagua mbeijing zaidi ya matakwa ya kikatiba. Lakini tupo kwenye njia sahihi maana mpaka Sasa wabeijing wanaonesha wanaweza maana aliepo ANAUPIGA MWINGI SANA.
 
Ujerumani, Uingereza ambazo zilikutawala na zinakupa misaada zote zimeongozwa na wanawake
Marekani 2016 Hilary Clinton alikuwa nominated na chama chake kugombea Urais, na alipigiwa kura nyingi zaidi kuliko Trump sema mfumo wao wa kupata mshindi hatuangalii tu kura nyingi

Mkosoe Samia kwa utendaji wake sio jinsia yake, huyo jiwe mliyekuwa mnamuabudu ndio huyo huyo alimteua Samia mara mbili kuwa makamu wake akijua kabisa ni mwanamke na alijua katiba inasemaje
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Labda Hayanga wa kwao hatakuwa arembui mimacho tu na ilimu yake siyo ya QT vipande vipande!
 
Ujerumani, Uingereza ambazo zilikutawala na zinakupa misaada zote zimeongozwa na wanawake
Marekani 2016 Hilary Clinton alikuwa nominated na chama chake kugombea Urais, na alipigiwa kura nyingi zaidi kuliko Trump sema mfumo wao wa kupata mshindi hatuangalii tu kura nyingi

Mkosoe Samia kwa utendaji wake sio jinsia yake,
Ujerumani ukiondoa enzi ya ukoloni si taifa la sifa kama nilizozitaja kwa hizo nchi tatu, atabaki chini ya hao naye malengo ya kuikamata dunia hana.

Muingeleza unaona hadi walipo kwa sasa kila siku wanapindua meza ndani ya miaka michache ma PM 5, £ chali na bado hawawezi kukaa kapu moja na hao wababe watatu.

Hakuna anaye msema Sa100, tunajaribu kuweka mizania huru ili tujadiri hii mitizamo kwa kuusanisha mambo kadhaa na kama mama naye anaangukia humu basi tusiwafunge watu midomo kujadiri maana hili ni jukwaa huru. Na kama lipo zuri la mama haina shda nalo kuliweka ila usisahau mada hii inahusu wanawake katika wakubwa hawa watatu, ni kwanini wao hawakai pale juu kulikoni?
 
Wenye akili timamu hawawezi fanya huo ujinga hata siku moja nyie wajinga wazee wa copy and paste ndo mtasumbuka Sana
 
Back
Top Bottom