Mpunilevel
JF-Expert Member
- Sep 14, 2015
- 3,140
- 1,871
Kila Rais atumbuapo majipu yamekuwepo malalamiko toka kwa baadhi ya watu, na wanaharakati kwamba Rais hafuati sheria.
Nauliza ni sheria zipi? ambazo Rais Magufuli hafuati? Na hao wanaotumbuliwa mbona hawaendi mahakamani kulalamikia uonevu wanaotendewa?, ni haki yao kwa mujibu wa katiba.
Hapo nyuma, utawala wa awamu ya nne ya Jakaya Kikwete yalisemwa mengi, serikali dhaifu, haina uwajibikaji, ya wala rushwa, ina fanya kazi kwa mazoea, wanatumia tumbo kufikiri badala ya kichwa na mengineo mengi yenye kudhalilisha utawala huo.
Na waliokua mstari wa mbele kulalamika ni hawa wanaharakati na wanasiasa, ambao wameanza tena ukigeugeu baada ya Rais Magufuli kuyafanyia kazi malalamiko yao.
Hii inaonyesha jinsi binadamu tulivyo wanafiki.
Tuache Rais Magufuli afanye kazi na nyie wanaharakati kama mnaona Rais anavunja sheria kuwawajibisha wabadhirifu, basi nendeni mahakamani kwa niaba yao kuwatetea ili ukweli uwekwe wazi.
Naamini hamkua na machungu ya kile kibaya kilicho kua kinafanywa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu kwa wananchi bali ilikua ni hadaa tu.
Na hii inadhihirisha hao watumishi wabovu walikua ni jamaa zenu wa karibu na walicho pora kila wafadhili.
Rais Magufuli piga kazi watanyamaza tu. Najua maumivu makali wanapata ila hakuna jinsi.
Viva Rais Magufuli, kanyaga twende.