Eti chenge ajitangazia uadilifu!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti chenge ajitangazia uadilifu!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dmalale, Feb 14, 2011.

 1. d

  dmalale Member

  #1
  Feb 14, 2011
  Joined: Jun 7, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Chenge ajitangazia uadilifu Send to a friend Sunday, 13 February 2011 21:06 0diggsdigg

  [​IMG] Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serikali, Andrew Chenge, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu uchunguzi kuhusu kashfa ya rada uliofanywa na ofisi ya Kuchunguza Rushwa Kubwa ya Uingereza (SFO).Picha na Emmanuel Herman

  Raymond Kaminyoge
  ALIYEKUWA Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge, amejitangazia uadalifu akisema uchunguzi wa kashfa ya rada uliofanywa na Taasisi ya Kuchunguzi wa Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza , umegundua hahusiki, lakini alikimbia maswali ya waandishi.

  Wakati Chenge maarufu mzee wa vijisenti, akitumia mkutano wake na waandishi wa habari jana kujitangazia uadilifu huo, Ikulu kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe, imeshikwa na ganzi kuthibitisha au kukaa uadilifu huo.

  Chenge mwenyewe alisema:, " “Mimi ni muadilifu. nimefanya kazi katika awamu zote nne za uongozi wa nchi yetu..., hata nilipojiuzulu sikuwa na hofu wala mashaka ya kupoteza kazi.”

  Chenge akirejea na kujivunia historia ya utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na kufanya kazi wakati wa Serikali ya Mwalimu Julius Nyerere, alisisitiza uadilifu wake akisema:, "Kwa kuwa nilijiamini sikutenda kosa lolote katika kashfa hiyo ya rada nilisema iko siku ukweli utajulikana.”

  Mbunge huyo wa Bariadi Magharibi, alisema alitajwa kwenye kashfa ya rada iliyolitikisa Bunge la Uingereza, baada ya SFO kubaini alikuwa amehifadhi takribani Sh1.2 bilioni kwenye akaunti yake ya benki moja kisiwani Jersey, ambazo baadaye aliziita vijisenti.

  SFO ilibaini akaunti hiyo wakati ikifuatilia mzunguko wa fedha zilizonunua rada. “ Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa walikamilisha uchunguzi wao na kugundua kwamba hakuna ushahidi ulionihusisha na rushwa, uchunguzi umefanyika Uingereza na imeonekana sihusiki,”alizidi kujisafisha

  Kwa mujibu wa Chenge, makubaliano yaliyofikiwa mahakamani hapo ni kwamba SFO, haitamshtaki mtu yoyote kufuatia uchunguzi huo wa rada. “ Pia hakutakuwa na uchunguzi wala mashtaka ya aina yoyote kwa uongozi wa BAE Systems unaohusu mambo ya kibiashara yaliyofanywa kabla ya Februari 5, 2010,”alizidi kuanika hukumu hiyo huku akigoma kujibu maswali ya waandishi wa habari.

  Chenge mwanasiasa na mwanasheria mwenye kupenda kutumia maneno ya mzaha alisisitiza:, “ Kwenye ukweli uongo hujitenga, SFO na Takukuru wamefanya uchunguzi wa kina na matokeo yamedhihirisha mimi ni mtu safi.”

  Katika kutaka kujijengea imani kwa umma, Chenge aliwaomba Watanzania kuacha kushabikia mambo kabla hawajayafanyia utafiti wa kina. ``Rada ilinunuliwa na Serikali kwa manufaa na ulinzi wa nchi yetu na ununuzi wake ulizingatia sheria na taratibu zote za Serikali,’’alifafanua.

  Sakata la rada limekuwa likitikisa Bunge na Serikali ya Uingereza, hadi wakati flani kumfanya Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa nchi hiyo, Clare Short kujiuzulu huku aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Robin Kook, akimshambulia aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Tony Blair baada ya kuidhinisha BAE Systems kuuza rada hiyo kwa Tanzania wakati ni nchi maskini.

  Kwa upande wa hapa nchini, sakata hilo limekuwa likitikisa ambalo hivi karibuni Chenge alitoa kauli kama hiyo wakati akitangaza kuwania kiti cha uspika wa Bunge, lakini baadaye Uingereza, ikasema jalada hilo halikuwa limefungwa.
   
 2. K

  Kapeche Member

  #2
  Feb 14, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  anafikiri watanzania bado mbumbu. HATUDANGANYIKI!!!
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,766
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mimi naomba aniambie kale ka 1billion alikapata wapi! alikusanya mshahara wake kwa muda gani, na kama ni biashara zake kwanini aweke kwenye mabenk ya watu??? CHENGE JIBU MASWALI HAYO NIKUONE MWADILIFU!
   
 4. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Uchunguzi ulimalizika akaonekana msafi AU kuna deal wali strike kati ya SFO na BAE na Mahakama baada ya BAE kulipa fine , kwamba baada ya kulipa fine uchunguzi uishie hapo, na hakuna tena kushitaki mtu! Kwani BAE walijua madudu yatakayo fumuka!
   
 5. czar

  czar JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa ulitegemea aseme yeye sio mwadilifu? Hata mwizi umshike anaiba atakataa katakata. Akili ni nywele.
   
 6. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Siasa za mazoea mbaya sana....................
   
 7. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,869
  Likes Received: 2,814
  Trophy Points: 280
  Yaani hivi viongozi wa TZ hawana aibu eti? Unaita watu kwa nia ya kijsafisha! Aibu ya mwaka hii. Mbona akiulizwa kuhusu vile vijisenti hasemi? Na kwa nini aweke kwenye benki za nchi za nje asiweke TZ kama amevipata kwa njia halali? Hebu atuondolee uchuro hapa mwenda wazimu mkubwa huyu!!
   
Loading...