Nyumba kubwa unatetea Nchi yako hata kama ni uongo?
Uongo upi? nimejifunza patriotism baada ya kugundua kuwa watu wana chuki binafsi na Tanzania...na bila kujua watanzania wanawasaidia kufanikisha hilo...
Mimi kwenye kuponda naponda...penye uwongo wa wazi natetea...
Ndio maana nilimponda Tibaijuka kuchukua 1m USD japo ni wa nyumbani...lol...
Lakini sio watu fulani humu hakuna zuri wanaloliona kwa nchi yao...
Huko ni kukosa uzalendo....
Kuna siku wakaka wawili walikuwa wana discuss Tanzania mimi nawasikiliza kwa chati...
Mmoja mganda...mwingine wa Ethiopia...
Mganda anatutetea...wa Ethiopia anaponda...
Sikuchangia sababu hawakunikaribisha...tulikuwa kwenye trip moja ndefu walikuwa karibu yangu kwenye bus...nawajua wote ilikuwa ni group trip...
Yani yule mEthiopia alinishangaza sana...eti anashangaa Tanzania kuleta wanafunzi wa master kwa pesa yake kusoma chuo alichosoma yeye master...walisomea uchumi...
Nikajiuliza...nikasema huu sasa ni wivu...kama haoni umuhimu wa Tz kusomesha wachumi wake vyuo vya nje..yeye anafanya nini kwenye vyuo vya ughaibuni...what is the difference yeye kusomeshwa kwa scholarship na Tz kujisomeshea watu wake???
Nilitabasamu baada ya Mganda kumpa za uso....
Kama kuna investment ya kujivunia ni nchi kuweza somesha watu wake...nchi zilizotoka zime invest kwenye elimu...
Kuna tofauti kati ya kusoma kwa scholarship na kusomeshwa na nchi yako...the later ina maana kuwa umesomeshwa kwa lengo maalumu...
Malaysia wamefanya sana hili...na wanaendelea kufanya pamoja na kuwa na vyuo 'vizuri' huko kwao...