tarimemjini
Member
- Jul 10, 2025
- 71
- 142
Mgombea Ubunge jimbo la Tarime mjini kupitia ACT-Wazalendo amemuwekea pingamizi Mgombea wa CCM, Esther Nicholas Matiko pingamizi zito sana.
Pingamizi hili kungekuwa na utawala wa sheria Hakika Esther Matiko angeondolewa kuwa mgombea na angeshitakiwa kwa ubadhirifu wa mali za Umma.
Soma Pia: Esther Matiko amuwekea pingamizi mgombe wa ACT-Wazalendo Tarime Mjini
Tujitahidi kuipitia.
==================
Mimi, Jackson Ryoba Kangoye, mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Mjini kwa tiketi ya Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), ninawasilisha pingamizi hili kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Toleo la 2023, Sheria ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kanuni zake, pamoja na Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258, kupinga uteuzi wa Bi. Esther Nicholas Matiko kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Tarime Mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
1. Uanachama wa CHADEMA na Ubunge wa Viti Maalum (2020)
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, Esther Nicholas Matiko aligombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Tarime Mjini lakini hakupata ushindi. Baadaye alikula kiapo cha Ubunge mbele ya Spika wa Bunge kuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Hata hivyo, viongozi wa chama chake walikana kupeleka majina ya wabunge 19 wa Viti Maalum kwa ajili ya kuapishwa kutokana na kukataa na kususia matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
2. Kufutwa Uanachama na Maamuzi ya CHADEMA
Baada ya kuapishwa, Baraza Kuu la CHADEMA lilitoa maamuzi ya kumfukuza uanachama kutokana na kukiuka taratibu na kudhoofisha mamlaka ya chama. Kwa mujibu wa Ibara ya 71(1)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

HISTORIA NA MUKTADHA