JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,177
- 7,472
Video ya pili ni Bulaya baada ya kuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Mara, Juni 30, 2025.
KUTOKA KWA MARTIN MARANJA MMMKauli ya Ester Bulaya aliyoitoa Juni 11, 2023 alipohojiwa na Stanslaus Lambart kuhusu mustakabali wao (yeye na Wabunge wenzake 19) waliokuwa na Mgogoro na Viongozi wao ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Video ya pili ni Bulaya baada ya kuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Mara, Juni 30, 2025.
Day dream huwa hazitokeini haki yake ata mbowe anaeza enda chauma na lissu akaenda ccm
aya we kaaa apoDay dream huwa hazitokei
ulikuja kujua halima mdee atahama?Day dream huwa hazitokei
Usimwamini mwanamke na ndiyo maana Mungu alikataa kuwapa mamlaka wanawake kwa sababu ya ukigeugeu.Kauli ya Ester Bulaya aliyoitoa Juni 11, 2023 alipohojiwa na Stanslaus Lambart kuhusu mustakabali wao (yeye na Wabunge wenzake 19) waliokuwa na Mgogoro na Viongozi wao ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Video ya pili ni Bulaya baada ya kuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Mara, Juni 30, 2025.
Inasikitisha kwa kweliKUTOKA KWA MARTIN MARANJA MMM
Chunga, tamaa mbaya!
Picha hii nzuri sana, ilipigwa siku ya Jumatatu, 17.08.2020 mbele lango kuingia katika ofisi za Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Bunda.
Hii ni siku ambayo Ester Bulaya alikuwa amekwenda kurejesha fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Bunda Mjini. Ubunge ambao hakika, tulishinda.
Naonekana hapo nyuma. Uso wenye tabasamu. Nilikuwa Meneja (Campaign Manager) katika kampeni za Ester Amos Bulaya katika Uchaguzi Mkuu wa 2020
Timu yetu ya kampeni ilifanya kampeni za kisasa sana katika mitaa yote 88 ya Jimbo la Bunda Mjini. Mikutano ya hadhara na kampeni ya nyumba kwa nyumba.
Mchakato wote wa uchaguzi uliporwa na DOLA katili la CCM. Fomu za matokeo Na.24 wasimamizi walijaza usiku wa siku ya kupiga kura, ukumbi wa halmashauri.
Mawakala wote wa CDM wakaondolewa katika vituo vya kupiga kura. Saini wakajaza wasimamizi wenyewe. Mgombea, Esther Bulaya alikataliwa kukagua fomu.
Katika ngome yetu ya majumuisho, iliyokuwa katika Hoteli ya De Light, mawakala wetu walikuwa wanakuja bila matokeo, waliokuja na matokeo hayana saini.
Kwa majumuisho yetu, mgombe wangu, Esther Amos Bulaya alipata kura 31,129. Lakini, kura za mgombea wa CCM 13,258 akapewa mgombea wangu, Ester Bulaya.
Wakati wa kampeni, ngome yetu ya uchaguzi ilivamiwa usiku na OC-CID Bunda, na kuanza upekuzi bila kibali, majira ya saa 9 usiku. Walimkuta mgombea siku hiyo.
Wakatuhoji kila aliyekuwa ndani siku hiyo kwa kuonesha vitambulisho vyetu. Ambaye hakuwa na kitambulisho, walitaka kuondoka naye. Tukaleta noma sana.
Vijana wetu wa ulinzi na matangazo wakiwa katika matangazo ya mkutano wa kufunga kampeni, walivamiwa na polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya.
Wengine walifanikiwa kukimbia mlimani. Wakalala huko kwa siku tatu. Vijana wetu 13, walikamatwa, wakapewa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha (armed robbery).
Gari ya matangazo iliendelea kushikiliwa hadi baada ya uchaguzi. Siku ya kufunga kampeni tulitafuta vifaa vingine vya matangazo. Vilivyopo, vipo polisi Bunda.
Baada ya uchaguzi, siku ya matokeo, Ester Bulaya akakimbilia kujificha Musoma Mjini. Kwa kuwa kulikuwa na sekeseke la kuwakamata viongozi wa CHADEMA.
Ni wakati huo Polisi walimkamata Freeman Mbowe, Godbless Lema na Boniface Jacob, Dar es Salaam, kwamba wanaratibu maandamano kupinga matokeo
Mimi nilibaki Bunda kwa miezi mitatu nikishughulika hao vijana wetu 13 wa ulinzi watoke gerezani. Nisingeweza kuwaacha. Walikuwa ndugu zangu wakati wa kampeni.
Bunda siyo kwetu na siyo kwangu. Hapo ilibidi kuishi hotelini kwa muda wote huo. Kesi inamalizika, nikashughulikia gari na vifaa vya muziki Polisi.
Siku moja tukiwa Mahakamani Bunda, tukishughulika na kesi ya vijana wale 13, tunamuona Ester Bulaya akiwa gereji chini ya tenti anaapishwa kuwa mbunge.
Hakuwahi hata kunishirikisha kwamba anao mpango wa kuwa mbunge wa viti maalum. Nilishangaa tu ameibuka bungeni, Job Ndugai anamuapisha kuwa mbunge.
Nikaendelea kubaki Bunda. Baada ya siku 62, vijana wetu wote waliwaachia huru baada ya DPP kuleta ombi mahakamani hana nia ya kuendelea na kesi.
Polisi wakaachia gari. Vijana wetu wakashukuru. Kila mmoja akarejea kwao baada ya kusota kwa miezi miwilo na siku kadhaa gerezani wakimpambania Bulaya.
Wakakumbuka ile siku ambayo msafara wa CHADEMA ukikutana msafara wa CCM jioni baada ya mkutano na vita ya mawe na mapanga kuibuka. Watu walichanika.
Ester Bulaya amesahau, anajiunga na MaCCM, kutafuta ubunge ambao MaCCM yalitupora kwa watu wetu kuumizwa? Ni jambo baya. Lakini amerejea kwao.
Watu wetu walipigwa mapanga na kujeruhiwa, walipewa kesi zisizo na dhamana, wakaishi gerezani kwa muda mrefu ili awe mbunge, leo anajiunga na mbogamboga?
Haina noma #NoReformsNoElection
View attachment 3391485